SHILOH INTERNATIONAL MINISTRIES TANZANIA

Friday, April 18, 2014

JINSI YA KUISHI NA BABA YAKO WA KIROHO.

SOMO:JINSI YA KUISHI NA BABA YAKO WA KIROHO.

Na.Wisdom Nyirenda,Son of Major Prophet Shepherd Bushiri.


Tukiangali  habari ya Eliya na Elisha  katika kitabu cha Wafalme tunaona namna Elisha alivyoomba   sehemu maradufu ya roho ya Eliya iwe juu yake,roho ya Eliya ikawa juu yake hivyo kuweza kufanya miujiza mara dufu ya baba yake .
WAFALME 2:9 “Hataikawa,walipokwisha kuvuka,Eliya akamwambia Elisha omba kwangu lolote utakalo nikutendee,kabla sijaondolewa kwako.Elisha akasema,Nakuomba,sehemu maradufu ya roho yako na iwe juu yangu.”

Nashukuru Mungu kwa upako wa Baba yangu wa kiroho(Shepherd Bushiri) kwa jinsi alivyonilea kiroho na Mungu ameniinua kuifanya huduma hii kimataifa.
Ukiishikilia imani itokayo kwa Baba yako Nabii Frank Julius Kilawah kazi anazo zifanya nawe utaweza kuzifanya maradufu kama ambavyo Elisha alivyopata upako mkubwa na kufanya miujiza maradufu ya ile iliyofanywa na Baba yake Eliya.

Kama ambavyo maandiko yanavyo tuthibitishia katika WAFALME2:8 tuona jinsi Eliya alivyotwaa vazi lake la juu akalikunja akayapiga maji yakagawanyika huku na huku na hao wawili wakavuka pakavu,naye Elisha  katika ule mstali wa 14 aliyapiga maji ya kagawanyika huku na kule,Elisha akavuka.

Muujiza huo ambao Elisha aliufanya uliwafanya wana wa manabii waliokuwa Yeriko wakimkabili, walipomwona,walikiri kuwa roho ya Eliya inakaa juu ya Elisha.
 Naamini somo la leo linakwenda kubadilisha kabisa kiwango cha imani yenu,na mtakuwa tofauti katika kila jambo lililopo mbele yenu,maisha yenu yanakwenda kubadilika

No comments: