SHILOH INTERNATIONAL MINISTRIES TANZANIA

Monday, August 22, 2016

UMUHIMU WA NENO LA MUNGU KATIKA MAISHA YA MKRISTO

Msingi wa maisha ya mkristo ni Neno la Mungu, pasipo neno la Mungu katika maisha yako kama mkristo ni kama vile mwili ukikosa chakula unakufa ndivyo na  mtu aliye na Yesu bila neno lake lazima atakufa kiroho. Neno la Mungu ni chakula cha roho yako, huwezi kukua kiroho , huwezi kukua katika kumjua Mungu kwa undani zaidi wala imani yako haiwezi kuongezeka kama hautokuwa msomaji wa neno la Mungu.

Kama unataka kukutana wewe  binafsi  na Mungu hauwezi kukutana naye au kumpata kwenye magazeti au vitabu vya stori bali utampata na kukutana naye kwa kusoma neno lake ambalo ni biblia. Mithali 8:17 inasema" nawapenda wale wanipendao, na wale wanitafutao kwa bidii wataniona”  hivyo basi kumpenda Mungu peke yake haitoshi, bali bidii katika kusoma neno la Mungu na kulifanyia kazi ndio itakupeleka katika kumuona Mungu. Yeremia 1:11-12TENA NENO LA BWANA likanijia, kusema, Yeremia, waona nini? Nikasema, Naona ufito wa mlozi. Ndipo Bwana akaniambia, Umeona vema, kwa maana ninaliangalia NENO LANGU, ILI NILITIMIZE. 
Unaposhindwa kuona kile unachoelekezwa na Bwana lazima ufahamu kuna vitu utavikosa. Kwasababu atashindwa kutimiliza kile alichokikusudia, hivyo unapofika wakati Roho Mtakatifu nakufundisha na kusema na wewe unatakiwa uwe makini na kumuelewa.

Si kila neno la Mungu utamuona na kumsikia Mungu bali ndani ya neno la Mungu lenye pumzi yake ndipo utakutana naye. 2 Timotheo 3:16  inasema “Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki”  Utaweza kufahamu hilo kupitia Roho Mtakatifu maana yeye ndio mwalimu wetu na kiongozi wetu katika maisha yetu hapa duniani. Imeandikwa katika  1Wakorintho 2:13-14 “Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu. Nayo twayanena, si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho, tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni.” Hauwezi kufasili mambo ya rohoni kwa ma

Neno la Mungu ni silaha/ ngao dhidi ya kila adui anayeinuka katika maisha yako na ndio maana maandiko yanatuambia katika Waefeso 6:17b  “tweni upanga wa roho ambao ni neno la Mungu” na ukisoma  mathayo 4:1-4  imeandikwa “Kisha Yesu alipandishwa na Roho nyikani, ili ajaribiwe na Ibilisi. Akafunga siku arobaini mchana na usiku, mwisho akaona njaa. Mjaribu akamjia akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, amuru kwamba mawe haya yawe mikate. Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.  Yesu alimshinda shetani kwa neno unapokuwa na wingi wa neno la Mungu ndani yako hautakuwa na shida ya kuogopa adui maana neno ni silaha tosha katika maisha yako.  

Litaendelea.......