NGUVU YA NENO KATIKA KINYWA CHAKO.
RUMI 10:9 “KWA
KINYWA MTU HUKIRI NA KWA MOYO MTU HUAMINI” UNAPOKIRI KITU MAANA YAKE UNAKUBALIANA NA KILE KITU ULICHOKISEMA.
Watu wengi wamekuwa ni watu wa kuongea maneno mengi
katika vinywa vyao na wamesahau kuwa ipo nguvu kubwa ya uumbaji ndani yake
katika kila NENO linalotoka katika kinywa chake (wanalolisema) haijalishi
umemaanisha au hakumaanisha hilo neno. Wanashindwa kuelewa kuwa shetani kazi
yake ni kufuatilia na kulibeba kila neno na kulifanyia kazi na wakati mwingine
kwa maneno yako mwenyewe anayafanya kuwa hati ya mashtaki mbele za Mungu..
Ukisoma Yeremia 1:11-12 “Tena neno la Bwana likamjia
kusema Yeremia waona nini?nikasema Naona ufito wa mlozi. Ndipo Bwana
akaniambia, umeona vema kwa maana ninaliangalia neno langu ili nilitimilize.” Hii
ni habari ambayo watu wengi mnaifahamu lakini leo kuna vitu nataka tujifunze
kupitia mistari hii. Ukisoma mistari hii kuna vitu vine vipo pale ambavyo
ningependa uvione.
>Waona
nini
>
Umeona vema
>Neno
langu
>
Nilitimize
A. WAONA
NINI
Si kwamba Mungu alikuwa haoni kitu
amabcho anamuuliza Yeremia bali alitaka kujua kitu anachokiona yeye na Yeremia
anakiona hivyo hivyo.
B. UMEONA
VEMA
Wakati mwingine unaweza kuona na
usielewe kitu unachokiona mathayo 13: 14, kwahiyo Mungu alipomwambia UMEONA
VEMA kwa maana nyingine naweza kusema umeona vizuri au nilichotaka ukiona
umekiona.
C. NENO
LANGU
Mpango naweza kusema ni mpango
ambao Mungu ameuweka katika maisha yako na ndio maana akasema NENO LANGU/
MPANGO WANGU katika maisha yako, kitu amabcho nimekikusudia wewe ufanye ila
nitakupa hilo neno (mpango) kama utakuwa tayari kuwa pamoja na mimi.
D. NILITIMILIZE
Kutimiliza kitu ni ile hali ya
umelianzisha jambo lakini bado
halijafikia mwisho sasa ndio unataka kulimalizia ndivyo jinsi ilivyo hata kwa
Mungu hawezi kulitimiliza jambo kama ndani ya hilo jambo hakuna neno (mpango )
wake na uwepo wake.
Hivi ni vitu ambavyo Mungu anasema nawe kila siku
katika maisha yako, ni kitu gani unaona ili aweze kutimiliza hicho kitu? Maandiko
yanatuambia Ezekieli alipoonyeshwa bonde
la mifupa mikavu, kwa macho ya damu na nyama aliona haiwezekani kwa ile mifupa
mikavu kuwa na uhai tena ,lakini MUNGU akamwambia itabirie hii mifupa
mikavu ipate kuishi.
Ndipo Ezekieli akatambua nguvu iliyopo katika KINYWA CHAKE, akaanza kutoa
unabii na kuitabiria ile mifupa, akaiambia ’’ enyi mifupa mikavu, lisikieni
neno la BWANA; BWANA MUNGU aiambia mifupa hii maneno haya; Tazama nitatia pumzi
ndani yenu, nanyi mtaishi .Nami nitatia mishipa juu yenu, nami nitaleta nyama
iwe juu yenu, na kuwafunika ngozi, nakutia pumzi ndani yenu nanyi mtaishi.’’ Maneno haya tunayapata katika kitabu cha (Ezekieli 37:1…..) Katika maandiko
haya tumeona, ni jinsi gani Ezekiel alivyoweza kutumia nguvu na uweza ulioko
ndani ya KINYWA CHAKE na
kuweza kuleta uhai tena. Na wewe mwana wa MUNGU nini ni kimekuwa mifupa mikavu
katika maisha yako? Yamkini ni ndoa ndio imekuwa mifupa mikavu itabirie nayo
itakuwa hai tena, au ni uchumi wako, afya yako, watoto wako, huduma yako, MUNGU
anakuambia leo simama na uvitabirie, maana kuna nguvu katika kutamka.
Vile unavyokiri ndivyo itakavyokuwa kwahiyo unakiri
nini kushindwa au kushinda? Nguvu ya MUNGU iko juu yako, badilisha yale yote
yanayoonekana kuwa yameshindikana na yatawezekana kupitia kinywa chako katika
Jina la YESU
KRISTO .
MAMBO YA MUHIMU
YA KUZINGATIA.
1. Chunga sana kinywa
chako na linda moyo wako
2. Jifunze kutamka yale
uyaamiyo na ushindi unaoutaka ,hata kama hali yako ya sasa haiendani na yale
uyatazamiayo. Usiache kusema....NAYAWEZA MAMBO YOTE KATIKA YEYE ANITIAYE NGUVU
3. Unaweza kuwatania
watu na ndoto zao lakini usifany utani na Bwana maana Mungu hataniwi
4. Na kila unapokiri kumbuka unatangaza vita hivyo
usiruhusu shetani akuletee mawazo mengine.
Usiache kukiri ushindi ndani mwako hata kama
mazingira hayaruhusu , Mithali 23:7 aonavyo mtu nafsi mwake ndivyo
alivyo . ndani ya moyo ndipo kuna kila kitu mawazo mazuri na mabaya,
moyo wako unapokuwa umejeruhika automatic utakuwa unaongea mambo ambayo hayana
ushindi na moyo unapokuwa na furaha ndipo utaongea mambo ya ushindi na ndio
maana biblia inasema linda sana moyo pia linasema neno la mungu na likae kwa wingi ndani mwenu. Neno la Mungu
litakapojaa kwa wingi ndani mwako ukiri, kusema kwako, kuwaza kwako na kuona
kwako kunakuwa tofauti utakuwa mshindi juu ya vitu vyote.
MAOMBI: ROHO
MTAKATIFU AKUSAIDIE KUCHUNGA KINYWA CHAKO KATIKA JINA LA YESU.