NGUVU YA MUNGU YAJIDHIHIRISHA NDANI YA CHUMVI
Sawasawa na neno la Elisha alilolinena katika kitabu cha:- 2Wafalme 2:21,22, ‘’Akasema nileteeni chombo kipya,mtie
chumvi ndani yake. Wakamletea Akatoka akaenda mpaka chemichemi ya maji, akatupa
ile chumvi humo ndani, akasema, Bwana asema hivi, Nimeyaponya maji haya;
hakutatoka huko tena kufa wala kuzaa mapooza”.
Upako wa Elisha umeendelea kufanya kazi katika kizazi hiki
kupitia mtumishi wa Mungu Nabii Frank Julius Kilawah mara baada kuendesha ibada
ya Chumvi iliyofanyika Jumapili ya tarehe 25/04/2014.
Wakati wa ibada hiyo
kila muumini alikuwa na pakiti yake ya chumvi ambayo iliombewa na mtumishi wa
Mungu Nabii Frank Julius Kilawah,Nguvu ya Mungu ilijidhihirisha na wengi
walishuhudia kupokea uponyaji na kufunguliwa.
Mnamo tarehe 6/05/2014, Bi Helen Mwabumba mkazi wa Sahare ambaye
ni muumini katika huduma ya shiloh alitoa taarifa katika chumba cha habari cha
Shiloh Internatinal Ministry kuhusiana na kung’oka kwa mti wa mbuyu na
kuangukia nyumba anayoishi mara baada ya kumwaga chumvi ya upako kuzunguka
nyumba hiyo.
Timu ya wanahabari wa Shiloh International Mininistry iliweza
kufika eneo la tukio na kushuhudia namna Mbuyu huo ulivyong’oka kuleta
uharibifu katika nyumba hiyo.
Akiongea na wanahabari Bi.Heleni alisema kuwa tukio hilo
limetokea siku tano baada ya kumwaga chumvi pembezoni mwa nyumba hiyo.
“Niliporudi nyumbani nilimwaga chumvi ya upako pembezoni mwa
nyumba ninayoishi,ambapo ubavuni mwa nyumba hiyo kuna mbuyu mkubwa unaosadikiwa
kutumika katika mambo ya kishirikina ambao ulianguka siku tano baadae kutokana
na Nguvu ya Mungu iliyokuwamo ndani ya chumvi”.
“Ki ukweli mbuyu huu una mauza uza mengi,ni mda mrefu
wamejaribu kufika eneo hili ili waweze kuukata lakini wameshindwa,tunashangaa
hata imekuwaje umeng’oka wenyewe kiurahisi namna hii.”walieleza wakazi wa eneo
hilo bila kujua kama ni Nguvu ya Mungu imetumika kusambaratisha ngome hiyo ya
Ibirisi.
Hata hivyo Bi.Helen alithibitisha kuwa,hakuna aliyepoteza
maisha katika tukio hilo,Ingawa familia yake ilikuwa ndani wakati mbuyu huo
unadondokea nyumba, lakini waliweza kukimbia nje na kuyasalimisha maisha yao.
Popote penye Nguvu za Mungu hakuna nguvu za Giza zitakazoweza
kujificha.
Utukufu kwa Mungu.
No comments:
Post a Comment