SOMO: UPANDE B WA MUNGU USIO UJUA.
Na: NABII FRANK JULIUS
KILAWAH
Upande B huwa haufi wala haushindwi kama upande A, kama kuna
mapito unayo pitia katika maisha yako tambua ya kuwa huo ni upande A, lakini
mbele yako kuna upande B ambao Mungu ameuandaa kwa ajili yako ambao ni ushindi
kwako, na hapo utakuwa wewe umezaliwa na mbegu isiyo haribika wala kufa.na
kuzaliwa kwako ni kwa mara ya pili. Mana hata katika maandiko Mungu akamwambia
Yoshua awapatie wayahudi upande B iliwaweze kujilinda na Israel kwamaana
watakuwa upande B wenye nguvu.
YOSHUA 6:1,2 “Basi Yeriko ulikuwa umefungwa kabisa kwa
sababu ya wana wa Israel; hapana mtu aliye toka wala hapana mtu aliyeingia ,
Bwana akamwambia Yoshua, Tazama, nimeutia Yeriko katika mkono wako, na mfalme
wake, na mashujaa wake”.
Kwanini Yeriko ilifungwa, ni kwasababu ya mtu mmoja jina lake
Izrael na haikufungwa kwaajili ya watu wote bali ni kwaajili ya huyo mtu mmjoja
tu,na watu wa mji huo walikuwa hawawezi kutoka wala kuingia, na ukiuliza ni
kwanini mlango umefungwa na wakajibu ni kwasababu ya mtu mmoja hatumtaki huyo
Izrael, na milango hatuta fungu mpaka aondoke ndipo watu wataingia na kutoka.
Maandiko yanasema hapata kuwa na mtu wa kuingia wala kutoka,
hapo lazima uelewe kwamba ni lazima mji uwe na mabadilishano ya fedha zinazo
toka na kuingia na kama kuna upako itakua vivyo hivyo kama fedha,maana maandiko
yanasema ni bora kutoa kuliko kupokea, kwa hiyo kuna milango ya kuingiza na yakutoa, Lakini kibibilia milango ya kutoa ni muhimu
sana kuliko ya kuingiza, hivyo kama utaenda kwa mtindo huo unaweza ukaelewa
vizuri ni kwanini yeriko imefungwa kwaajili ya wana wa Izrael, na ukienda kwa
mwendo huu pengine kwenye maisha ya kwako ya kawaida unaweza ukaelewa kabisa
kunabaadhi ya vitu haviendi vizuri kwenye maisha yako si kwaajili ya watu bali
na wewe mwenyewe hauwezi kutoka wala kuingia.
Hata hivyo hao wate waliokuwepo watasababisha vita na Yule
mtu aliye sababisha milango kufungwa, kwa maana waliokuwepo ndani walikosa
mahitaji kwaajili ya Izrael, hivyo nilazima kutakuwa na vita kubwa kwaajili ya milango kufungwa, na milango hiyo wayahudi wanataka
kupita, na nguvu za mfalme wa Eriko kazielekeaza kwenye malango yake na kusema
haruhusiwi mtu kupita wala kutoka. Mfalme wa eriko akasema peleka wanajeshi na
fungeni hiyo milango mtu asiweze kutoka.
Lakini Mungu akamwamba Yushua waambie wayahudi wasibomoe
milango na waiache kama ilivyo, bali wao wanachotakiwa kufanya maana upande A
ndio wanaoujua hebu wapatie upande B wasio ujua, najua watachanganyikiwa, kwa
maana maombi yao wanayofanya kwaajili ya kujilinda na waizrael wamepewa mpango
na mbinu za upande A hawana mbinu za upande B na kwasababu hawana mbinu za
upande B uwenauhakika hawajajipanga na kujikinga na upande B na itakapo anza
kazi na kwasababu hawana upande wa B na hawapo makini na kitakacho tokea upande
B bali wapo makini na kitakacho tokea kwenye mlango.
Hivyo basi Mungu akawambia hamhitaji tena kupambana na milango ya eriko, Maandiko
yanasema Mungu alimwambia Yoshua chukuwa makuhani, maana yake chukuwa waombaji, ndani yao wabebe sanduku la agano, maana maombi
haya hauwezi ukaomba kama ndani yake hamna agano, kama wataka nikusikilize ni kweli lazima uwe
na makuhani lakini siwezi kukusikiliza mpaka mikononi mwao wawe
na maagano, ili mimi Mungu nitumie
maombi yao ni changanye na agano ni weze kuwavusha wanapotakiwa kupita. “Mungu
anasema mimi ni Mungu wa maangano na siwezi kuipiga eriko kwa sababu umeomba
bali cha kufanya lazima uchukuwe agano ambalo nimewekeana na waizilaeli ndio
naweza kuomba” .
YUSHUA 6:12 “Yoshua akaondoka
asubuhi na mapema, nao makuhani wakalichuka sanduku la Bwana, Na wale
makuhania saba wakazichukuwa tarumbeta
saba za pembe za kondoo waume mbele ya sanduku la Bwana. Wakaendelea wakazipiga
tarumbeta; nao watu wenye silaha wakawatanguli na hao waliokuwapo nyuma
wakalifuata sanduku la Bwana; makuhani wakazipiga tarumbeta walipokuwa
wakienda”.
Mungu akamwambia Yushua kama
unataka ufanikiwa upande B nenda na uchukuwe agano la Baba yako Ibrahimu weka
ndani ya sanduku halafu nenda alfajili nitakuelekeza hilo agano linasema kitu
gani na nitakapo kuelekeza utafanya sawasawa na hilo agano na ndipo nitakapo
ifuta nchi yote ya Izrael.
Kama Mungu aliweza kuwazuia
wasipite kwenye mlango wa eriko na miji mingine kwa sababu hao wameshapita
kwenye mlango wa kwao na umesha wafungua kwasababu wao wametoka utumwani na
walitoka kwa damu iliyo pakwa kwenye ile milango, na milango yote ilifungwa
bali mmoja wa nyumba ya Falao ulikombolewa kwa damu ya wazaliwa wa kwanza ya
wanyama na binadamu,na hata hiyo iliyofungwa wanajua imefunguliwa. Lakini
maadamu Yesu tunae mtumikia alikufa na
hakutoka kwenye mlango bali alitoka ukutani, na hawa jaama wanasema tulipita
kwenye mlango mara moja sasa tunapita kwenye ukuta.
No comments:
Post a Comment