Haya ni maandalizi ya kuvuka mwaka 2013 kuelekea mwaka 2014.
Yaani mkesha wa mwaka mpya.
SHILOH INTERNATIONAL MINISTRIES TANZANIA
Tuesday, December 31, 2013
Friday, December 27, 2013
Shiloh ni huduma ya
kinabii iliyoko nchini Tanzania katika mkoa wa Tanga inayosimamiwa na mtumishi
wa Mungu Nabii Frank Julius Kilawah
ambaye ni mwana wa Nabii Shepherd Bushiri wa nchini Malawi.
-Shiloh ni huduma iliyoanzishwa mwaka 2012 tarehe 11 mwezi wa 11 chini ya mtumishi wa Mungu nabii Frank
Julius Kilawah eneo la Mikanjuni kabla ya kuhamia katika ukumbi wa Majestic mahali ilipo kwa
sasa.
-Nabii Frank Julius Kilawah ni mtumishi wa Mungu aliyetokea mkoa
wa Iringa akiwa na wito wa Ki-Tume na Ki- Nabii ndani yake.Alikuja katika mkoa
wa Tanga ikiwa ni wito aliopewa na Mungu kwa ajili ya kuanzisha huduma hii
katika mkoa huu
-Shiloh ni huduma inayojishughulisha na maisha ya watu
ki-roho na ki-mwili.Tunaposema ki-roho tunamaanisha kuwa,tunafundisha
mafundisho ya biblia,maombi na maombezi,uponyaji unaotumia nguvu za
Mungu,unabii pia mafundisho ya jinsi kukua katika wokovu.Ki-mwili,ni huduma
inayojishughulisha na kuhudumia watoto yatima,wajane na watu wanaoishi katika
mazingira magumu kama watoto wa mitaani na wazee.
Kupitia huduma hii watu wengi wameona mabadiliko makubwa ya
ki-roho na ki-mwili,watu wengi wamekuwa wakitolewa unabii,wakipokea uponyaji na
matendo mengine makubwa ya Ki-Mungu.Nabii Frank Julius Kilawah amekuwa
akitumiwa na Mungu kwa namna ya ajabu sana,matendo makubwa ya Mungu
yamedhihilika kupitia yeye,watu wengi wamekuwa wakitoa shuhuda ya nini
kimetokea baada ya kuombewa na nabii Frank Julius Kilawah.
-Huduma ya Shiloh
imekuwa Baraka kubwa kwa watu wa mkoa wa Tanga na nchini nzima kwa ujumla na
kufanya watu wa mkoa huu wamtukuze Mungu aliye hai,Pia na kusababisha watu mataifa mengine kuja kumwabudu Mungu aliye hai
mahali hapa.
-Kupitia huduma hii,shuhuda nyingi zimetolewa na watu wakishuhudia matendo makubwa Mungu
aliyowatendea.Unabii ambao umekuwa ukitolewa na Nabii Frank Julius Kilawah
amefanyika msaada mkubwa katikati ya maisha ya watu walio wengi.Mungu amekuwa
akimtumia nabii Frank kwa ajili ya uponyaji wa watu na watu wametoa shuhuda
nyingi sana.
SOMA SHUHUDA HIZI.
1)Namshukuru Mungu
kwa kuniponya.Ni wiki moja sasa imepita tangu Nabii Frank Julius Kilawah
aliponiombea juu ya ugonjwa uliokuwa ukinisumbua kwa mda mrefu.Nilikuwa
nikisumbuliwa na VVU,midomo kubabuka,vidonda sehemu za siri vilivyokuwa
vikinisababisha kushindwa hata kutembea na kupata maumivu makali sana wakati
nikienda maliwato.Lakini kwa sasa nimepona ni mzima kabisa
2)Nilikuwa ninasumbuliwa na
ugonjwa wa Ukosefu wa Kinga Mwilini(UKIMWI) lakini baada ya kukutana na mtumishi wa Mungu nabii Frank
Julius Kilawah na kuniombea nimepona kabisa ugonjwa huo.
Ibada za hapa SHILOH pia zimekuwa zikihudhuliwa na viongizi
mbalimbali wa serikali,wakiwemo wakuu wa wilaya na mikoa na idara nyingine kama
TRA,maafisa wa jeshi la polisi na magereza.
-Tunamshukuru Mungu kwa hapa tulipo,kwani ni mwaka mmoja
sasa tangu tumeanza huduma hii hapa mkoa waTanga ila imekuwa ni huduma ya
mafanikio sana.Tulipoanza mwaka jana tulikuwa watu watatu hadi watano katika
ibada,ila sasa Mungu amekuwa akiongeza watu katika ibada siku hadi
siku.Tulianza tukiwa tunakaa chini ila tunamshukuru Mungu kwa kuwa hatukai
chini tena.
-Kulingana na jinsi
huduma ya SHILOH inavyozidi kukuwa napenda kutumia nafasi hii kukualika na
wewe katika ibada za hapa SHILOH zinazofanyika kwa siku tofauti
tofauti kila siku.Karibu sana Mungu
atasema na wewe kupitia mtumishi wake nabii Frank Julius
Kilawah.
SIKU ZA IBADA.
Ijumaa;-Miujiza,Uponyaji na Mafundisho
Muda;-Saa 9:30-1:00 Usiku
Jumamosi;-Urejesho wanafsi,Mafundisho na
Maombezi
Muda;-Saa 9:00-1:00 Usiku
Jumapili;-Asubuhi
Muda;-Saa 3:00-4:00 Maombi ya Kujijenga
Saa 4:00-5:00 Sifa na Kuabudu
Saa 5:00-6:00 Shuhuda
Saa 6:00-9:00 Maombezi na Baraka
kutoka kwa Nabii
Jumatatu;-Maombi Maalum(Special Service)
Muda;-Saa 9:30-1:00 Usiku
MAWASILIANO
Simu;0768 828 181
0653 992 274
Face book;Prophert Frank Julius Kilawah
Face book page; Shiloh International Ministry
Tanzania
Email;shilohministrytanga@gmail.com
Subscribe to:
Posts (Atom)