SHILOH INTERNATIONAL MINISTRIES TANZANIA

Monday, March 16, 2015

NGUVU YA SADAKA MBELE ZA MUNGU



SADAKA
 Neno SADAKA ni neno ambalo si geni masikioni mwa watu wengi na lina maana nyingi sana, nitatoa maana kama tatu hivi za neno sadaka.  Na zipo aina nyingi za sadaka kuna fungu la kumi, limbuko , sadaka ya shukrani na nk. Leo tutaangali sadaka kwa ujumla, Nguvu ya sadaka unapotoa katika Uwepo wa Mungu

Sadaka ni sehemu moja wapo ya kumuabudu Mungu, mwanzo 22:5  "Ibrahimu akawaambia vijana wake , kaeni hapa pamoja na punda , na mimi na kijana tutakwenda kule TUKAABUDU na kuwarudia tena"
Sadaka ni "kuonyesha upendo wako kwa Mungu" au unaweza kusema Sadaka ni "ushirika wetu katika kazi ya Mungu" 
Mungu aliweza kurudisha majira mapya katika nchi baada ya Nuhu kutoa sadaka. Hatuoni mahali ambapo Mungu amemuangizia/amemwambia Nuhu atoe sadaka au atengeneze madhabahu kwa ajili ya kumtolea Mungu sadaka kama alivyokuwa akiwaangiza baadhi ya watumishi wengine mfano: Musa aliagizwa awaambie wana wa Israel watoe sadaka au Ibrahimu amtoe mwanae wa pekee Isaka.
Swali la kujiuliza ni kitu gani kilimfanya Nuhu amtolee Bwana sadaka? Hatuoni Mungu akiongea na Nuhu baada ya kutoka ndani ya safina na wala biblia haituambi Nuhu alichukua muda gani tangu atoke ndani ya safina Mungu aliongea naye tena, inachotuambia ni Nuhu mara baada ya kutoka ndani ya safina alimjenge Bwana madhabahu na kumtolea sadaka ya kuteketezwa na iliyompelekea Mungu kufanya jambo jipya, Mungu anarudisha majira mapya katika nchi, na kumpa kutawala na kumiliki juu ya vitu vyote vya dunia hii yeye pamoja na watoto wake Nuhu. 
Kuna kitu lazima ujifunze wakati mwingine unashindwa kupokea Baraka zako kwanini,kwasababu haumtolei Mungu katika kiwango kinachompendeza na mahali ambapo hapana uwepo wake,Watu wengi tumetoa sadaka zetu katika hali ya mazoea,desturi na taratibu za ibada,kujilazimisha wakati mwingine hata kutaka kuonekana na watu unashindwa kuelewa nguvu iliyopo ndania ya sadaka? kwasababu unapotoa sadaka pasipo uwepo wa Mungu mahali hapo ujue sadaka yako haitaleta majibu ila ukitoa sadaka yako mahali ambapo kuna uwepo wa Mungu huwa majibu hayachelewi mfano kwa Nuhu, Ibrahimu

Tunaona katika mwanzo 8:21-22 Mungu amesikia harufu nzuri ya sadaka ya Nuhu ambayo hiyo sadaka imemlazimisha Mungu ajisemeshe(ajiapize) mwenyewe moyoni mwake au kwa lugha nyingine tunaweza kusema sadaka ya Nuhu ilimlazimisha Mungu kufanya kitu hata kama Mungu hakukipanga kukifanya.
Mwanzo 8:21b “WALA SITAIPIGA TENA BAADA YA HAYO KILA KILICHO HAI KAMA NILIVYOFANYA SITAILAANI NCHI……” Kutokana na andiko la mwanzo Mungu anaposema sitailaani nchi kwa lugha nyingine tunaweza kusema Mungu alikuwa na kawaida ya kuilaani nchi au kuna laana iliyokuwa inakuja mbele kwa ajili ya nchi kutomsaidi kwa kitu chochote atakachokifanya juu yake, ila kwa ajili ya na sadaka ya Nuhu, Mungu alijiapiza mwenyewe moyoni kuwa hatafanya hivyo tena, na anaposema TENA maana yake milele hakitakuwepo au hakitajirudia. Kwahiyo sadaka inanguvu ya kubadilisha kitu chochote unachokitaka na ndio maana wapo watu wanaoenda kwa waganga kwa ajili ya kutaka utajiri hivyo ilawazimu kutoa sadaka sawasawa na mganga aliyowaangiza ili kupata kitu wanachokitaka.
Jifunze kumtolea Mungu sadaka hata kama uliyokuwa nayo ni kidogo kwa kiasi gani au kinauhitaji mkubwa kwa wakati huo ili Mungu ajue na kukuamini katika kitu kidogo na chenye umuhimu kwako wewe hukumyima Mungu na ukamfanya kuwa wa kwanza katika yote kuliko hitaji lako ndipo malaki 3:10 itakapotimia kwako.

Mungu akubariki. 

SISI NI MBENGU YA IBRAHIMU



SISI NI MBEGU YA IBRAHIMU
Waebrania 11-1,17 inasema “ Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana…..
Imani ni nini?
     Imani ni ile hali ya kuamini jambo hata kama bado halijatokea ila  Unaamini ndani yako kuwa limeshatokea kwahiyo unaamini katika ulimwengu wa Roho tayari ni lakwako japo kuwa katika ulimwengu wa mwili bado halijatokea.
Neno HAKIKA maana yake kuwa ndani yake hakuna shaka/kweli nk, na Naposema MAMBO YASIYOONEKANA maana yake ni jambo ambalo halijaonekana bado katika ulimwengu wa mwili ila lipo katika ulimwengu wa Roho na hakuna mtu mwingine aliyeliona zaidi ya kwako yani ni mafunuo ya kwako peke yako ambayo Mungu amekupa na anataka uyatoe katika ulimwengu wa Roho na uyalete katika ulimwengu wa mwili na kitu ambacho kitakusaidia uyatoe hayo maono yako ndani yako ni kwa njia ya Imani. Mfano unaona Nyumba ndani yako ( NAFSI MWAKO) ikiwa huna bado kiwanja sasa hapo ndipo unatakiwa utumie imani yako na hutakiwi kukata tamaa hata kama kuna mambo ambayo yanakatisha tamaa katika maisha yako  na yanakupelekea unaona kuwa huwezi kufika katika ufunuo wako wewe hutakiwi kukata tamaa unachotakiwa ni kuwa na imani ile ile.
            Tunaposema sisi ni mbegu ya Ibrahimu maana yake tunashiriki Baraka zake
Ambazo ni  :-
1)      Nguvu ya utajiri
2)      Umri mrefu (umri mtimilifu)
3)      Kuongea na Mungu muda wowote, mahali popote na wakati wowote.
4)      a)Nguvu ya Baraka zinazohama kwa watu unaowapenda mwanzo 12:3
b)Laana zinazowapiga adui zako
5)      Uwezo wa kuvunja sheria zilizowekwa katika ulimwengu wa Roho na ulimwengu wa mwili
6)      Uwezo wa kuzaa watoto
7)      Nguvu ya maagano uliyoweka wewe na Mungu itadumu vizazi na vizazi
8)      Nguvu ya kutoa sadaka zitakazomfanya mwanao aishi kwa neema.

Neno la Mungu linatuambia katika  Waebrania 11:17Kwa imani Ibrahimu alijaribiwa akamtoa Isaka awe dhabihu na  yeye aliyezipokea hizo ahadi alikuwa akimtoa mwanawe , mzaliwa pekee.”  Lazima ujiulize swali kabla hujatoa sadaka Unatoa sadaka ili iweje? Ni kitu gani unachokitegemea baada ya kutoa sadaka yako? Kwasababu maandiko yanatuambiaakamtoa Isaka awe dhabihu na  yeye aliyezipokea hizo ahadi”  kuna uhusiano gani kati ya sadaka ya Isaka na ahadi za Mungu kwa Ibrahimu? Kwanini Mungu asimpe tu bila kumjaribu kwa kumtoa sadaka mwanae wa pekee, lazima kuna kitu ambacho Mungu alikuwa anakitafuta kutoka kwa Ibrahimu kabla hajaachilia ahadi zake na Baraka zake alizomuahidi na ndio anachokitafuta na kwako leo hii mtumishi wa Mungu.

Imani iliyo ndani ya sadaka inamleta Mungu na kubadilisha mfumo wa maisha ulio nao. Imani inayotembea na sadaka ni kwa ajili ya kuzishinda sadaka nyingine. Imani iliyo ndani ya sadaka  ina nguvu ya kushawishi akili za Mungu akufanyie jambo lako kwa muda huo hata kama hakupanga kukufanyia kwa wakati huo. Unapotaka kufanikiwa katika fedha zako lazima uangalie unamtolea Mungu sadaka kwa imani ya kiwango gani.
Wakati mwingine ibome nafsi yako maana imekusababisha kuamini kwamba bila kuwa na kitu huwezi kupata.
Weka mkono katika kifua chako na sema maneno haya. “NAFSI YANGU NAKUBOMOA KUANZIA LEO USITEGEMEE VITU VINAVYOONEKANA ILI UWE NA IMANI TEGEMEA VITU AMBAVYO HAVIPO ILI VIWEZE KUTOKEA MAANA NDIO KAZI YA IMANI KATIKA JINA LA YESU”
AMEN, UBARIKIWE!!!!!!!!!!

Monday, March 2, 2015

JINSI YA KUONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU.



MADHABAHU  ZA  ROHO MTAKATIFU

MAFUTA
Isaya 61: 1 “Roho ya Bwana i juu yangu;kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri  wanyenyekevu  habari  njema, amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliovungwa habari za kufunguliwa kwao.”
Swali la kujiuliza kwanini mafuta? Na si kila mafuta yanayotumiwa kumpaka mtu na kuachilia nguvu za Roho Mtakatifu ndani ya mtu.
Zipo Sababu nyingi sana ila ngoja tuangalie sababu kuu tano (5) za kupakwa mafuta na Roho Mtakatifu pia Roho Mtakatifu  kuchagua kuwa ni moja ya madhabahu yake ni kama zifuatazo:-
       
        1. Ni kuweka wakfu (kuchaguliwa, kutengwa au kuteuliwa kwa kazi maalumu tu)
        2. Kuonyesha ishara ya kupewa agizo au kazi maalumu (appointment) ya Mungu.
        3. Kuonyesha ya kuwa umepewa mamlaka au uwezo maalumu kwa kazi  maalumu ya Mungu.
       4. Kuhalalisha kwa kazi maalumu na si kwa kazi nyingine.
       5. Kupitisha vitu vya ki-Muungu kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine.

Mtu anapomiminiwa mafuta maana yake ametengwa maalum kwa ajili ya kazi maalum, mfano katika kipindi cha agano la kale mtu hakuweza kuwa mfalme au kuhani pasipo Nabii kumpaka mafuta, kwahiyo Mungu anapomuagiza mtu kukuwekea mafuta maana yake anakuandaa kwa ajili ya kazi yake, na ni lazima uelewe ni kazi gani ambayo Mungu amekutenga maalum kwa ajili ya kuifanya.
Ila kuna kitu lazima uelewe Chochote ambacho Mungu anakifanya ujue kuna sehemu ya pili wanatumia yaani wanaomtumikia shetani wanaotumia pia mafuta. Kama yapo mafuta ambayo Roho Mtakatifu anayatumia kwa ajili ya kuleta furaha maana yake yapo pia mafuta ambayo mtu anaweza kuyatumia na akasababisha huzuni kwa mtu.

Pia kazi nyingine ya mafuta ni kuchukua  mipango ambayo wazazi wako wameshindwa kufanya kipindi ambacho wao walikuwa na nguvu walikuwepo yaani mafuta yanachukua sehemu ambapo baba yako ameshindwa kufanya mfano Sulemani alijenga hekalu la Bwana sawasawa na jinsi ambavyo baba yake Daudi alitaka kujenga..

Kufeli kwa wazazi wako kushindwa kufanya maendeleo katika maisha yenu si msiba kwako bali kunakupatia nafasi ya wewe kumuuliza Mungu ni kitu gani wazazi wako walitakiwa kufanya kwa ajili yenu na wewe ukafanya. 

Mungu akusaidie kuweza kutambua vitu ambavyo wazazi wako wameshindwa kuvifanya na wewe ukavifanye kwa nafasi yako.

Amen