NENO LA KINABII LAMUINUA NA KUCHUKUA NAFASI YA KWANZA CHUONI.
Beatrice Michael,Mkazi wa maeneo ya Chumbageni Jijini Tanga, na Mwanafunzi wa mwaka wa Nne, katika chuo kikuu cha Dar es salaam(UDSM),amefanikiwa kushika nafasi ya kwanza kwa
upande wa wasichana, katika matokeo yake ya muhula wa kwanza wa mwaka wa nne, mara baada ya kupokea neno la Kinabii kutoka kwa Nabii Frank Julius Kilawah.
Akitoa ushuhuda mbele ya madhabahu ya Kanisa la Shiloh International Ministry,Beatrice ambaye anachukua kozi ya (Civil Engeneering and water Resource) alisema kuwa, awali hakuwahi kushika nafasi hiyo kwa miaka yote mitatu ya nyuma,lakini mara baada ya kulipokea Neno la Kinabii kwa imani kutoka kwa Nabii Frank Julius Kilawah, amefanikiwa kushika nafasi ya kwanza.
Alisema kuwa, kwa kawaida alikuwa akishika nafasi ya tatu,nne na kuendelea,lakini kwa mara ya kwanza ameshika nafasi ya kwanza, matokeo ambayo ameyapata baada ya kutamkiwa neno la kinabii na kulipokea kwa imani.
Alipokuwa akitoa neno hilo la kinabii Nabii Frank Julius Kilawah alisema”Wanavyuo hamtapata supplementary na mtakuwa wa kwanza”Beatrice,alilipokea neno hilo kwa imani na hatimaye Mungu amelisimamia Neno hilo katika matokeo ya mitihani yake.
Kuna nguvu kubwa ya Mungu ndani ya neno la kinabii,likitamkwa lipokee kwa Imani kuu, nalo linakwenda kubadilisha historia ya maisha yako kielimu,kiafya, kiuchumi na katika maeneo yote yanayogusa maisha yako.
No comments:
Post a Comment