SHILOH INTERNATIONAL MINISTRIES TANZANIA

Tuesday, August 5, 2014

JIFUNZE KUHESHIMU NAFASI AMBAYO MUNGU AMEKUPATIA





JIFUNZE KUHESHIMU NAFASI AMBAYO MUNGU AMEKUPATIA.
Watu wengi wamekuwa wakidharau nafasi zao katika mahali ambapo Mungu amewaweka, na wakati mwingine inafika mtu kuacha kazi tu kwasababu nafasi ambayo aliyokuwa nayo yeye hakuitaka au kutoridhika au kutopandishwa cheo kwa muda ambao yeye aliona anastahili kupandishwa cheo. Na unashindwa kuelewa kuwa Mungu amekuweka mahali hapo kwa kusudi gani? Kama Mkristo lazima ujifunze kuishi kwa mtindo wa kumuuliza Mungu maswali  katika eneo  ulipo? Je huko mahali hapo kwa mpango na kusudi la Mungu? Na kama ndio  je? Ni kusudi gani  Mungu kukuweka mahali hapo na si mahali pengine na kama hapana je?  ni mahali gani ambapo yeye amekuandalia na kukusudia wewe uwepo?. ukienda kwa mtindo huu hauwezi kuacha kazi , biashara au jambo lolote la kwako unalolifanya kwasababu utaelewa kabisa umewekwa mahali pale kwa kusudi maalum la Mungu.

Neno la Mungu linasema katika  isaya  43:26 “ unikumbushe na tuhojiane ; eleza mambo yako, upate kupewa haki yako. Kama Mungu mwenyewe amesema njoo tuhojiane maana yake kuna vitu anataka kusikia kutoa kwako , na anaposema UPATE KUPEWA HAKI YAKO maana yake kuna haki nyingine haipatikani hivi hivi pasipo wewe kumwambia Mungu mfano umeonewa kazini  wenzako kila siku wanapadishwa cheo na msharaha halafu wewe uko katika kiwango kile kile cha mshahara na cheo,  ni wajibu wako uende mbele za Mungu na kumwambia haki yako unakosa mahali pale ili yeye awezekukutetea na ukapata haki yako.

Pia utakuta wapo watu wengine wanashindwa kuanzisha biashara au kuendeleza biashara zao kwanini kwasababu yupo mtu ambaye biashara yake ina jina kubwa au huyo mfanyabiashara jina lake ni kubwa na utakuta biashara yake haina ubora ila kinachomfanya biashara yake itoke ni jina lake ,  basi utakuta mtu anakata tamaa au anashindwa kuendelea kufanya biashra katika eneo hilo na kuenda kutafuta eneo lingine, swali la kujiuliza ni hili je?  utahama maeneo mangapi kwa kuogopa mtu biashara  yake inavyotoka.

Hupaswi kuogopa , lazima uelewe wakati unaanza biashara yako ni Roho Mtakatifu ndiye alisema na wewe kwahiyo hautofanya kwa akili zako bali utafanya kwa akili za Roho Mtakatifu na uwepo wake, kumbuka hakuna mtu Mungu anayemuwazia mabaya katika yeremia 29:11 inasema “ Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana ni mawazo ya amani wala si ya mabaya kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.” Kama Mungu amesema mwenyewe  hakuna mtu anayemuwazia mabaya maana yake hakuna mtu ambaye amepangiwa kufeli katika jambo lolote lile ambalo Mungu amemuagiza kufanya na akafanya sawasawa na  jinsi alivyomuagiza. Haleluyah..

            Ngoja tuangalie mfano mmoja wa mtu aliyeweza kuheshimu nafasi na mahali ambapo Mungu alimuweka.
1sam 16:1 “ BWANA akamwambia Samweli, hata lini utamlilia Sauli, ikiwa mimi nimemkataa asiwamiliki Israel? Ijaze pembe yako mafuta uende, nami  nitakupeleka kwa Yese, Mbethlehemi; maana nimejipatia mfalme katika wanawe.
Mungu anajaribu kumwambia Samweli asiendelee kumlilia mtu ambaye yeye tayari ameshamkataa na Roho yake haipo pamoja naye   na anajaribu kumuelekeza mahali pengine ambapo amejipatia mfamle huko, kuna kitu nataka uone Sauli ndiye alikuwa ni mfame katika nchi ya Israel na alikuwa hodari sana na maarufu kwasababu ya uwezo wake wa kupigana vita na kumcha Bwana, siku alipomkosea Bwana ndipo Mungu alipoamua kumuinua Mfalme mwingine japokuwa Sauli bado alikuwa mfalme ila uwepo wa Bwana haukuwa pamoja naye kwanini kwasababu tayari Mungu amemwambia Samweli nimejipatia mfalme mwingine.Kama Mungu alivyoweza kumchagua  Daudi  ikiwa Sauli bado alikuwa  ni mfalme  basi haina sababu ya wewe kuendelea kuogopa  kufanya biashara yako kwasababu huwezi kujua Mungu ameacha kuwabariki watu wangapi na amekuchagua wewe , huwezi kujua pia ameinua wateja wangapi kuja kwako. Daudi hakujua ni nini kinaendelea ila Mungu alijua ni kwanini alimuweka mahali pale kuchunga kondoo za kwako kwasababu Mungu alimpitisha katika shule ya kumuuwa dubu na simba kwa mikono yake ila yamkini Daudi hakujua ni kwanini yuko mahali pale ila baada ya kukutana na goliati ndipo Daudi aliweza kugundua kwanini Mungu alimuweka mahali pale kwanza na sehemu nyingine. Tatizo watu wengi kinachowafanya wakate tamaa ni kutokana na namna wanavyoangali nje  tofauti na jinsi Mungu anavyoaangalia ,

 Wakati mwingine mtu ameweka imani yake katika jambo flani na lile jambo linapokuja tofauti na yeye alivyodhani utakuta anakata tamaa na anashindwa kujua ni kitu gani afanye? Kumbuka wanafunzi wa Yesu walipoona Yesu ametuliza upepo Yesu aliwauliza Iko wapi Imani yenu? Wao walichojibu walimwambia Bwana tuongezee Imani, hawakusema nimekataa tamaa kwanini kwasababu kuna 
jambo/mambo mengine ambayo yanakuja juu ya kiwango chako cha Imani, sasa wewe huwapaswi kukata tamaa wala kulia unachotakiwa ni kumwambia Yesu niongezee Imani katika hilo jambo na wala si dhambi kuomba kuongezewa Imani. Nafasi au mahali ambapo Mungu amekuweka usiidharau kwasababu katika nafasi hiyihiyo ndogo ndipo Mungu anapoenda kukuinua, kumbuka hakuna vitu vikubwa vilivyoanza vikubwa vitu vyote vikubwa vimetokana na vidogo hivyo paheshimu heshimu mahali hapo huku ukiwa na bidii katika kazi yako na kumuomba Mungu kusudi lake likasimame mahali hapo.
                             
                   
       UBARIKIWE


 JOSHUA  1:5 HAPATAKUWA NA MTU YEYOTE ATAKAYEWEZA KUSIMAMA MBELE YAKO SIKU ZOTE ZA MAISHA YAKO”


           

No comments: