SHILOH INTERNATIONAL MINISTRIES TANZANIA

Monday, August 22, 2016

UMUHIMU WA NENO LA MUNGU KATIKA MAISHA YA MKRISTO

Msingi wa maisha ya mkristo ni Neno la Mungu, pasipo neno la Mungu katika maisha yako kama mkristo ni kama vile mwili ukikosa chakula unakufa ndivyo na  mtu aliye na Yesu bila neno lake lazima atakufa kiroho. Neno la Mungu ni chakula cha roho yako, huwezi kukua kiroho , huwezi kukua katika kumjua Mungu kwa undani zaidi wala imani yako haiwezi kuongezeka kama hautokuwa msomaji wa neno la Mungu.

Kama unataka kukutana wewe  binafsi  na Mungu hauwezi kukutana naye au kumpata kwenye magazeti au vitabu vya stori bali utampata na kukutana naye kwa kusoma neno lake ambalo ni biblia. Mithali 8:17 inasema" nawapenda wale wanipendao, na wale wanitafutao kwa bidii wataniona”  hivyo basi kumpenda Mungu peke yake haitoshi, bali bidii katika kusoma neno la Mungu na kulifanyia kazi ndio itakupeleka katika kumuona Mungu. Yeremia 1:11-12TENA NENO LA BWANA likanijia, kusema, Yeremia, waona nini? Nikasema, Naona ufito wa mlozi. Ndipo Bwana akaniambia, Umeona vema, kwa maana ninaliangalia NENO LANGU, ILI NILITIMIZE. 
Unaposhindwa kuona kile unachoelekezwa na Bwana lazima ufahamu kuna vitu utavikosa. Kwasababu atashindwa kutimiliza kile alichokikusudia, hivyo unapofika wakati Roho Mtakatifu nakufundisha na kusema na wewe unatakiwa uwe makini na kumuelewa.

Si kila neno la Mungu utamuona na kumsikia Mungu bali ndani ya neno la Mungu lenye pumzi yake ndipo utakutana naye. 2 Timotheo 3:16  inasema “Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki”  Utaweza kufahamu hilo kupitia Roho Mtakatifu maana yeye ndio mwalimu wetu na kiongozi wetu katika maisha yetu hapa duniani. Imeandikwa katika  1Wakorintho 2:13-14 “Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu. Nayo twayanena, si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho, tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni.” Hauwezi kufasili mambo ya rohoni kwa ma

Neno la Mungu ni silaha/ ngao dhidi ya kila adui anayeinuka katika maisha yako na ndio maana maandiko yanatuambia katika Waefeso 6:17b  “tweni upanga wa roho ambao ni neno la Mungu” na ukisoma  mathayo 4:1-4  imeandikwa “Kisha Yesu alipandishwa na Roho nyikani, ili ajaribiwe na Ibilisi. Akafunga siku arobaini mchana na usiku, mwisho akaona njaa. Mjaribu akamjia akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, amuru kwamba mawe haya yawe mikate. Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.  Yesu alimshinda shetani kwa neno unapokuwa na wingi wa neno la Mungu ndani yako hautakuwa na shida ya kuogopa adui maana neno ni silaha tosha katika maisha yako.  

Litaendelea.......


Wednesday, May 25, 2016

NGUVU YA NENO KATIKA KINYWA CHAKO.

RUMI 10:9  “KWA KINYWA MTU HUKIRI NA KWA MOYO MTU HUAMINI” UNAPOKIRI  KITU MAANA YAKE UNAKUBALIANA NA KILE KITU ULICHOKISEMA.
Watu wengi wamekuwa ni watu wa kuongea maneno mengi katika vinywa vyao na wamesahau kuwa ipo nguvu kubwa ya uumbaji ndani yake katika kila NENO linalotoka katika kinywa chake (wanalolisema) haijalishi umemaanisha au hakumaanisha hilo neno. Wanashindwa kuelewa kuwa shetani kazi yake ni kufuatilia na kulibeba kila neno na kulifanyia kazi na wakati mwingine kwa maneno yako mwenyewe anayafanya kuwa hati ya mashtaki mbele za Mungu..
Ukisoma Yeremia 1:11-12 “Tena neno la Bwana likamjia kusema Yeremia waona nini?nikasema Naona ufito wa mlozi. Ndipo Bwana akaniambia, umeona vema kwa maana ninaliangalia neno langu ili nilitimilize.” Hii ni habari ambayo watu wengi mnaifahamu lakini leo kuna vitu nataka tujifunze kupitia mistari hii. Ukisoma mistari hii kuna vitu vine vipo pale ambavyo ningependa uvione.
>Waona nini
> Umeona vema
>Neno langu
> Nilitimize

