10/07/2014
AMEPONA
KANSA YA INI
Bi. Fatuma Mvungi kutoka Magaoni jijini Tanga
aliyemleta kijana wake Miraji Mvungi mwenye umri wa miaka 27, aliyekuwa akisumbuliwa
na kansa ya Ini. Alianza kusumbuliwa na tumbo kwa muda mrefu,na pia alilazwa
katika Hospitali zifuatazo, Hindumandali, Muhimbili, na baadaye walichukua
hatua ya kwenda katika Hospitali ya Ocean Road kwa ajili ya uchunguzi zaidi. Ambapo vipimo
vilionyesha kuwa anatatizo la kansa ya Ini.
Tarehe 04/07/2014, Bi. Fatuma Mvungi alichukua
hatua ya imani na kuweza kumleta kijana wake hapa kanisani ili aweze kukutana
na mtumishi wa Mungu Nabii Frank Julius Kilawa ambaye Mungu anamtumia kwa
viwango vikubwa vya kuponya matatizo mbalimbali katika maisha ya watu, kwa
kupitia jina la Yesu Kristo.
Nabii Frank Julius Kilawa alimuombea kijana
huyo na kuweza kupokea uponyaji wake papo hapo, kwa nguvu za Mungu
zilizoachiliwa juu na ndani yake zilimfanya kijana huyo aamke kutoka kwenye
godoro alilokuwa amelalia na kuanza kutembea.
Kitu ambacho kilimfanya kila mmoja amshangae
Mungu kwa matendo makubwa anayoyafanya kwa kupitia mtumishi wake Nabii Frank Kilawa.
"Kwa
kupigwa kwake sisi tumepona".
KABLA YA MAOMBEZI
BAADA YA MAOMBEZI
TUMSHUKURU MUNGU ANAYEMTUMIA MTUMISHI WAKE NABII FRANK JULIUS KILAWAH.
1 comment:
Ooh, that was very powerful. I really enjoy reading this blog. These are the might things that the church of today ought to experience! Hallelujah!
May God bestow his fresh oil and wisdom in his mission. Here in Morogoro, I'm so blessed to have such prophetic ministries as yours.
With these testimonies, the people that have gone through tough and hopeless situation, will find help in God.
Thank you Prophet.
Apostle Kuhanda J.N
Post a Comment