Mnamo tarehe 17/04/2014 Bwana Michael alifika katika kanisa la Shiloh International Ministry Tanga kwa ajili ya kuombewa, na alipata neema ya kuonana na Nabii Frank Julius Kilawah akiwa katika ibada iliyokuwa inaendelea siku hiyo.
Nabii Frank Julius Kilawah aliweza kumpatia unabii juu ya afya yake Bwana Michael, Aliyekuwa akisumbuliwa na matatizo ya upasuaji ya kibofu cha mkojo ambacho kidonda chake kilikuwa hakija pona kwa ndani na kilichokuwa kinaendelea mpaka kwenye utumbo wa haja kubwa na kumpelekea maumivu makali.
Unabii huu ulithibitishwa na Bwana Michael kuwa nikweli alifanyiwa upasuaji wa kibofu cha mkojo.
Baada ya unabii kutoka kwa Mtumishi wa Mungu,kiganja chake cha mkono kilibadilika na kuwa chekundu kabla hajauweka kifuani mwa Bwana Michael, hii ilidhihirisha kuwa nguvu za Mungu tayari zilishuka kwaajili ya uponyaji. Na baada ya kuwekewa mkonokifuani mwa Bwana Michael mkono wa mtumishi uligeuka na kuwa katika hali yake ya kawaida.
Siku ya juma nne tarehe 22/04/2014 Bwana Michael alifika kanisani na kushuhudia juu ya matendo makubwa Mungu aliyo mtendea kupitia Mtumishi wake Nabii Frank Julius Kilawah.
Na huu ndio udhibitisho alioutoa Bwana Micheal kwa Mtumishi wa Mungu mbele ya waumini wa kanisa la Shiloh.
Nabii Frank . Unaendeleaje mzee na kuumwa?
Bwana Michael , Naendelea vizuri baba, Mungu ananibariki.
Nabii .Nakuona hata afya yako ipo vizuri sasa,
Bwana Michael. Ndio najisikia vizuri . Ila nina jeraha tu sasa hivi, kwasababu baada ya maombi siku ileile nilipofika nyumbani ile sehemu yenye mshono paliota jipu, na baada ya siku tatu lilipasuka.
Nabii Frank, sawa sasa kidonda kimesha pona?
Bwana Michael, akathibitisha kuwa kidonda kimepona.
TUNA MTUMIKIA MUNGU ALIYE HAI HAPA SHILOH INTERNATIONAL MINISTRY
KWA KUPITIA MTUMISHI WAKE NABII FRANK JULIUS KILAWAH.
KABLA YA MAOMBEZI
BAADA YA MAOMBEZI
No comments:
Post a Comment