      A.    WAONA NINI
Si kwamba Mungu alikuwa haoni kitu amabcho anamuuliza Yeremia bali alitaka kujua kitu anachokiona yeye na Yeremia anakiona hivyo hivyo.

        B.   UMEONA VEMA
Wakati mwingine unaweza kuona na usielewe kitu unachokiona mathayo 13: 14, kwahiyo Mungu alipomwambia UMEONA VEMA kwa maana nyingine naweza kusema umeona vizuri au nilichotaka ukiona umekiona.

      C.  NENO LANGU
Mpango naweza kusema ni mpango ambao Mungu ameuweka katika maisha yako na ndio maana akasema NENO LANGU/ MPANGO WANGU katika maisha yako, kitu amabcho nimekikusudia wewe ufanye ila nitakupa hilo neno (mpango) kama utakuwa tayari kuwa pamoja na mimi.

D. NILITIMILIZE
Kutimiliza kitu ni ile hali ya umelianzisha jambo  lakini bado halijafikia mwisho sasa ndio unataka kulimalizia ndivyo jinsi ilivyo hata kwa Mungu hawezi kulitimiliza jambo kama ndani ya hilo jambo hakuna neno (mpango ) wake na uwepo wake.

Hivi ni vitu ambavyo Mungu anasema nawe kila siku katika maisha yako, ni kitu gani unaona ili aweze kutimiliza hicho kitu? Maandiko yanatuambia Ezekieli alipoonyeshwa  bonde la mifupa mikavu, kwa macho ya damu na nyama aliona haiwezekani kwa ile mifupa mikavu kuwa na uhai tena ,lakini MUNGU akamwambia itabirie hii mifupa mikavu ipate kuishi. 

Ndipo Ezekieli akatambua nguvu iliyopo katika KINYWA CHAKE, akaanza kutoa unabii na kuitabiria ile mifupa, akaiambia ’’ enyi mifupa mikavu, lisikieni neno la BWANA; BWANA MUNGU aiambia mifupa hii maneno haya; Tazama nitatia pumzi ndani yenu, nanyi mtaishi .Nami nitatia mishipa juu yenu, nami nitaleta nyama iwe juu yenu, na kuwafunika ngozi, nakutia pumzi ndani yenu nanyi mtaishi.’’ Maneno haya tunayapata katika kitabu cha (Ezekieli 37:1…..) Katika maandiko haya tumeona, ni jinsi gani Ezekiel alivyoweza kutumia nguvu na uweza ulioko ndani ya KINYWA CHAKE na kuweza kuleta uhai tena. Na wewe mwana wa MUNGU nini ni kimekuwa mifupa mikavu katika maisha yako? Yamkini ni ndoa ndio imekuwa mifupa mikavu itabirie nayo itakuwa hai tena, au ni uchumi wako, afya yako, watoto wako, huduma yako, MUNGU anakuambia leo simama na uvitabirie, maana kuna nguvu katika kutamka.

Vile unavyokiri ndivyo itakavyokuwa kwahiyo unakiri nini kushindwa au kushinda? Nguvu ya MUNGU iko juu yako, badilisha yale yote yanayoonekana kuwa yameshindikana na yatawezekana kupitia kinywa chako katika Jina la YESU KRISTO .

