SHILOH INTERNATIONAL MINISTRIES TANZANIA

Tuesday, April 22, 2014

JINSI KIBALI KINAVYOWEZA KUKUINUA KATIKA MAISHA YAKO

  19/04/2014
SOMO:  KIBALI  (JINSI  YA KUKUBALIKA MBELE  ZA  WATU)

Na: Nabii Frank Julius Kilawah

Kibali  kimegawanyika katika sehemu kuu mbili, ya kwanza ni kukubalika kwa mtu ambaye hakupatii  faida ila wewe ndiye unamfaidisha, sehemu ya pili ni kukubalika pande zote mbili,hata kama  huna vigezo vya kukubalika katika eneo hilo.
Ukipata kibali kwa mtu ambaye unamfaidisha yeye binafsi hiyo ni sawa na bure,lakini Mungu akikupatia kibali unakwenda kukubalika katika maeneo ambayo katika hali ya kawaida  huna sifa ya kukubalika.
Kwa mfano; mtu anaweza kupata nafasi ya kufanya kazi Ikulu akiwa na kiwango cha chini kabisa cha elimu, katika kitengo ambacho kilipaswa kisimamiwe na mtu mwenye kiwango cha juu cha elimu lakini kutokana na kibali anapata nafasi hiyo.
Tukimwangalia Yusuph ambaye alikuwa mchunga kondoo,Mungu alimpatia kibali cha kuwa Waziri mkuu katika ile nchi ya Misri. kama ambavyo maandiko matakatifu yanavyosema katika kitabu cha, MWANZO 41:41” Farao akamwambia Yusufu, Tazama,nimekuweka juu ya nchi yote ya Misri.”
Watu wengi hulinda kibali cha mtu na Bibilia inasema alaaniwe mtu Yule amtegemeaye mwanadamu ,Mimi Baba yako Nabii  Frank Julius Kilawah natumia kibali cha macho ya Mungu,kuwa makini na ujichunguze ni aina gani ya kibali ulicho nacho.
Wanangu Mungu awapatie kibali kila mmoja cha kuondoa  roho ya umasikini,leo unakwenda kupokea muujiza na kupata majibu ya maombia yako kwa haraka,maana tunaongea na Mungu anaye jibu .maandiko yanasema mwenye kibali huwa na maamuzi, kama vileYusufu .
UTOKA 1:8,9 ,10 “Basi akainuka mfalme  mpya kutawala Misri, asiyemjua Yusuph, akawaambia watu wake, Angalieni, watu wa wana wa Israel ni wengi tena wana nguvu kuliko sisi. Haya, Na tuwatendee kwa akili, wasije wakaongezeka; tena, ikatokea vita, wao nao wasije wakashikamana na adui zetu na kupigana nasi, na kutoka katika nchi hii.”

Roho ya mungu iwe juu yenu leo wanangu naenda kuvunja kibali cha Farao nakupatia kibali cha Mungu alie  hai,katika kitabu cha KUTOKA 3:11,12  “Musa akamwambia Mungu,Mimi ni nani, hata niende kwa Farao, nikawatoe  wana wa Israeli watoke Misri?. Akasema, bila shaka mimi nitakuwa pamoja nawe; na dalili ya kuwa nimekutuma ndiyo hii; utakapo kuwa umekwisha kuwatoa hao watu katika Misri, mtamwabudu Mungu katika mlima huu.’’

No comments: