SHILOH INTERNATIONAL MINISTRIES TANZANIA

Monday, March 2, 2015

JINSI YA KUONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU.



MADHABAHU  ZA  ROHO MTAKATIFU

MAFUTA
Isaya 61: 1 “Roho ya Bwana i juu yangu;kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri  wanyenyekevu  habari  njema, amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliovungwa habari za kufunguliwa kwao.”
Swali la kujiuliza kwanini mafuta? Na si kila mafuta yanayotumiwa kumpaka mtu na kuachilia nguvu za Roho Mtakatifu ndani ya mtu.
Zipo Sababu nyingi sana ila ngoja tuangalie sababu kuu tano (5) za kupakwa mafuta na Roho Mtakatifu pia Roho Mtakatifu  kuchagua kuwa ni moja ya madhabahu yake ni kama zifuatazo:-
       
        1. Ni kuweka wakfu (kuchaguliwa, kutengwa au kuteuliwa kwa kazi maalumu tu)
        2. Kuonyesha ishara ya kupewa agizo au kazi maalumu (appointment) ya Mungu.
        3. Kuonyesha ya kuwa umepewa mamlaka au uwezo maalumu kwa kazi  maalumu ya Mungu.
       4. Kuhalalisha kwa kazi maalumu na si kwa kazi nyingine.
       5. Kupitisha vitu vya ki-Muungu kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine.

Mtu anapomiminiwa mafuta maana yake ametengwa maalum kwa ajili ya kazi maalum, mfano katika kipindi cha agano la kale mtu hakuweza kuwa mfalme au kuhani pasipo Nabii kumpaka mafuta, kwahiyo Mungu anapomuagiza mtu kukuwekea mafuta maana yake anakuandaa kwa ajili ya kazi yake, na ni lazima uelewe ni kazi gani ambayo Mungu amekutenga maalum kwa ajili ya kuifanya.
Ila kuna kitu lazima uelewe Chochote ambacho Mungu anakifanya ujue kuna sehemu ya pili wanatumia yaani wanaomtumikia shetani wanaotumia pia mafuta. Kama yapo mafuta ambayo Roho Mtakatifu anayatumia kwa ajili ya kuleta furaha maana yake yapo pia mafuta ambayo mtu anaweza kuyatumia na akasababisha huzuni kwa mtu.

Pia kazi nyingine ya mafuta ni kuchukua  mipango ambayo wazazi wako wameshindwa kufanya kipindi ambacho wao walikuwa na nguvu walikuwepo yaani mafuta yanachukua sehemu ambapo baba yako ameshindwa kufanya mfano Sulemani alijenga hekalu la Bwana sawasawa na jinsi ambavyo baba yake Daudi alitaka kujenga..

Kufeli kwa wazazi wako kushindwa kufanya maendeleo katika maisha yenu si msiba kwako bali kunakupatia nafasi ya wewe kumuuliza Mungu ni kitu gani wazazi wako walitakiwa kufanya kwa ajili yenu na wewe ukafanya. 

Mungu akusaidie kuweza kutambua vitu ambavyo wazazi wako wameshindwa kuvifanya na wewe ukavifanye kwa nafasi yako.

Amen
 





2 comments:

Unknown said...

naomba roho mtakatifu amimine mafuta kwa ajili ya huduma yake kwangu kusudi nitembee kwenye kusudi lake.

Unknown said...

Karibu daima Roho mtakatifu, kaa ndani yangu, miminika kwa mafuta mabichi, katika Jina la Yesu Kristo. Ubarikiwe Nabii.