MAMBO YA MUHIMU YA KUZINGATIA.
1. Chunga sana kinywa chako na linda moyo wako
2. Jifunze kutamka yale uyaamiyo na ushindi unaoutaka ,hata kama hali yako ya sasa haiendani na yale uyatazamiayo. Usiache kusema....NAYAWEZA MAMBO YOTE KATIKA YEYE ANITIAYE NGUVU
3. Unaweza kuwatania watu na ndoto zao lakini usifany utani na Bwana maana Mungu hataniwi
4. Na kila unapokiri kumbuka unatangaza vita hivyo usiruhusu shetani akuletee mawazo mengine.
Usiache kukiri ushindi ndani mwako hata kama mazingira hayaruhusu , Mithali 23:7 aonavyo mtu nafsi mwake ndivyo alivyo . ndani ya moyo ndipo kuna kila kitu mawazo mazuri na mabaya, moyo wako unapokuwa umejeruhika automatic utakuwa unaongea mambo ambayo hayana ushindi na moyo unapokuwa na furaha ndipo utaongea mambo ya ushindi na ndio maana biblia inasema linda sana moyo  pia linasema neno la mungu na likae kwa wingi ndani mwenu. Neno la Mungu litakapojaa kwa wingi ndani mwako ukiri, kusema kwako, kuwaza kwako na kuona kwako kunakuwa tofauti utakuwa mshindi juu ya vitu vyote.

MAOMBI:  ROHO MTAKATIFU AKUSAIDIE KUCHUNGA KINYWA CHAKO KATIKA JINA LA YESU.




Tuesday, November 10, 2015

NANI UMEMUWEKA KUWA NI MSIMAMIZI KATIKA BIASHARA YAKO NA MAISHA YAKO.

   
   Zaburi 23:1 ''Bwana ndiye mchungaji wangu sitapungukiwa na kitu'' neno MCHUNGAJI ninaweza kusema ni kama MSIMAMIZI, anayesimamia kitu flani kwa ajili ya mtu kupata faida. Kwanini nasema kupata faida asingeweza kusema mchungaji na kutopungukiwa na kitu.
     mfano: Mtu anayechunga ng'ombe hazichungi ili zipotee ila atazichunga na kuzitunza ili zizidi kuongezeka.

Ndivyo jinsi ilivyo katika maisha yako ya kila siku nani umemuweka kuwa msimamizi wa kazi yako, biashara , ndoa , uchumba, masomo , maisha yako ya kiroho nk.
Daudi anatuambia katika zaburi anasema Bwana ndiye mchugaji wake na kuna mahali pengine amesema " tangu amekuwa kijana mpaka mzee hajawahi kuina mwenye haki akiachwa "  kwanini kwasababu katika maisha yake yote alimuweka Roho Mtakatifu kuwa msimamizi kwahiyo katika mambo yote alitembea akiwa chini ya uangalizi wa Roho Mtakatifu.

Kitendo cha wewe kumuweka Roho Mtakatifu kuwa msimamizi wa maisha yako uwe na uhakika hakuna kitu kitakachopungua haijalishi utapitia katika magumu gani ila bado Bwana atakutetea na utaona wema na fadhili zake kila siku.

Katika dunia hii tunayoishi wapo watu wanaoendesha biashara zao, kazi kwa kusimamiwa na majini, misukule ( watu waliokufa kabla ya wakati), hirizi nk na hao wazimamizi (roho ya shetani ) ndio zinawafanya waendelee katika biashara , kazi ( kupandishwa cheo na mshahara au kumiliki ofisi hata kama anacheo kidogo ) , ndoa ( limbwata ) na mambo mengine mengi.

Ila wakristo wachache ndio utakuta wanamtumia Roho Mtakatifu kama msaidizi wao na Ila wengi wao hawamtumii na bado utakuta mtu anajiita yeye ameokoka. Huwezi kusema umeokoka ikiwa huongozwi na roho wa Mungu katika maisha yako. Na ndio utakuta walokole wengi hawaendelei sio kwamba Mungu hawaoni wanavyopata shida ila siku waliyompokea roho mtakatifu na ndio siku waliomuacha  roho mtakatifu hakukuwa na muunganiko tena. Au utakuta wanamtumia Roho Mtakatifu katika kiwango kidogo sana wakati maandiko yanatuambua katika Yohana 14:26 " lakini huyo msaidizi , huyo Roho Mtakatifu ...."  unaelewa kabisa sikuzote msaidizi anafanya kazi kubwa kuliko mhusika au boss wake, ndivyo jinsi ilivyo utakapomuweka Roho Mtakatifu kama msaidizi ujue hakuna kitu chochote kitakachopotea, hakuna kushuka chini kiuchumi, hakuna magonjwa kwako, hakuna kulia kwako.

Wana wa Mungu ni wakati wa kubadilika ili uzidi kuongezeka lazima ubadilishe mfumo wa maisha yakouliyokuwa ukiishi mwanzo, muweke Roho Mtakatifu ili aweze kukusimamia katika njia zako ili uweze kuongezeka na kwenda katika njia inayopasa.

Mbarikiwe.

Monday, March 16, 2015

NGUVU YA SADAKA MBELE ZA MUNGU



SADAKA
 Neno SADAKA ni neno ambalo si geni masikioni mwa watu wengi na lina maana nyingi sana, nitatoa maana kama tatu hivi za neno sadaka.  Na zipo aina nyingi za sadaka kuna fungu la kumi, limbuko , sadaka ya shukrani na nk. Leo tutaangali sadaka kwa ujumla, Nguvu ya sadaka unapotoa katika Uwepo wa Mungu

Sadaka ni sehemu moja wapo ya kumuabudu Mungu, mwanzo 22:5  "Ibrahimu akawaambia vijana wake , kaeni hapa pamoja na punda , na mimi na kijana tutakwenda kule TUKAABUDU na kuwarudia tena"
Sadaka ni "kuonyesha upendo wako kwa Mungu" au unaweza kusema Sadaka ni "ushirika wetu katika kazi ya Mungu" 
Mungu aliweza kurudisha majira mapya katika nchi baada ya Nuhu kutoa sadaka. Hatuoni mahali ambapo Mungu amemuangizia/amemwambia Nuhu atoe sadaka au atengeneze madhabahu kwa ajili ya kumtolea Mungu sadaka kama alivyokuwa akiwaangiza baadhi ya watumishi wengine mfano: Musa aliagizwa awaambie wana wa Israel watoe sadaka au Ibrahimu amtoe mwanae wa pekee Isaka.
Swali la kujiuliza ni kitu gani kilimfanya Nuhu amtolee Bwana sadaka? Hatuoni Mungu akiongea na Nuhu baada ya kutoka ndani ya safina na wala biblia haituambi Nuhu alichukua muda gani tangu atoke ndani ya safina Mungu aliongea naye tena, inachotuambia ni Nuhu mara baada ya kutoka ndani ya safina alimjenge Bwana madhabahu na kumtolea sadaka ya kuteketezwa na iliyompelekea Mungu kufanya jambo jipya, Mungu anarudisha majira mapya katika nchi, na kumpa kutawala na kumiliki juu ya vitu vyote vya dunia hii yeye pamoja na watoto wake Nuhu. 
Kuna kitu lazima ujifunze wakati mwingine unashindwa kupokea Baraka zako kwanini,kwasababu haumtolei Mungu katika kiwango kinachompendeza na mahali ambapo hapana uwepo wake,Watu wengi tumetoa sadaka zetu katika hali ya mazoea,desturi na taratibu za ibada,kujilazimisha wakati mwingine hata kutaka kuonekana na watu unashindwa kuelewa nguvu iliyopo ndania ya sadaka? kwasababu unapotoa sadaka pasipo uwepo wa Mungu mahali hapo ujue sadaka yako haitaleta majibu ila ukitoa sadaka yako mahali ambapo kuna uwepo wa Mungu huwa majibu hayachelewi mfano kwa Nuhu, Ibrahimu

Tunaona katika mwanzo 8:21-22 Mungu amesikia harufu nzuri ya sadaka ya Nuhu ambayo hiyo sadaka imemlazimisha Mungu ajisemeshe(ajiapize) mwenyewe moyoni mwake au kwa lugha nyingine tunaweza kusema sadaka ya Nuhu ilimlazimisha Mungu kufanya kitu hata kama Mungu hakukipanga kukifanya.
Mwanzo 8:21b “WALA SITAIPIGA TENA BAADA YA HAYO KILA KILICHO HAI KAMA NILIVYOFANYA SITAILAANI NCHI……” Kutokana na andiko la mwanzo Mungu anaposema sitailaani nchi kwa lugha nyingine tunaweza kusema Mungu alikuwa na kawaida ya kuilaani nchi au kuna laana iliyokuwa inakuja mbele kwa ajili ya nchi kutomsaidi kwa kitu chochote atakachokifanya juu yake, ila kwa ajili ya na sadaka ya Nuhu, Mungu alijiapiza mwenyewe moyoni kuwa hatafanya hivyo tena, na anaposema TENA maana yake milele hakitakuwepo au hakitajirudia. Kwahiyo sadaka inanguvu ya kubadilisha kitu chochote unachokitaka na ndio maana wapo watu wanaoenda kwa waganga kwa ajili ya kutaka utajiri hivyo ilawazimu kutoa sadaka sawasawa na mganga aliyowaangiza ili kupata kitu wanachokitaka.
Jifunze kumtolea Mungu sadaka hata kama uliyokuwa nayo ni kidogo kwa kiasi gani au kinauhitaji mkubwa kwa wakati huo ili Mungu ajue na kukuamini katika kitu kidogo na chenye umuhimu kwako wewe hukumyima Mungu na ukamfanya kuwa wa kwanza katika yote kuliko hitaji lako ndipo malaki 3:10 itakapotimia kwako.

Mungu akubariki. 

SISI NI MBENGU YA IBRAHIMU



SISI NI MBEGU YA IBRAHIMU
Waebrania 11-1,17 inasema “ Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana…..
Imani ni nini?
     Imani ni ile hali ya kuamini jambo hata kama bado halijatokea ila  Unaamini ndani yako kuwa limeshatokea kwahiyo unaamini katika ulimwengu wa Roho tayari ni lakwako japo kuwa katika ulimwengu wa mwili bado halijatokea.
Neno HAKIKA maana yake kuwa ndani yake hakuna shaka/kweli nk, na Naposema MAMBO YASIYOONEKANA maana yake ni jambo ambalo halijaonekana bado katika ulimwengu wa mwili ila lipo katika ulimwengu wa Roho na hakuna mtu mwingine aliyeliona zaidi ya kwako yani ni mafunuo ya kwako peke yako ambayo Mungu amekupa na anataka uyatoe katika ulimwengu wa Roho na uyalete katika ulimwengu wa mwili na kitu ambacho kitakusaidia uyatoe hayo maono yako ndani yako ni kwa njia ya Imani. Mfano unaona Nyumba ndani yako ( NAFSI MWAKO) ikiwa huna bado kiwanja sasa hapo ndipo unatakiwa utumie imani yako na hutakiwi kukata tamaa hata kama kuna mambo ambayo yanakatisha tamaa katika maisha yako  na yanakupelekea unaona kuwa huwezi kufika katika ufunuo wako wewe hutakiwi kukata tamaa unachotakiwa ni kuwa na imani ile ile.
            Tunaposema sisi ni mbegu ya Ibrahimu maana yake tunashiriki Baraka zake
Ambazo ni  :-
1)      Nguvu ya utajiri
2)      Umri mrefu (umri mtimilifu)
3)      Kuongea na Mungu muda wowote, mahali popote na wakati wowote.
4)      a)Nguvu ya Baraka zinazohama kwa watu unaowapenda mwanzo 12:3
b)Laana zinazowapiga adui zako
5)      Uwezo wa kuvunja sheria zilizowekwa katika ulimwengu wa Roho na ulimwengu wa mwili
6)      Uwezo wa kuzaa watoto
7)      Nguvu ya maagano uliyoweka wewe na Mungu itadumu vizazi na vizazi
8)      Nguvu ya kutoa sadaka zitakazomfanya mwanao aishi kwa neema.

Neno la Mungu linatuambia katika  Waebrania 11:17Kwa imani Ibrahimu alijaribiwa akamtoa Isaka awe dhabihu na  yeye aliyezipokea hizo ahadi alikuwa akimtoa mwanawe , mzaliwa pekee.”  Lazima ujiulize swali kabla hujatoa sadaka Unatoa sadaka ili iweje? Ni kitu gani unachokitegemea baada ya kutoa sadaka yako? Kwasababu maandiko yanatuambiaakamtoa Isaka awe dhabihu na  yeye aliyezipokea hizo ahadi”  kuna uhusiano gani kati ya sadaka ya Isaka na ahadi za Mungu kwa Ibrahimu? Kwanini Mungu asimpe tu bila kumjaribu kwa kumtoa sadaka mwanae wa pekee, lazima kuna kitu ambacho Mungu alikuwa anakitafuta kutoka kwa Ibrahimu kabla hajaachilia ahadi zake na Baraka zake alizomuahidi na ndio anachokitafuta na kwako leo hii mtumishi wa Mungu.

Imani iliyo ndani ya sadaka inamleta Mungu na kubadilisha mfumo wa maisha ulio nao. Imani inayotembea na sadaka ni kwa ajili ya kuzishinda sadaka nyingine. Imani iliyo ndani ya sadaka  ina nguvu ya kushawishi akili za Mungu akufanyie jambo lako kwa muda huo hata kama hakupanga kukufanyia kwa wakati huo. Unapotaka kufanikiwa katika fedha zako lazima uangalie unamtolea Mungu sadaka kwa imani ya kiwango gani.
Wakati mwingine ibome nafsi yako maana imekusababisha kuamini kwamba bila kuwa na kitu huwezi kupata.
Weka mkono katika kifua chako na sema maneno haya. “NAFSI YANGU NAKUBOMOA KUANZIA LEO USITEGEMEE VITU VINAVYOONEKANA ILI UWE NA IMANI TEGEMEA VITU AMBAVYO HAVIPO ILI VIWEZE KUTOKEA MAANA NDIO KAZI YA IMANI KATIKA JINA LA YESU”
AMEN, UBARIKIWE!!!!!!!!!!

Monday, March 2, 2015

JINSI YA KUONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU.



MADHABAHU  ZA  ROHO MTAKATIFU

MAFUTA
Isaya 61: 1 “Roho ya Bwana i juu yangu;kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri  wanyenyekevu  habari  njema, amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliovungwa habari za kufunguliwa kwao.”
Swali la kujiuliza kwanini mafuta? Na si kila mafuta yanayotumiwa kumpaka mtu na kuachilia nguvu za Roho Mtakatifu ndani ya mtu.
Zipo Sababu nyingi sana ila ngoja tuangalie sababu kuu tano (5) za kupakwa mafuta na Roho Mtakatifu pia Roho Mtakatifu  kuchagua kuwa ni moja ya madhabahu yake ni kama zifuatazo:-
       
        1. Ni kuweka wakfu (kuchaguliwa, kutengwa au kuteuliwa kwa kazi maalumu tu)
        2. Kuonyesha ishara ya kupewa agizo au kazi maalumu (appointment) ya Mungu.
        3. Kuonyesha ya kuwa umepewa mamlaka au uwezo maalumu kwa kazi  maalumu ya Mungu.
       4. Kuhalalisha kwa kazi maalumu na si kwa kazi nyingine.
       5. Kupitisha vitu vya ki-Muungu kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine.

Mtu anapomiminiwa mafuta maana yake ametengwa maalum kwa ajili ya kazi maalum, mfano katika kipindi cha agano la kale mtu hakuweza kuwa mfalme au kuhani pasipo Nabii kumpaka mafuta, kwahiyo Mungu anapomuagiza mtu kukuwekea mafuta maana yake anakuandaa kwa ajili ya kazi yake, na ni lazima uelewe ni kazi gani ambayo Mungu amekutenga maalum kwa ajili ya kuifanya.
Ila kuna kitu lazima uelewe Chochote ambacho Mungu anakifanya ujue kuna sehemu ya pili wanatumia yaani wanaomtumikia shetani wanaotumia pia mafuta. Kama yapo mafuta ambayo Roho Mtakatifu anayatumia kwa ajili ya kuleta furaha maana yake yapo pia mafuta ambayo mtu anaweza kuyatumia na akasababisha huzuni kwa mtu.

Pia kazi nyingine ya mafuta ni kuchukua  mipango ambayo wazazi wako wameshindwa kufanya kipindi ambacho wao walikuwa na nguvu walikuwepo yaani mafuta yanachukua sehemu ambapo baba yako ameshindwa kufanya mfano Sulemani alijenga hekalu la Bwana sawasawa na jinsi ambavyo baba yake Daudi alitaka kujenga..

Kufeli kwa wazazi wako kushindwa kufanya maendeleo katika maisha yenu si msiba kwako bali kunakupatia nafasi ya wewe kumuuliza Mungu ni kitu gani wazazi wako walitakiwa kufanya kwa ajili yenu na wewe ukafanya. 

Mungu akusaidie kuweza kutambua vitu ambavyo wazazi wako wameshindwa kuvifanya na wewe ukavifanye kwa nafasi yako.

Amen