JUMATANO
16.04.2014
SOMO:NGUVU YA DAMU YA YESU
Na:Nabii
Frank Julius Kilawah.
Leo tunakwenda
kutengeneza roho ya kupata fedha na nguvu ya utajiri katika maisha ya
kwako,kupitia damu ya Yesu kristo utakwenda kuona milango minne ikifunguka kwa kila hitaji la
moyo wako.
1WARAKA WA PETRO 1:2 “kama vile Mungu Baba
alivyotangulia kuwajua katika kutakaswa na Roho,hata mkapata kutii na
kunyunyiziwa damu ya Yesu kristo,na neema na amani na ziongezwe kwenu”
Tunaona jinsi maandiko yanavyo tuthibitishia juu ya damu ya
Yesu, na kabla ya siku saba nilizokutangazia,umasikini wako unakwenda
kuisha,wakati naendelea kukufundisha naona kuna
damu zina kwenda kutiririka na mikono yako kujaa maji na malaika wakishuka.
Namshukuru Mungu anavyozidi kuongea na mimi juu ya kuondoa
roho ya umasikini katika maisha yako na kukupatia roho ya fedha na utajiri
kupiti damu ya Yesu, na uwe na uhakika leo naenda kupambana na wachawi
wanaopambana na wewe kwa ajili kurudisha maendeleo yako nyuma na hakuna kitu
kitakachobakia.
Kama ambavyo maandiko yanavyo tuambia katika kitabu cha WAEBRANI 12:24 “na Yesu mjumbe wa agano jipya ,na damu ya kunyunyizwa inenayo mema
kuliko ile ya Habili.”
Tambua ya kuwa damu ya Yesu inatenda mema juu ya maisha yako
ukiamini na kulitii neno lake unakuwa mshindi katika kila eneo, mimi baba yako Nabii Frank Julius Kilawah
nimelishika neno la Mungu ndio maana leo hii nakutamkia kwa ujasiri kuwa utakwenda
kupokea muujiza mkubwa na kuwa kiumbe kipya.
UFUNUO WA YOHANA 1:5;6
“tena zitokazo kwa Yesu kristo ,shahidi
aliye ,mwaminifu mzaliwa wa kwanza wa waliokufa,na mkuu wa wafalme
wa dunia,yeye atupendae na kutuosha dhambi zetu katika damu yake.’’
Nina habari njema kwako juu ya ujio wa Yesu kristo ndani
yako,anakwenda kuvunja kila nguvu za giza, na wakati huu hatakuja kama
ulivyomzoea bali anakuja kubadilisha
hata yale uliyokuwa huyafahamu, damu yake inakuwa kinga yako kwa kuwa damu hii
ina nguvu ya tofauti hasa katika kipindi hiki cha kufa na kufufuka kwake.
Utakwenda kuona mambo ya ajabu na makuu,Roho ya Mungu
imekwisha kuingia ndani yako, kama ambavyo Baba yangu yu ndani yangu,ndivyo
anavyokwenda kuwa ndani yako kuanzia sasa.
Amini nawaambieni damu ya Yesu ni jibu la maombi yako uiitapo
kwa uaminifu, ikiingia ndani yako papo hapo unapokea Roho ya utawala ambayo inakwenda
kumiliki mifupa yako na uzao wako unainuliwa.
No comments:
Post a Comment