14/07/2014
SOMO: MACHO YA ROHONI
Na: NABII FRANK JULIUS
KILAWAH.
Macho ya rohoni .Ni macho ambayo yanauwezo wa kuona vitu
ambavyo kwa macho ya kawaida (nyama) hayawezi kuona ila mpaka uwe na macho haya,ila inatengemaea
unamtumikia Mungu gani, maana ukiwa unamtumikia Mungu utakuwa unaviona vya
kwake na Shetani utakuwa unaona vya kwake,ingawa macho haya yote yana uwezo wa
kuona vitu vyote vya gizani na vya
nuruni. lakini macho ya mungu yana nguvu ya kukuvusha zaidi kwa kila upande utakao
onyeshwa.
Umuhimu wa kuwa na macho ya rohoni, utakuwa katika ulimwengu
tofauti katika hali isiyokuwa ya kawaida kwako, kwasababu utaona vitu vilivyo
pita vya sasa na vinavyokuja mbele yako,
itakuwa rahisi katika maisha yako na kutambua nini unatakiwa kufanya sasa,
mfano wa kitu kilicho pita inawezekana kuna mahali ulikosea na baada ya kupata
macho ya rohoni ukajua ulipokosea ni rahisi kuenda mbele za Mungu na kuomba
msamaha,maana hata ulimi hauwezi kutamka kitu kama macho hayajaona , maandiko
yanasema jicho likiwa na giza mwili
hauwezi kuona kwamana jicho ndio linaweza kumsaidia kuona.
MWANZO
6:14,17 “Kwahiyo akapeleka huko farasi na
magari, na jeshi kubwa; wakafika usiku, wakauzingira mji ule pande zote.Hata
asubuhi na mapema mtumishi wake yule mtu wa Mungu alipoondoka,na kwenda
nje,kumbe! Panajeshi la watu, na farasi na magari,wameuzingira mji ule.mtumishi
wake akamwambia,Ole wetu! Bwana wangu,tufanyeje?Akamjibu, usiogope;maana
waliopamoja nasi ni wengi kuliko wale waliopamoja nao.Elisha akaomba akasema,Ee
Bwana,nakusihi mfumbue macho yake,apate kuona.Bwana akamfumbua macho yule
mtumishi; naye akaona; na tazama kile kilima kilikuwa kimejaa farasi na magari
ya moto yaliyomzunguka Elisha pande zote”.
Mungu anamacho? Kweli Mungu ana macho, maana maandiko
yanasema katika kitabu cha MWANZO 3,”Baada
ya Adamu kumuacha mke wake na kuwa mbali naye, na huyu mwanamke hakumuaga Adamu
lakini alikoelekea njia zote zina majina na Mungu alisha weka malaika katika
zile njia iliasiweze kula tunda,lakina nyoka aliweza kuwadanganya,na baada ya
kula wakafunguliwa macho, kwamaana ya kufunguliwa macho sikwamba hawakuwa na
macho, bali walikuwa nayo lakini kuna kitu kilikuwa kikisubiriwa kwa hamu
kikiingia ndani ya miili yao kitafungua macho waliyokuwa nayo na kama mungu
aliwanyima kwa muda ule wasione kitu, lakini aliwapatia macho ya kuona kitu
kingine wakati haya haja funguliwa”.
Baada ya kula tunda na kufunguliwa macho, adamu aliposikia
sauti ya Mungu alikimbia,Maandiko ya nasema alipoulizwa na Mungu, Kwanini
umejificha?akamjibu nipo uchi, Mungu akamwambia adamu umejuaje kama upo uchi
wakati sikuzote ulikuwa uchi na hujajiona na mimi niliyafunika macho yako
iliusijione upo uchi. kwamana umejua upo
uchi basi kutakuwa na mtu mwingine anaye fanana na mimi Mungu.
Adamu akamwambia Mungu umenipatia mwanamke bila kukuomba kwa hiyo
huyu mwanamke uliye nipati,amekwenda na amekutana na shetani wakaongea wakanipatia tunda akaniletea ndilo
ambalo lilinifungua macho nikaona nipo uchi. Maandiko yanasema Mungu alipo anza
kugawa adhabu Adamu alikuwa wa mwisho kupokea adhabu, wa kwanza alikuwa
mwanamke, wapili shetani adamu akawa wa tatu, maana alikuwa yupo kwenye namba ya tatu akijua baada ya namba
tatu ya Adamu kuna namba tatu ya Masia atakae kaa ndani yake.
