SHILOH INTERNATIONAL MINISTRIES TANZANIA

Tuesday, February 11, 2014

IMANI ILETAYO MAJIBU






IMANI
Imani ni nini?
     Imani ni ile hali ya kuamini jambo hata kama bado halijatokea ila  Unaamini ndani yako kuwa limeshatokea kwahiyo unaamini katika ulimwengu wa Roho tayari ni lakwako japo kuwa katika ulimwengu wa mwili bado halijatokea.
Waebrania 11:1 inasema “ Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo      yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.”
Anaposema IMANI ni kuwa na UHAKIKA maana yake ni lile Neno HAKIKA maana yake kuwa ndani yake hakuna shaka, na Naposema MAMBO YASIYOONEKANA maana yake ni jambo ambalo halijaonekana bado katika ulimwengu wa mwili ila lipo katika ulimwengu wa Roho na hakuna mtu mwingine aliyeliona zaidi ya kwako yani ni mafunuo ya kwako peke yako ambayo Mungu amekupa na anataka uyatoe katika ulimwengu wa Roho na uyalete katika ulimwengu wa mwili na kitu ambacho kitakusaidia uyatoe hayo maono yako ndani yako ni kwa njia ya Imani. Mfano unaona Nyumba ndani yako ( NAFSI MWAKO) ikiwa huna bado kiwanja sasa hapo ndipo unatakiwa utumie imani yako na hutakiwi kuona shaka hata kama kuna mambo ambayo yanakatisha tamaa katika maisha yako  na yanakupelekea unaona kuwa huwezi kufika katika ufunuo wako wewe hutakiwi kukata tamaa wala kuona shaka unachotakiwa ni kuwa na imani ile ile ya kwanza uliyoikuwa nayo.

Kuna aina mbalimbali za imani :-
A. IMANI  INAYOBEBA  NENO LA  MUNGU/ NENO  LA  MUNGU INAITUMIA  KUKUPA  MAJIBU.
Waebrani 11:3  “ kwa imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu…..”
Kazi ya imani iliyondani ya neno la Mungu ni kuumba vitu ambavyo havina chanzo, katika  Yohana 1:1 neno la Mungu linasema “ hapo mwanzo kulikuwa na neno na neno alikuwa Mungu….” Halafu mbele kidogo anasema “ vyote vilifanyika kwa huyo wala pasipo yeye hakikufanyika chochote kilichofanyika” 
NENO ni chanzo, na chanzo kilikuwepo ila  matokeo ya chanzo yalikuja kuonekana baada ya chanzo kubadilika na kuwa kitu kingine au tunawezakusema kuwa imani ya kwako itatoa matokeo pale ambapo utabadilisha mfumo na mtazamo wako wa ndani wa maisha ya kwako ya zamani.
Imani ni sawasawa na daraja, tunaweza kuliita  daraja kama Passover/crossover.
Na neno daraja linamaanisha kuna kipengele cha maisha yanayoishia sehemu flani ambayo hayawezi kuunganika na maisha yanayounganika mbele.
Tunaelewe kabisa kuwa kuna aina mbalimbali za madaraja kuna mwengine ni  membamba , pana , kubwa , dogo  ,bonde. Na tunaelewa kabisa kuna utofauti katika uvukaji wa hayo madaraja kutokana na jinsi yalivyo. Kuna eneo lengine inakulazimu utumie nguvu zako kwako mwenye ili uweze kuvuka ng’ambo ya pili, pia kuna eneo lengine ukivuka lazima uingie ndani pia unapovuka kuna baadhi ya madhara yanaweza kutokea,  mengine matokeo yake ni hapo kwa hapo mengine baada ya muda na wengine ukivuka vizuri hakuna madhara ambayo yanaweza kuyapata.
Wakati mwingine nafsi yako ndiyo imekuwa chanzo cha wewe kutokuwa na imani iliyo thabiti. Kwahiyo ifike mahali uibome nafsi yako maana imekusababisha kutokuwa na imani iliyothabiti na kwamba bila kuwa na kitu huwezi kupata.


Weka mkono katika kifua chako na omba maombi  haya:-

“NAFSI YANGU NAKUBOMOA KUANZIA LEO USITEGEMEE VITU VINAVYOONEKANA ILI UWE NA IMANI TEGEMEA VITU AMBAVYO HAVIPO ILI VIWEZE KUTOKEA MAANA NDIO KAZI YA IMANI KATIKA JINA LA YESU, AMEN”

            Itaendelea……..