SHILOH INTERNATIONAL MINISTRIES TANZANIA

Monday, March 16, 2015

NGUVU YA SADAKA MBELE ZA MUNGU



SADAKA
 Neno SADAKA ni neno ambalo si geni masikioni mwa watu wengi na lina maana nyingi sana, nitatoa maana kama tatu hivi za neno sadaka.  Na zipo aina nyingi za sadaka kuna fungu la kumi, limbuko , sadaka ya shukrani na nk. Leo tutaangali sadaka kwa ujumla, Nguvu ya sadaka unapotoa katika Uwepo wa Mungu

Sadaka ni sehemu moja wapo ya kumuabudu Mungu, mwanzo 22:5  "Ibrahimu akawaambia vijana wake , kaeni hapa pamoja na punda , na mimi na kijana tutakwenda kule TUKAABUDU na kuwarudia tena"
Sadaka ni "kuonyesha upendo wako kwa Mungu" au unaweza kusema Sadaka ni "ushirika wetu katika kazi ya Mungu" 
Mungu aliweza kurudisha majira mapya katika nchi baada ya Nuhu kutoa sadaka. Hatuoni mahali ambapo Mungu amemuangizia/amemwambia Nuhu atoe sadaka au atengeneze madhabahu kwa ajili ya kumtolea Mungu sadaka kama alivyokuwa akiwaangiza baadhi ya watumishi wengine mfano: Musa aliagizwa awaambie wana wa Israel watoe sadaka au Ibrahimu amtoe mwanae wa pekee Isaka.
Swali la kujiuliza ni kitu gani kilimfanya Nuhu amtolee Bwana sadaka? Hatuoni Mungu akiongea na Nuhu baada ya kutoka ndani ya safina na wala biblia haituambi Nuhu alichukua muda gani tangu atoke ndani ya safina Mungu aliongea naye tena, inachotuambia ni Nuhu mara baada ya kutoka ndani ya safina alimjenge Bwana madhabahu na kumtolea sadaka ya kuteketezwa na iliyompelekea Mungu kufanya jambo jipya, Mungu anarudisha majira mapya katika nchi, na kumpa kutawala na kumiliki juu ya vitu vyote vya dunia hii yeye pamoja na watoto wake Nuhu. 
Kuna kitu lazima ujifunze wakati mwingine unashindwa kupokea Baraka zako kwanini,kwasababu haumtolei Mungu katika kiwango kinachompendeza na mahali ambapo hapana uwepo wake,Watu wengi tumetoa sadaka zetu katika hali ya mazoea,desturi na taratibu za ibada,kujilazimisha wakati mwingine hata kutaka kuonekana na watu unashindwa kuelewa nguvu iliyopo ndania ya sadaka? kwasababu unapotoa sadaka pasipo uwepo wa Mungu mahali hapo ujue sadaka yako haitaleta majibu ila ukitoa sadaka yako mahali ambapo kuna uwepo wa Mungu huwa majibu hayachelewi mfano kwa Nuhu, Ibrahimu

Tunaona katika mwanzo 8:21-22 Mungu amesikia harufu nzuri ya sadaka ya Nuhu ambayo hiyo sadaka imemlazimisha Mungu ajisemeshe(ajiapize) mwenyewe moyoni mwake au kwa lugha nyingine tunaweza kusema sadaka ya Nuhu ilimlazimisha Mungu kufanya kitu hata kama Mungu hakukipanga kukifanya.
Mwanzo 8:21b “WALA SITAIPIGA TENA BAADA YA HAYO KILA KILICHO HAI KAMA NILIVYOFANYA SITAILAANI NCHI……” Kutokana na andiko la mwanzo Mungu anaposema sitailaani nchi kwa lugha nyingine tunaweza kusema Mungu alikuwa na kawaida ya kuilaani nchi au kuna laana iliyokuwa inakuja mbele kwa ajili ya nchi kutomsaidi kwa kitu chochote atakachokifanya juu yake, ila kwa ajili ya na sadaka ya Nuhu, Mungu alijiapiza mwenyewe moyoni kuwa hatafanya hivyo tena, na anaposema TENA maana yake milele hakitakuwepo au hakitajirudia. Kwahiyo sadaka inanguvu ya kubadilisha kitu chochote unachokitaka na ndio maana wapo watu wanaoenda kwa waganga kwa ajili ya kutaka utajiri hivyo ilawazimu kutoa sadaka sawasawa na mganga aliyowaangiza ili kupata kitu wanachokitaka.
Jifunze kumtolea Mungu sadaka hata kama uliyokuwa nayo ni kidogo kwa kiasi gani au kinauhitaji mkubwa kwa wakati huo ili Mungu ajue na kukuamini katika kitu kidogo na chenye umuhimu kwako wewe hukumyima Mungu na ukamfanya kuwa wa kwanza katika yote kuliko hitaji lako ndipo malaki 3:10 itakapotimia kwako.

Mungu akubariki. 

3 comments:

Unknown said...

Amina! Hakika kuna nguvu ya maagano na Mungu, katika sadaka. Ubarikiwe nabii wa Mungu katika Jina la Yesu Kristo.

Dennis said...

Amen Prophet

Patrick said...

Nguvu ya Sadaka ni kubwa kuliko wengi wanavyofikiri. Tuondokane na mazoea, tutoe kwa kuzingatoa Neno na Uwepo wa Mungu. Nabii katuamsha.