SOMO:
NAFSI ILIVYO HARIBIKA
KWA VITU VIWILI.
Na: NABII FRANK
JULIUS KILAWAH.
Neno “nafsi “ linamaana ya mwili wa nje na ndani wa
mwanadamu, mbali na mwanadamu kuwa na
roho pia ni nafsi katika maana yake ya kawaida , neno “nafsi” linamaanisha “
uhai” ingawa zaidi ya hii maana kuu ,
Bibilia inazungumzia nafsi katka maana mbalimbali, na moja wapo ya hizi ni
nia ya mwanadamu kutenda dhambi.na nafsi zetu zime jeruhiwa na kuharibika
kwaajili hiyo.
Vitu viwili vilivyo haribu nafsi za watu, Moja nafsi inaharibika
kwa kitu unacho kisikia na cha pili ni kile kitu unacho kiona kwa macho ya
kwako na hukupaswa kukiona wala kukisikia kwa mana kitaharibu nafsi yako, Kwa maana hiyo hayupo mtu anaye weza kuibadilisha nafsi
yako zaidi ya yeye aliye ifanya nafsi kuwepo, ni Mungu pekee.hata mwanadamu
akibadilisha nafsi yako ataharibu ya nje
lakini ya ndani itaumia tu.
Wapo watu wengi nafsi zao zimeharibika na wamebaki
wakilalamika na kuwa na roho ya hasira, kupaniki, hawana stori nzuri za
kuongea,wana mchukia mtu kwa ghafla na hata
histori ya maisha yao imeharibika.
ZABURI 35:1 “Ee BWANA, utete nao wanaoteta nami, Upigane nao wanaopigana nami. Ushike
ngao na kigao, usimame unisaidie.Uutoe na mkuki uwapinge wanaonifuatilia,
Uiambie nafsi yangu, mimi ni wokovu wako”.
Maandiko yanaonyesha jinsii Daudi alivyo jigawanya kwenye
makundi mawili, la kwanza ni pale anapo sema Bwana pigana nao wanao pigana nami,
la pili amejiona kwamba anapigana na vita anavyo vipiga lakini nafsi yake
imenyamaza na haiwezi kumsidia vita
vinavyoendelea.ndipo Daudi alipo mwambia Mungu sema na nafsi yangu na uiambie
wewe ni wokovu wako. Ili mimi nipigane nje na nafsi ipigane kama ninavyo pigana mimi.
Ukisoma vizuri na kuelewa maneno ya Paulo utagundua kuna watu
wawili wa nje na ndani, wanje anachakaa na akichakaa anampatia nafasi wa ndani afanye upya kipindi cha
mabadiliko kinachofanyika kule ndani iliyule wa ndani awe mpya , nje ni lazima
kusinyae ni kwasababu Yule yupo gereji anafanyiwa kazi upya iliatokea na vita
ya kumsaidia wa nje.
Kama tunavyo soma na kuona wapo watu wawili wa ndani na nje, hivyo ni
muhimu sana kusikiliza nafsi yako inasema nini , maana unavyo sikia na kujiona
ni vitu viwili tofauti, na hakuna kitu kibaya katika maisha yako kama
kutokuelewa nafsi yako ipoje, hayupo mtu
anaye weza kuibadilisha nafsi yako zaidi ya yeye aliye itengeneza nafsi na kufa msalabani kwaajili yako.
ZABURI 35:4 “Waaibishwe, wafedheheshwe, wanaoitafuta
nafsi yangu. Warudishwe nyuma, wafadhaishwe, wanaonizuria mabaya. wawe kama
makapi mbele ya upepo , malaika wa
Bwana akiwafuatilia , maana bila sababu
wamenifichia wavu,, Bila sababu
wameichimbia shimo nafsi yangu”.
Kuokoka ni sawa na kuondoa nafsi ya kabila la kwenu na
utaichukuwa nafsi isiyo chakaa ya Yesu kristo, ndio itakaa huko ndani kwako, lakini katika kipindi hicho watatokea
watu wengi watasema wanachokisema lakini ndani
kwako jua yanafanyika mabadiliko makubwa. Nafsi yako ina kazi
ya kuzalisha na inaweza ikakata mawasiliano na Mungu wakati akili
zako bado zinawasiliana na Mungu, kwasababu usingeweza kutegemea kama
Daudi aliweza kumwambia Mungu azungumze
na nafsi yake.
ZABURI 35:9 “Na nafsi yangu itamfurahia BWANA, Na
kuushangilia wokovu wake”.
No comments:
Post a Comment