SHILOH INTERNATIONAL MINISTRIES TANZANIA

Friday, April 4, 2014

ANGALIA NAMNA MAPOKEZI YA MAJOR PROPHET SHEPHERD BUSHIRI YALIVYOLITIKISA JIJI LA ARUSHA.

MAPOKEZI YA MAJOR SHEPHERD BUSHIRI YATIKISA JIJI LA ARUSHA.
 MTOTO WAKE WA KIROHO NABII FRANK JULIUS KILAWAH AMPOKEA KWA KISHINDO  AKIAMBATANA NA WATOTO WA SHILOH INTERNATIONAL MINISTRY KUTOKA  JIJINI TANGA.

    Ilikuwa ni mtikisiko katika kambi ya LUSIFA, baada ya Nabii kutoka Malawi Major Shepherd Bushiri kukanyaga ardhi ya Tanzania kwa mara nyingine tena katika Jiji Arusha, kwa ajili ya Mkutano mkubwa wa Kinabii uliofanyika mwishoni mwa mwezi  wa tatu mwaka huu,ulioandaliwa na Kanisa la Enlightened Church Gathering (ECG) lililopo Jijini humo.

Kulikuwa na Shamrashamra za kila aina katika uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro( KIA),wakati wakazi wa Jiji  hilo walipokuwa uwanjani hapo kwa ajili ya kumsubiri Major Shepherd Bushiri,Msululu wa watu ulitanda kandokando ya barabara za Jiji hilo kwa ajili ya mapokezi hayo, huku wengi wakiamini ujio wa Nabii huyo wa kimataifa ni Neema na Baraka ya namna ya Tofauti .

Wengi walikuwa wakisubiri kwa hamu kubwa kupokea Upako, uponyaji,na kufunguliwa katika maeneo mbalimbali  ya kiuchumi,Ndoa,kiafya na kielimu.

Mara baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Kilimanjaro (KIA),Nabii  Shepherd Bushiri alielekea katika hoteli ya Ngurudoto  mahali maalumu palipoandaliwa kwa ajili ya kufikia Mtumishi huyo wa Mungu,alipofika Hotelini hapo alipata nafasi ya kuzungumza na watu wote waliokuwa wakimsubiri kwa shauku kubwa .

Akizungumza na umati huo,Nabii Shepherd Bushiri aliuhakikishia umati huo kuwa, ana upendo mkubwa sana juu yao,na Kazi kubwa ya kubomoa na kuvunja minyororo ya shetani aliyowafunga watu wa Mungu ataifanya siku inayofuata.

Kila mmoja alikuwa na Imani kuu kwani matarajio ya kila mtu ni kukutana na muujiza wake,kwa kuwa  walitambua Nabii ni jicho la Mungu,na ni uso wa Mungu,unapokutana nae  akazungumza juu ya tatizo lako,huo ndio unakuwa mwisho wa kilio chako.

Hatimaye Nabii Major Shepherd Bushiri  alikutana na umati wa watu waliokuwa wakimsubiri kwa shauku kubwa katika ukumbi wa Lush Garden,Eneo lililoandaliwa kwa ajili ya Mkutano huo,Wengi walipokea miujiza yao,viwete walitembea,wenye matatizo ya uti wa mgongo waliponywa,na wengi walipokea upako na unabii kutoka kwa mtumishi wa Mungu.
                                                         
Major Prophet Shepherd Bushiri akiongozana na wenyeji wake,Mara baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Kilimanjaro (KIA) Tanzania.


Huu ni umati mkubwa wa watu waliokua wakimsubiri Major Prophet Shepherd Bushiri katika uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro(KIA),Tanzania.


No comments: