IJUMAA : 18 /04/2014
SOMO : KUZIKA MBEGU ILI ZIFUFUKE ZIKIWA NA KITU KINGINE NDANI YAKE.
Na: Nabii. Frank Julius Kilawah.
Roho wa Mungu amenipatia kibali kufundisha neno hili, Yeyote aliye tayari kubadilika na kuwa mtu mpya na kuinua kiwango cha imani yake ili kila atakalofanya atumie akili tofauti, maana sasa unakwenda kupanda mbegu ambayo utaivuna Yesu akiwa pamoja nawe.
Ijumaa kuu inaunganisha siku mbili muhimu zinazogongana katika ulimwengu wa Roho,jiandae kuwa mshindi kwa maana unakwenda kuwa kiumbe kipya na kuvuna sawasawa na mapando uliyoya panda.
YOHANA 4:36 “Naye avunaye hupokea mshahara, na kukusanya matunda kwa uzima wa milele , ili yeye apandae na yeye avunae wapate kufurahi pamoja”.
Maandiko yanasema kwa maana hapo neno hilo huwa kweli, Mmoja hupanda akavuna mwingine, maana mimi naliwatuma myavune yale msiyo ya taabikia;wengine walitaabika nanyi mmeingia katika taabu.
Ukilisimamia neno hili hutaingia katika taabu ya kuzika mbegu isiyofufuka na kitu kingine ndani yake,kwa maana kuvuna na kupanda vyote kwa pamoja vinamshuhudia Mungu wokovu.
Biblia takatifu inatuambia, Mungu aliupenda ulimwengu, haijasema aliwapenda wanadamu, mazingira yasikupe wasiwasi , kama ambavyo Daniel hakuwa na hofu hata alipokuwa kwenye tundu la Simba aliomba na Mungu alimjibu Papo hapo.
YOHANA 3:16-17 “kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee,ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.Maana Mungu hakumtuma mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu bali uokolewe katika yeye.
Maandiko yana yanazidi kutuweka wazi juu ya kila mmoja kuutambua uwepo wake mbele ya madhabahu ya Mungu, Amwaminiye yeye nhahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwasababu hakuliamini jina la mwana pekee wa Mungu.
Na leo nakwenda kukuweka karibu na uwepo wa Mungu, utakwenda kupata majibu mapya ya maombi yako, tunakwenda kulishusha giza tupate majibu ya mchana na unakwenda kubadilika kama Daniel, omba bila kuchoka ndio hadhina ya uzima wa milele.
YOHANA 3:19 “Na hii ndio hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni,na watu wakapenda giza kuliko nuru;kwa maana matendo yao yalikuwa maovu.Maana kila mtu atandaye mabaya huichukia nuru, wala haji kwenye nuru,matendo yake yasije yakakemewa.
No comments:
Post a Comment