SISI
NI MBEGU YA IBRAHIMU
Waebrania
11-1,17 inasema “ Basi imani ni kuwa na
hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana…..
Imani
ni nini?
Imani ni ile hali ya kuamini jambo hata
kama bado halijatokea ila Unaamini ndani
yako kuwa limeshatokea kwahiyo unaamini katika ulimwengu wa Roho tayari ni
lakwako japo kuwa katika ulimwengu wa mwili bado halijatokea.
Neno
HAKIKA maana yake kuwa ndani yake
hakuna shaka/kweli nk, na Naposema MAMBO
YASIYOONEKANA maana yake ni jambo ambalo halijaonekana bado katika
ulimwengu wa mwili ila lipo katika ulimwengu wa Roho na hakuna mtu mwingine
aliyeliona zaidi ya kwako yani ni mafunuo ya kwako peke yako ambayo Mungu
amekupa na anataka uyatoe katika ulimwengu wa Roho na uyalete katika ulimwengu
wa mwili na kitu ambacho kitakusaidia uyatoe hayo maono yako ndani yako ni kwa
njia ya Imani. Mfano unaona Nyumba ndani yako ( NAFSI MWAKO) ikiwa huna bado
kiwanja sasa hapo ndipo unatakiwa utumie imani yako na hutakiwi kukata tamaa
hata kama kuna mambo ambayo yanakatisha tamaa katika maisha yako na yanakupelekea unaona kuwa huwezi kufika
katika ufunuo wako wewe hutakiwi kukata tamaa unachotakiwa ni kuwa na imani ile
ile.
Tunaposema sisi ni mbegu ya
Ibrahimu maana yake tunashiriki Baraka zake
Ambazo
ni :-
1)
Nguvu ya utajiri
2)
Umri mrefu (umri mtimilifu)
3)
Kuongea na Mungu muda wowote, mahali popote na
wakati wowote.
4)
a)Nguvu ya Baraka zinazohama kwa watu
unaowapenda mwanzo 12:3
b)Laana
zinazowapiga adui zako
5)
Uwezo wa kuvunja sheria zilizowekwa katika
ulimwengu wa Roho na ulimwengu wa mwili
6)
Uwezo wa kuzaa watoto
7)
Nguvu ya maagano uliyoweka wewe na Mungu
itadumu vizazi na vizazi
8)
Nguvu ya kutoa sadaka zitakazomfanya mwanao
aishi kwa neema.
Neno
la Mungu linatuambia katika Waebrania 11:17 “Kwa imani Ibrahimu alijaribiwa
akamtoa Isaka awe dhabihu na yeye
aliyezipokea hizo ahadi alikuwa akimtoa mwanawe , mzaliwa pekee.” Lazima ujiulize swali kabla hujatoa sadaka Unatoa sadaka ili iweje? Ni kitu
gani unachokitegemea baada ya kutoa sadaka yako? Kwasababu maandiko yanatuambia “akamtoa
Isaka awe dhabihu na yeye aliyezipokea
hizo ahadi” kuna uhusiano gani kati ya sadaka
ya Isaka na ahadi za Mungu kwa Ibrahimu? Kwanini Mungu asimpe tu bila kumjaribu
kwa kumtoa sadaka mwanae wa pekee, lazima kuna kitu ambacho Mungu alikuwa
anakitafuta kutoka kwa Ibrahimu kabla hajaachilia ahadi zake na Baraka zake
alizomuahidi na ndio anachokitafuta na kwako leo hii mtumishi wa Mungu.
Imani
iliyo ndani ya sadaka inamleta Mungu na kubadilisha mfumo wa maisha ulio nao. Imani
inayotembea na sadaka ni kwa ajili ya kuzishinda sadaka nyingine. Imani iliyo
ndani ya sadaka ina nguvu ya kushawishi
akili za Mungu akufanyie jambo lako kwa muda huo hata kama hakupanga kukufanyia
kwa wakati huo. Unapotaka kufanikiwa katika fedha zako lazima uangalie unamtolea
Mungu sadaka kwa imani ya kiwango gani.
Wakati
mwingine ibome nafsi yako maana imekusababisha kuamini kwamba bila kuwa na kitu
huwezi kupata.
Weka
mkono katika kifua chako na sema maneno haya. “NAFSI YANGU NAKUBOMOA KUANZIA
LEO USITEGEMEE VITU VINAVYOONEKANA ILI UWE NA IMANI TEGEMEA VITU AMBAVYO HAVIPO
ILI VIWEZE KUTOKEA MAANA NDIO KAZI YA IMANI KATIKA JINA LA YESU”
AMEN,
UBARIKIWE!!!!!!!!!!
1 comment:
Amen! Nakutukuza Bwana Yesu kwa somo hili, kupitia kinywa cha nabii wa Mungu aliye hai. Ushuhuda nimeweka mkono na nimeomba, nimetikisika kama kwa dakika,moja hivi. Namwamini Bwana kuwa something has happened, katika kurithi ahadi za baba yetu Ibrahimu.
Post a Comment