Maandiko yanasema baaada ya Adamu kujijua yupo uchi akajisikia
aibu na yale macho yaliyo mwonyesha kuwa yupo uchi, yalikuja kwa aina yake kule ndani na kuanza kumuonyesha
vitu vingine tofauti, ambapo Mungu alikasirika na kuiziba njia ya kwenda
kwenye mti wa uzima, alipo ifunika hiyo njia, zile njia nyingine zote ambazo
yale macho yaliyo funguliwa yakawa yapo wazi kwa hiyo kila alichokuwa akikiona
ndicho kilichokuwa kikimwingia.
Ukitaka kuwa na macho ya rohoni, kwanza unatakiwa kuwa na
hekima ndani yako na msiri wa kila utakacho kiona ama kutokea mbele yako,pia unatakiwa
kujua aina ya vyakula unavyo kula kwa maana
sikila chakula na kila nyama unatakiwa kula,
KUTOKA 12:5 “Mwana kondoo wenu atakuwa hana ila,mume wa
mwaka mmoja; mtamtwaa katika kondoo au
katika mbuzi. Nanyi mtamweka hata siku ya kumi na nne ya mwezi ule ule;
na kusanyiko lote la Israel watamchinja jioni. Nao watatwaa baadhi ya damu yake
na kuitia miimo miwili na katika kizingiti cha juu katika zile nyumba watakazo
mla.Watakula nyama yake usiku ule ule,imeokwa motoni, pamoja na mkate usiotiwa chachu;tena
pamoja na mboga zenye uchungu; msiile mbichi, wala ya kutokoswa majini,bali
imeokwa moto;kichwa chake pamoja na miguu yake, na nyama zake za ndani”.
MWANZO 2.1” Mungu alipo umba kila kitu
akawaleta wanyama mbele ya Adamu iliaone atawaitaje, na alipo tokea nyati na
Adamu akasema ataitwa nyati na ika hivyo,Mungu hakupinga Kwasababu macho aliyokuwa akiyatumia Adamu
kipindi hicho atakacho kiona ndicho kitakacho tokea kwasababu yalikuwa ni macho
ya Mungu ndiyo yapo ndani yake. Macho aliyofunguliwa macho ya aibu kwahiyo
macho hayakuishia kuona uchi wa Adamu na Mke wa Adamu.na ndipo akaanza kuona
zaidi akaona uchi akakimbia akahitaji nguo akavaa lakini kwa adamu hazikuwa na
umuhimu.
Roho ikiwa kwenye mwili inaweza kumudu lakini mwili ukifa
nafsi yako ikiwa inatoka kwenye mwili ikienda kwenye ulimwengu wa roho na kukaa
na kujadilia kuhusu kesho utaona au kukuonyesho mambo gani yanatokea kesho,
lakini utakuja kufahamu kwamba roho inataka lakini nafsi haiwezi kuvuka kwa
sababu imezuia kwaajili nafsi ndiye mtu wa ndani na roho ya mtu inafanya kazi
kupitia nafsi na mwili.
Ili roho iweze kusema ni rahisi roho yako kuamini umepona na
roho yako ikaiambia nafsi mweleze mwili umepona na mwili atamwambia nafsi
kamwambia roho anaamini kwake amepona lakini mimi huku kwangu inje bado mwili
unauma, roho anamwambia nafsi kamwambie mwili imani bila matendo inakufa na
asimame sasa, kama mwili umeunganika na
nafsi uponyaji wa roho hauwezi kuja kwenye mwili mpaka nafsi iunganike na roho
ndipo mwili uwe sawa.kwamaana hazina ya mtu iliko ndio roho ilipo.
Mwanangu mimi Baba yako nataka ufike mahali huna kitu
kinakusumbu kwenye ulimwengu wa mwili kwa sababu nina kutengeneza na kukuweka
katika sehemu ambayo Mungu atajibu kwa upesi na kuwa na macho ya rohoni ambayo
yanaweza kuona kila kitu bila kuambiwa na mtu,maana ulimi hauwezi kutamka kitu
kama macho hayaja ona.