SOMO:
WATAKUTAFUTA
Na.Wisdom Nyirenda.(Son
of Major Prophet Shepherd Bushiri of Malawi)
04/APRIL/2014.
WAAMUZI 11:1-10,tunamuona
mpiganaji hodari aitwaje Yeftha,aliyekuwa akiishi huko Gileadi,mwana wa mama
mmoja Malaya,na baba yake aliitwa Gileadi, ambaye alikuwa pia na wana wengine
kutoka kwa mke wake halali.
Wakati Yeftha anakua,
alikua ni mtu mwenye nguvu sana,hivyo kaka zake wakaingiwa na wivu
wakasemezana, “Tumfukuze kwa sababu anaweza kurithi ardhi za baba zetu,na mpango
wao ulifanikiwa.”
Ukisoma andiko hili utaona namna ndugu zake
Yeftha walivyomfukuza pale nyumbani na kumwambia kuwa hana haki ya kupata
urithi kutoka kwa baba yao, kwa sababu alikuwa amezaliwa na mama mwingine.
WAAMUZI 11:2“Gileadi
alikuwa pia na wana wengine kwa mke wake wa halali.watoto wa mke huyo
walipokuwa wakubwa,walimfukuza Yeftha kutoka nyumbani ,wakamwambia, “wewe huna
haki ya kupata urithi kutoka kwa baba yetu,maana wewe ni mtoto wa mwanamke
mwingine.”
Biblia inatuambia
kuwa, baada ya Yeftha kufukuzwa na ndugu zake,aliondoka na kwenda kuishi katika
nchi ya Tobu ambako alipokelewa na watu wa mji huo,wakajiunga naye katika
safari zake za mashambulio.
Andiko hili linatufundisha kuwa, vita vingi
katika maisha yako havitoki mbali, vinatoka kwa watu walio karibu yako, kama
ambavyo Yeftha alivyoibuliwa vita na kufukuzwa na
kaka zake mwenyewe.
Lakini baada ya muda fulani Waamoni walishambulia
Israel na baada ya vita kupamba moto,wakakumbushana kuwa wana ndugu yao
waliomfukuza anaitwa Yeftha ambaye atawasaidia ,ndipo wazee wa Gileadi walienda
kumtafuta Yeftha kutoka katika nchi ya Tobu ili aweze kuwasaidia katika vita
hiyo,hapa tunajifunza kuwa,waliokufukuza watakwenda kukutafuta.
Katika Waamuzi 11:5-6
wakati vita vilipopamba moto,wazee wa
Gileadi wakaenda kumleta Yeftha kutoka katika nchi ya Tobu,wakamwambia “Njoo
utuongoze katika vita yetu na Waamoni.”
Tafsiri ya Jina Yeftha
ni Funguo,walipomfukuza Yeftha inamaana walichukua funguo wakaitupa nje ,na vita
vilipopamba moto wakaanza kutafuta funguo iliyopotea kwa kuwa walikua wamejifungia
ndani wenyewe bila kujua watatokaje nje .
Wakati wanamfukuza Yeftha walimfukuza kama mbwa,walimwambia,wewe mwana wa kahaba toka nje ya ardhi
yetu na mambo yalivyokuwa magumu kwa upande wao wakati wa vita,wakawatuma wazee
wa nchi ile ambao kwa nyakati hizi ndio tunawaita Mawaziri wakaenda kumtafuta Yeftha, walipompata walimpigia magoti wakasema, “wewe ni kaka yetu tusamehe
njoo nyumbani na uwe kiongozi wetu.”
WAAMUZI 11:8 “hao
wazee wa Gileadi wakamwambia “Ndio maana tumekujia ili uende nasi kupigana na
waamoni,nawe utakuwa kiongozi wetu na wa wakazi wote wa Gileadi.”
Inawezekana mpaka
sasa katika familia yako wanakukataa,usiogope,wewe ni funguo,waliokukataa
watapiga magoti wanapokuja kukutafuta,kwa
kuwa wamejifungia ndani alafu wameitupa nje funguo, hivyo
ni lazima watakutafuta kwa maana hawataweza kutoka nje ya nyumba bila
kuwa na funguo na hiyo ndiyo itakuwa
hatma yako.
Kuanzia sasa tambua
kuwa wewe ni funguo,haijarishi umedharauliwa kwa kiwango gani ,unakwenda
kufungua hatma ya familia yako,kuanzia sasa historia yako inabadilika,kila
aliyekukataa atarudi kwa ajili yako, nawe utakuwa kiongozi wake kwa maana wewe
ni kichwa na wala sio mkia.
No comments:
Post a Comment