SHILOH INTERNATIONAL MINISTRIES TANZANIA

Wednesday, April 2, 2014

SHILOH ANOINTING PRODUCTS(BIDHAA ZENYE UPAKO)

  SHILOH ANOINTING PRODUCTS(BIDHAA ZENYE UPAKO)

Nguvu ya  Mungu hujidhihirisha kwa namna tofauti tofauti na kupitia vitu mbalimbali ambavyo Yehova  Yire huwaongoza watumishi wake kuvitumia  vitu hivyo, kuwaponya na kuwafungua watu wenye matatizo ya kila aina.

Katika Maandiko matakatifu  tunaona Yesu Kristo alivyomponya  kipofu kwa kutumia tope, Yohana 9:7-6 alipokwisha kusema hayo,alitema mate chini,akafanya tope kwa yale mate,akampaka kipofu tope za macho,akamwambia ,nenda kanawe katika birika la siloamu,(maana yake ,aliyetumwa)Basi akaenda na kunawa ;akarudi anaona.
 

Hizi ni picha za bidhaa za upako (Anointing Product)zilizotolewa na Nabii Frank Julius Kilawah wa Kanisa la Shiloh International Ministry Tanga,Tanzania  kwa ajili ya kuwaponya na kuwafungua watu mbalimbali wanaosumbuliwa na nguvu za giza,magonjwa yaliyoshindikana na matatizo ya kila aina.;


Wengi wameshuhudia namna bidhaa hizi zilivyoleta uponyaji na kuwafungulia milango ya mafanikio,kiafya,kielimu na kiuchumi.

Kumekuwa na kiwango kikubwa sana cha ufaulu kwa ya wanafunzi waliomaliza kidato cha nne mwaka 2013 ambao walitumia Anointing Pen  wakati wa mitihani yao, ambao wengi walishuhudia jinsi Roho Mtakatifu alivyoungana nao na kuwakumbusha kile walichokisoma wakati wa kufanya mitihani yao na hatimaye kufaulu kwa kiwango cha daraja nla kwanza.

Hapa tunaona mama huyu aliyekuwa akisumbuliwa na Nguvu za giza, akifunguliwa kupitia Anointing Sticker iliyozinduliwa mapema hivi karibuni na Nabii Frank Julius Kilawah.






Mama huyu Bi.Matrona Aloyce Mushi,mara baada ya kuwekewa Anointing sticker mgongoni na Nabii Frank Julius Kilawah,ghafla Pepo la nyoka  lililokuwa likiishi ndani ya tumbo lake lilikutana na nguvu ya Mungu kupitia Anointing Sticker, na hatimaye Bi.Matrona alianza kupiga makelele ya kutaka aachiwe akidhani kuwa ni Nabii ndiye aliyemshika mgongoni mwake.


Nguvu ya Anointing Sticker iliendelea kufanya kazi kwa kuachilia moto wa Mungu ,ambao ulilifanya Pepo la Nyoka lililokuwa ndani mama huyu kufungasha virago na kuondoka.

Akitoa unabii kwa mama huyu Nabii Frank Julius Kilawah alimwambia  kuwa, anaona anaishi na Nyoka aina ya Chatu ndani ya tumbo lake ,ambaye ndiye chanzo cha kusambaratika kwa ndoa yake.

Baada ya kupokea unabii huo, mama huyu alithibitisha kuwa ni kweli wameachana na mume wake, Mama huyu kwa sasa yuko huru baada ya kufunguliwa kutoka katika mateso ya mapepo kupitia nguvu ya mungu iliyokuwa ndani ya Anointing Sticker.






2 comments:

Unknown said...

Mungu akubariki sana baba kwa bidhaa hizo zenye nguvu ya Mungu

IPtheLight said...

amen baba Mungu akubariki sana kwa kila jambo ulifanyalo