SHILOH INTERNATIONAL MINISTRIES TANZANIA
Tuesday, November 10, 2015
NANI UMEMUWEKA KUWA NI MSIMAMIZI KATIKA BIASHARA YAKO NA MAISHA YAKO.
Zaburi 23:1 ''Bwana ndiye mchungaji wangu sitapungukiwa na kitu'' neno MCHUNGAJI ninaweza kusema ni kama MSIMAMIZI, anayesimamia kitu flani kwa ajili ya mtu kupata faida. Kwanini nasema kupata faida asingeweza kusema mchungaji na kutopungukiwa na kitu.
mfano: Mtu anayechunga ng'ombe hazichungi ili zipotee ila atazichunga na kuzitunza ili zizidi kuongezeka.
Ndivyo jinsi ilivyo katika maisha yako ya kila siku nani umemuweka kuwa msimamizi wa kazi yako, biashara , ndoa , uchumba, masomo , maisha yako ya kiroho nk.
Daudi anatuambia katika zaburi anasema Bwana ndiye mchugaji wake na kuna mahali pengine amesema " tangu amekuwa kijana mpaka mzee hajawahi kuina mwenye haki akiachwa " kwanini kwasababu katika maisha yake yote alimuweka Roho Mtakatifu kuwa msimamizi kwahiyo katika mambo yote alitembea akiwa chini ya uangalizi wa Roho Mtakatifu.
Kitendo cha wewe kumuweka Roho Mtakatifu kuwa msimamizi wa maisha yako uwe na uhakika hakuna kitu kitakachopungua haijalishi utapitia katika magumu gani ila bado Bwana atakutetea na utaona wema na fadhili zake kila siku.
Katika dunia hii tunayoishi wapo watu wanaoendesha biashara zao, kazi kwa kusimamiwa na majini, misukule ( watu waliokufa kabla ya wakati), hirizi nk na hao wazimamizi (roho ya shetani ) ndio zinawafanya waendelee katika biashara , kazi ( kupandishwa cheo na mshahara au kumiliki ofisi hata kama anacheo kidogo ) , ndoa ( limbwata ) na mambo mengine mengi.
Ila wakristo wachache ndio utakuta wanamtumia Roho Mtakatifu kama msaidizi wao na Ila wengi wao hawamtumii na bado utakuta mtu anajiita yeye ameokoka. Huwezi kusema umeokoka ikiwa huongozwi na roho wa Mungu katika maisha yako. Na ndio utakuta walokole wengi hawaendelei sio kwamba Mungu hawaoni wanavyopata shida ila siku waliyompokea roho mtakatifu na ndio siku waliomuacha roho mtakatifu hakukuwa na muunganiko tena. Au utakuta wanamtumia Roho Mtakatifu katika kiwango kidogo sana wakati maandiko yanatuambua katika Yohana 14:26 " lakini huyo msaidizi , huyo Roho Mtakatifu ...." unaelewa kabisa sikuzote msaidizi anafanya kazi kubwa kuliko mhusika au boss wake, ndivyo jinsi ilivyo utakapomuweka Roho Mtakatifu kama msaidizi ujue hakuna kitu chochote kitakachopotea, hakuna kushuka chini kiuchumi, hakuna magonjwa kwako, hakuna kulia kwako.
Wana wa Mungu ni wakati wa kubadilika ili uzidi kuongezeka lazima ubadilishe mfumo wa maisha yakouliyokuwa ukiishi mwanzo, muweke Roho Mtakatifu ili aweze kukusimamia katika njia zako ili uweze kuongezeka na kwenda katika njia inayopasa.
Mbarikiwe.
Subscribe to:
Posts (Atom)