SOMO: JINSI
JINA LINAVYOWEZA KUZUIA AU KUTOA BARAKA KATIKA MAISHA YAKO.
Na: NABII
FRANK JULIUS KILAWAH
Jina ni roho
kwa sababu linauwezo wa kubadilisha
mfumo wa maisha yako ya awali na kukupapatia mfumo mpya wa maisha,jina
linauwezo wakuzuia kupitisha kusudi la
Mungu kwa wakati maalumu,kwamaana jina
lipo kwenye ulimwengu wa roho na sisi tumerithi jina la Yesu kristo .
Yapo majina ambayo yamebeba laana hasa majina
ya kurithi, ambayo yanasababisha kutokufanikiwa
kwa kile unacho kifanya katika maisha yako.Nalipo jina moja tu lenye
uwezo wa kutenganisha jina lililo beba laana na jina hilo ni la “YESU KRISTO”.
Katika kitabu cha mwanzo
tunaona jinsi Mungu alivyoweza
kulibadilisha jina la Abramu na kumpatia jina jipya aliloitwa Ibrahimu.
MWANZO 17:5 “Wala jina lako
hutaitwa tena Abramu lakini jina lako litakuwa Ibrahimu, kwani nimekuweka uwe
baba wa mataifa mengi. Nitakufanya uwe
na uzao mwingi sana, nami nitakufanya
kuwa mataifa, na wafalme watatoka kwako”.
Jina lilivyokuwa na nafasi katika
maisha yako maana hata Mungu aliweza kumbadilishia jina Abramu na kumwita Ibrahimu hata Mungu aliweza kumwambia nitafanya maagano mimi na wewe nami nitakuzidishia sana na kubadilisha jina
uje kuwa baba wa mataifa na nitalipanua
nakulikuza jina lako, jina unalitumia linaweza kukufanya usione maono yako.
Kuna vitu vitatu vikubwa Mungu
alivyomwambia Abramu kwanza toka wewe katika nchi yako,na jamaa zako na nyumba
ya baba yako, uende mpaka huko utakakokwenda nitakupatia jina jingine pamoja na nchi.jina
lina nguvu ya kuyakamilisha malengo yako pale litakapo kuwa limetoka katika
ulimwengu wa roho.
Tulivyo sisi tupo kwenye
ulimwengu wa roho na Mungu ametuweka mbali na sisi , kwa hiyo kwenye ulimwengu wa
roho kuna majina yanayo kaa huko, unaweza ukaelewa sasa majina yapo kwenye ulimwengu wa roho,Maandiko
yanasema katika kitabu cha WAEFESO 1:20,21 “aliotenda katika kristo alipomfufua
katika wafu,akamweka mkono wake
wa kuume katika ulimwengu wa roho, juu sana kuliko ufalme wote,na mamlaka, na
nguvu na usultani, na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humu tu bali
katika ule ujao pia”.
WAEBRANIA 1:4 “amefanyika bora kupita malaika, kwa kadri jina alilorithi lilivyo
tukufu kuliko lao, kwa maana alimwambia malaika
yupi wakati wowote, Ndiwe mwanangu,mimi leo nimekuzaa?Na tena mimi
nitakuwa kwake baba,Na yeye atakuwa kwangu mwana?’’
Hivyo basi yapasa mzazi kutambulisha
jina la mtoto kabla hajazaliwa katika
ulimwengu wa roho, kwa kupitia njia ya maombi hii hufanya jina la mtoto liwe na busara, hekima na kibali mbele
ya wadogo na wakubwa na pia utambulishaji wa jina la mtoto katika ulimwengu wa
roho ni vema kwa sababu itamsaidia mtoto
kutokurithishwa majina ya ndugu yanayobeba laana za kutokufanikiwa ,
kifo, kichaa, kutokuwa na kibali mbele za watu.
1 comment:
AMEN BABA KWELI MAJINA YANAMAANA KUBWA JAPO WENGI WETU HATUJUI NINI HATIMA YA JINA HIVYO ASANTE SANA KWA MAFUNDISHO YAKO BABA
Post a Comment