SHILOH INTERNATIONAL MINISTRIES TANZANIA
Monday, March 24, 2014
JUMAMOSI
22/MARCH/2014.
SOMO
NGUVU YA UUMBAJI.
Na.Nabii Frank Julius Kilawah
Kuna vitu ambavyo watu wengi wanaomcha Mungu hawavielewi, ndio maana hawavitumii hivyo kutoa mwanya kwa waliopo upande wa pili wa Shetani kuvitumia.
Watu wengi waliookoka bado hawajatambua Nguvu ya Uumbaji,Yesu kristo ndiye mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote, hivyo kuna nguvu kubwa sana ndani Uumbaji,ukiitambua nguvu hiyo utakuwa na uwezo mkubwa wa kumiliki mazingira unayoishi.
Wakolosai 1:15-16 Naye ni mfano wa Mungu asiyeonekana ,mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote,kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa,vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi,vinavyoonekana na visivyoonekana;ikiwa ni vitu vya enzi ,au usultani,au enzi,au mamlaka;vitu vyote viliumbwa kwa njia yake,na kwa ajili yake.
Andiko hili linathibitishia kuwa Yesu kristo ndiye mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote,neno hili likikaa katika fikra zako,hutaogopa chochote,hutakuwa na hofu juu ya magonjwa ya aina yeyote, maana hicho kijidudu kinachosababisha ugonjwa,kina mzaliwa wake wa kwanza ambaye ni Yesu Kristo.
Kwa hiyo tunatakiwa tuwe na uhakika kuwa juu ya magonjwa yote,kuna mzaliwa wake wa kwanza nayo humtii mzaliwa huyo ambaye ni Yesu Kristo.
Hii inakuthibitishia kiwango cha kumiliki na mamlaka uliyonayo ya kuamrisha kila kiumbe kilichopo katika mazingira unayoishi kwa kulitumia jina la mzaliwa wa kwanza Yesu Kristo.
Kama unasumbuliwa na virusi vya ukimwi tambua Yesu ni mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote,,hata katika vijidudu vya ukimwi Yesu ni mzaliwa wa kwanza wa vijidudu hivyo,kwa hiyo huna haja ya kuwa na hofu kwa maana kupitia jina la Yesu, vijidudu vya ukimwi vinafungasha virago na kuondoka katika damu yako na kuiacha ikiwa safi kabisa.
Marko 16:14-15 Baadaye akaonekana kwa wale kumi na mmoja walipokuwa wakila,akawakemea kwa kutokuamini kwao na ugumu wa mioyo yao,kwa kuwa hawakusadiki wale waliomwona alipofufuka katika wafu,akawaambia ,Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila KIUMBE.
Hapa Yesu akuwaambia mkaihubiri Injili kwa kila MTU,bali aliwaambia mkaihubiri Injili kwa kila KIUMBE kwa maana kila kiumbe kilichopo chini ya jua yeye ndiye mzaliwa wake wa kwanza.
Ukilijiua Neno hili vyema hutasumbiwa na mazingira unayoishi,chochote kinachotokea kisibadilishe akili yako, ukaacha kuamini unachokiamini,kwa maana nataka kukutambulisha kwa huyu anayeitwa mwanzo ili aanze na wewe katika ALFA na amalize na wewe katika OMEGA kwa kuwa ni yeye pekee ndiye mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote vilivyopo katika Mazingira unayoishi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment