JUMANNE
01/APRIL/2014
SOMO:
NGUVU YA MAFUTA
YANAVYOWEZA KUMALIZA UMASKINI YAKIWA KATIKA MIKONO YA NABII
Na:Nabii Frank Julius
Kilawah.
Neno MIZEITUNI linamaanisha ni mti wa upako,Neno UPAKO linamaanisha
kuna kitu au kuna kimiminika au ni nguvu inayovutia si ndani yako bali inakua
juu yako inakufunika.
Tafsiri ya pili ya neno MIZEITUNI ni MEMSHAKI,tafsiri ya neno MEMSHAKI ni nguvu ambayo inakwenda zaidi ya
mipaka uliyowekewa,Pia mafuta haya ndiyo yaliyokuwepo hapo awali kabla hayajawa
mmea na kuitwa Mizeituni.
MEMSHAKI ni mafuta ya kwanza ambayo Mungu alimmiminia
aliyekuwa Malaika wa Sifa huko Mbinguni, aliyejulikana kwa jina la LUSIFA , ni
Malaika pekee wa Mbinguni aliyemiminiwa mafuta hayo na kazi kubwa ya haya
mafuta ni kukifanya kitu kiende zaidi ya mipaka yake.
Ikiwa asili ya Mizeituni ni Memshaki,na kazi ya haya Mafuta
ni Kwenda zaidi ya mipaka,ndio maana watumishi wa Mungu hutumia mafuta haya ili
kuwavusha watu zaidi ya mipaka yao ya Kiuchumi, Kiafya,Kielimu,Ndoa na Mafanikio
ya kila aina, kwa maana mafuta haya yakiwa na neno la Nabii ndani yake yanakuwa
na nguvu ya Mungu.
Tukiangalia katika maandiko matakatifu tunamuona mwanamke
mmoja miongoni mwa wake za wana wa Manabii, alivyomlilia Nabii Elisha kutokana
na tatizo lililokuwa linamkabili la kutokuwa na fedha,hivyo kutakiwa kulipa deni kwa kuwatoa wanawe wawili wakawe watumwa.
Mwanamke huyu alitumia mafuta kumaliza shida ya fedha iliyokuwa inamkabili,2WAFALME 4:2 Elisha akamwambia,Nikufanyie
nini?Niambie;una kitu gani nyumbani?Akasema,Mimi mjakazi wako sina kitu
nyumbani ,ila chupa ya mafuta .
Ukiendelea kusoma andiko hili katika ule mstari wa saba, tunaona
jinsi mafuta yalivyotumika kulipa deni na yaliyobaki aliyatumia kwa ajili ya
kutengeneza utajiri kama maandiko yanavyosema katika 2WAFALME 4: 7 “Ndipo akaja akamwambia
Yule mtu wa Mungu.Naye akasema,Enenda ukayauze mafuta haya,uilipe deni
yako;nayo yaliyosalia uyatumie wewe na watoto wako”.
Katika ule mstari wa sita maandiko yanasema mafuta
yalikoma,hii haimaanishi mafuta yaliisha,tafsiri ya neno ni sawa na mfano wa
bomba la maji,unapokinga maji ndoo ikijaa haimaanishi maji yameisha bali ulipata kiwango ulichokihitaji kwa wakati huo
Andiko hili linatuonyesha namna mafuta yanavyoweza kutumika
kama njia ya kukuondolea umaskini na kukupatia fedha, ndio maana Watumishi
wengi wa Mungu hasa Manabii hutumia mafuta kwa ajili ya kuwafungua watu
katika matatizo mbalimbali yakiwemo ya Kiuchumi
.
Ukiangalia wakati wa
Daudi,mara baada ya kupakwa mafuta na kuwekwa wakfu kuwa Mfalme kuna kitu kilibadilika
ndani yake,Masikio ya Daudi yalifunguka
na kuanza kusikia sauti ya Mungu hivyo kupata ujasiri wa kupambana na Goliati
kwa maana kwa kupakwa MAFUTA akajitambua kuwa ana nguvu kubwa ya Mungu ndani yake.
Daudi ambaye alikuwa akichunga Mbuzi za Baba yake kabla ya
kupakwa mafuta Masikio yake yalikuwa yakisikia sauti za Mbuzi ,Ng’ombe na Punda
machungioni, lakini mara baada ya kupakwa mafuta aliaminika hadi kufikia hatua
ya kupelekwa vitani, kwa maana waliitambua nguvu ya Mungu iliyokuwamo ndani yake
kutokana na MAFUTA aliyopakwa.
Baada ya kupakwa mafuta Daudi aliishi kama Nabii, kwa maana
macho yake ya ndani yaliona na alielewa kuwa Yesu ni Jiwe Kuu la pembeni ndio maana alikwenda kupambana na GOLIATI kwa
Jiwe kwa kutambua kuwa jiwe la pembeni halitambakisha GOLIATI salama.
Kazi ya mafuta ya upako ni kwa ajili ya kubadilisha jina na
mfumo wako maisha,ili watu waliokuzoea kukuona
kuwa wewe ni wa kiwango cha chini,washangae kuona namna Mungu
anavyokuinua katikati yao.
Mkilielewa somo hili nawahakikishia kwamba hapa duniani hamtakuwa
ombaomba, siwafundishi ili mbaki maskini, nataka muitambue nguvu ya mafuta ili
mnapowekwa wakfu muipokee nguvu hiyo kwa imani kuu na maisha yenu yakapate
kubadilika katika nyanja zote.
No comments:
Post a Comment