JUMANNE 17/05/2014
SOMO: NGUVU ZA GIZA
Na: NABII FRANK
JULIUS KILAWAH.
Maana ya nguvu za giza.Ni akili za watu ambazo
zimefunikwa na haziwezi kitu fulani
ndani yake,na hukaa na kufanya kazi ndani ya mtu muongo,na roho ya uongo
inaleta karibu nguvu za giza,na kudili
nazo inahitaji ujasili maana uoga unasababisha adui zako kukipata kile
unachokitafuta na chochote unachokiogopa ndicho kitakacho kutokea, ni lazima
unachokifanya kitetemeshe watu.
Giza ni kitu kinacho funika kitu kisionekane, ndivyo ambavyo
maandiko yanatuambia, maana giza ndani yake linalo uwezo wa kubadilisha kitu
hatakama kipo wazi,na tunapo zungumzia habari za giza sio tunazungumzia usiku
peke yake, bali akili fulani iliyofunikwa ndani ya akili za watu ambayo haiwezi
kujua nini kifanyike na kiweze kutokea.pia nguvu ni kitu kinacho lazimisha
kitu kingine kiweze kutokea.
MWANZO 1:1,3. “Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na
nchi. Nayo nchi ilikuwa ukiwa,tena utupu,na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi
vya maji Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.Mungu akasema, Iwe nuru;
ikawa nuru. Mungu akaiona nuru,yakuwa ni njema;Mungu akatengeneza nuru na
giza”.
Kutanda kwa giza maana yake giza halikuumbwa, bali lilikuwepo
lakini nuru ilikuwepo na iliubwa, maandiko hayatuambii giza lilitoka wapi lakini
yanatuelezea nuru ilitoka wapi, kwamaana wa kwanza kutengeneza nuru ni Mungu,
na Mungu akasema kuwe nuru na ikawa nuru lakini haikuweza kumaliza giza lote.
Tunapo zungumzia habari za nguvu za giza kwa maana
nyingine tunazungumzia habari za wachawi, maana wachawi wanakaa kwenye nguvu za giza,kila
unacho taka kukifanya na wachawi wanataka kufanya pia kama wewe, na sio kwako
wewe tu, bali hata mimi Baba yako Nabii Frank Julius Kilawah ninapo hubiri na
kutoa unabii basi wachawi nao huwa nyanyua wa chawi wengine wahubiri injili
kinyume na mimi, kwa maana hiyo hata nikitoa unabii wa mtu kupata mimba na
mganga wa kienyeji naye atatafuta dawa na kumpatia mtu apate mimba.yote
ilikumeza miujiza ya Mungu ninaye mtumikia.
Mwanangu ninayo fimbo ya kumeza anayetabiri kwa jina la
shetani, hivyo ndivyo maandiko yananyo niambia, maana hata wewe ukipanga
mipango ya kwako kazi yake ni kumeza mipango mingine ya Falao, lakini siku ya
leo fimbo ya Musa itameza fimbo ya falao.nataka nikubadilishe kuanzia leo uwe
ni mtu wakuchukuwa neno na kulituma.
Maana maandiko yanasema nimelituma neno likaokoe mataifa
,hivyo kudili na nguvu za giza unahitaji kuwa na ujasili, kwaamana chochote
unacho kiogopa ndicho kitakacho kuharibia malengo yako na kukuuwa kabisa,hutakiwi
kuogopa nguvu yoyote ile ya giza maana sisi ni nuru ya ulimwengu kwa maana nuru
haingii katikati ya nuru bali inangaa katikati ya giza.
WAKOLOSAI 1:9 “Kwasababu hiyo sisi nasi,tangu siku ile
tulipo sikia hatuachi kufanya maombi na dua kwaajili yenu, ilimjazwe maarifa ya
mapenzi yake katika hekima yote na ufahamu waroho”.
Neno yote katika andiko hili,nikufanikiwa katika ulimwengu waroho
uwekamili, na kushindwa au kuto kufanikiwa sio kwa sababu hatuna Mungu, tatizo
kubwa ni kukosa maarifa,maana maarifa ni matendo yanayo kiumba kitu ilikiweze kutokea kwenye
macho ya kawaida.
1 comment:
Be blessed!
I pray that the lord who called you into that prophetic office will bless and anoint you more and more...
As I was reading your message titled "nguvu za giza", I was wonderfully blessed and inspired with the Holy Spirit..
Thank you.
Apostle Kuhanda J.N
Post a Comment