SOMO
TEMBEA KATIKA UWEPO WA
ROHO MTAKATIFU.
Na.Nabii Frank Julius
Kilawah
16.03.2014
Kama
mzaliwa wa pili baada ya Yesu Kristo, unatakiwa kuishi chini ya mwongozo wa
Roho Mtakatifu katika kila jambo unalolifanya, wakati wote Roho Mtakatifu anapaswa
kukuongoza juu ya nini cha kufanya na ukiwa naye ndani yako unakuwa na ujasiri
wa kukabiliana na jambo lolote
linalokuja mbele yako. mfano kama ambavyo mlevi anayeongozwa na pombe anavyokuwa na
ujasiri wa kupita katika msitu mnene huko akikutana na simba anakuwa na ujasiri
wa kumkabili.
Yohana
7:6 “Basi Yesu akawaambia, haujafika bado
wakati wangu; ila wakati wenu siku zote upo”. Neno hili linatufundisha kuwa
hatupaswi kufanya maamuzi yetu wenyewe pasipo kusubiri wakati wa Bwana,Mungu
wetu. na wakati huo unatimilika pale Roho Mtakatifu anapokuongoza kufanya jambo
hilo.
Wengi
wanakwama katika mambo mengi kwa kuwa hufanya maamuzi kwa akili zao wenyewe
bila ya kumsikiliza Roho Mtakatifu ,unapoongozwa kufanya jambo lolote na Roho
Mtakatifu,Yesu Kristo anakusikia lakini
unapojiongoza mwenyewe katika mambo yako,mfano katika biashara,elimu, ndoa nk., hatokusikia bali utajisikia mwenyewe na
watu waliokuzunguka.
Mzaliwa
wa pili amepewa nafasi ya kuwa juu ya kila kiumbe chini ya jua na katika
ulimwengu wa roho,usiache neema ya mzaliwa wa pili ukaukumbatia ulokole, Roho Mtakatifu
hawezi hata siku moja kukupa nafasi ya kufurahia neema yake milele ikiwa haupo katika kusudi na mpango wa Mungu hivyo tambua
kuwa umezaliwa mara ya pili ili uwe chini ya uangalizi wa Roho Mtakatifu.
Mwanzo
25:34 na Mwanzo 27:36 tunamuona Yakobo ambaye ni mzaliwa wa pili anavyoipata
haki ya mzaliwa wa kwanza katika uzao wa Isaka na kuzibeba Baraka zote
alizostahili kuzipata Esau.
Shetani
muda wote yupo kazini kuhakikisha haukai katika kusudi na mpango wa Mungu ,hivyo kama mzaliwa wa pili inakupasa ukae chini ya uangalizi wa Roho Mtakatifu.
Wokovu ni kuishi
katika mwongozo wa Roho Mtakatifu katika kila jambo ulifanyalo“Watu
wote wanaoongozwa na Roho Mtakatifu hao ndio wana wa Mungu.”
No comments:
Post a Comment