UTHIBITISHO WA UNABII
WA MR CHRISTOPHE WATIMIA MARA MOJA.
Mnamo tarehe
17/04/2014 katika ibada ya Alhamisi mtumishi wa Mungu; Nabii Frank Julius Kilawah alitoa unabii juu
ya wanandoa waliokuja kuabudu katika
kanisa la Shiloh International Ministry Tanga kwa mara ya kwanza na Mungu
alijidhihirisha kwa wana ndoa hao.
‘’Kaka uliye kamata mtoto’’
Jina lako nani?
Christopher Omary
Nabii.. Naona
roho ya Mungu inanipeleka Dar es salaam, Unaishi wapi?
Umewahi kuishi Dar es salaam
Mr Christopher Omary: Ndio Baba
Nabii; Naona vitu viwili moja, naona kama msalaba na
hapo ni maingilio ya barabara, ya pili Mungu
ananiambia Tanzania Region
Mr Christopher : Ndio Baba napafahamu.
Nabii: Kaka Mungu amesema nikusaidie, Naona watu
wamekutumikisha kwa kiwango kikubwa
ambacho usingebaki hivyo ulivyo sasa, na
fedha ulizo pata ni kidogo sana, Halafu naona kuna kanisa sehemu Fulani?
Umewahi kufanya kazi kanisani?
Mr Christopher: Ndio nilishafanya kazi kanisani.
Nabii: Kaka kuna roho ya Mungu inaenda
kukubadilisha, Naona watu wawili mmoja anaitwa mzee .Mbuna na Mzee. Mwaisaka .
Mr . Christopher: Ndio wote na wafahamu.
Ninacho kiona sasa kuna watu wawili kabila moja ni wasambaa, na mmoja ni mfupi,
naona mashemasi wawili wamefanya vita kali na wewe mmoja mfupi mweupe, anakaa
Gong’olamboto Dar es salaam, kilicho fanyika kwako hawa mashemasi wawili
wamekufanyia fitina na tena mmoja ni kiongozi wa maombi .
Kuna mtu mmoja Alisha kufa miaka tisa
9 iliyo pita alikuwa anafanya kazi ya ulinzi. Anaitwa Wille. Roho iliyokuwa
ndani yake ndio ipo kwako sasa, alikuwa anakaa Kimara Dar es salaam nyuma ya kanisa la K.K.K.T. mlikuwa mnafanya kazi pmj na kipindi
alipofariki ulijitolea kununua jeneza lakini hilo jeneza halikutumika na Roho
ile ile ndio inakutumikisha na ndio
iliyotumika kukufanya ufukuzwe kazi ndio mana hata mambo yako hayaendelei.
Mr Christopher.
“Ni kweli na mfahamu kwasababu huyo uliye sema mfupi mweupe ambaye ni Baba
yangu wa Kiroho nilikwenda kutoa mahali
Iringa alikuwa kama shemas, na mimi ndiye mwanzilishi wa Kanisa na ndio
nilikuwa wa kwanza kuwekewa mikono, Lakini kwa sasa kanisa lipo mikononi mwake,
Na ndipo vita ilipoanzia hapo”.
Nabii: Frank Julius Kilawah, Kuna Roho ambayo ipo nikikuombea saa hizi kuna watu karibia
tisa watakutafuta,na wakikukosa Mungu atakupeleka huko huko walipo, na unakwenda kuwa mtu tofauti kuanzia leo, Kaka
usijali, leo ndio breakthrough imeanza kwako.
Mtu wa Mungu aliwaita waje mbele
wanandoa hao.
Nabii Frank Julius Kilawah alielekea ofisini kwake na kurudi ameshikai Nguo na
kuwapatia mzee Christopher na mkewe.
MATHAYO 25:40 “ Na Mfalme atajibu,
akiwaambia, amini, na waambia, kadri mlivyo mtendea mmoja wapo wa hawa ndugu
zangu walio wadogo, mlinitendea mimi”.
Na utoaji haukuishia hapo waumini
waliguswa na maisha magumu wanayo ishi wanandoa hao, waliweza kutoa misaada
tofauti, kama T-shirt tano, suruali
tano, pea mbili za viatu, shuka moja, pea nne za vitenge, na fedha keshi laki
mbili na elfu nne.
Wana Ndoa hawo wana mshangaa Mungu
aliye waleta katka kanisa la Shiloh International Ministry Tanga Tanzania.
HAPA NABII FRANK JULIUS KILAWA AKIWA AMEWAITA NA KUWATOLEA UNABII
HAPA NABII FRANK JULIUS KILAWAH AKIWABARIKI
HAPA NABII FRANK JULIUS KILAWAH AKIWA KABIDHI FEDHA.
HAPA WAKIWA NA ZAWADI WALIZO KABIDHIWA
No comments:
Post a Comment