JUMAPILI
23/MARCH/2014.
SOMO:JUMAPILI
23/MARCH/2014.
SOMO:
JINSI YA KUJITENGA NA UKOO WAKO ULETAO LAANA.
Na.Nabii Frank Julius Kilawah.
Kuna vitu ambavyo vinaendelea katika maisha uliyonayo,na wakati mwingine unapata shida kujitoa katika tatizo linalokusumbua kwa sababu ya LAANA ya ukoo wako.
Kwanza inabidi muelewe maana halisi ya neno LAANA ;
LAANA ni hali ya kusogezwa chini kutoka chini au kutokufanikiwa kwa kiwango ulichokusudiwa au kutokuuona wakati wako mpya au kutokubadilisha majira katika umri wako unaokuja na kwa lugha nyingine waweza kusema ni kutokustawi au kutokuendelea.
Mtu mwenye laana siku zote hasongi mbele,bali laana humvuta mtu huyo chini ili aende chini
Kwa kuwa katika kila Ukoo kuna pande mbili,upande wa Baba na upande wa Mama,mtoto anapozaliwa anaunganika na laana za pande zote mbili,laana zinazotoka upande wa Baba na laana zinazotoka upande wa Mama.
Leo ninataka kukubadilisha ili uweze kubaki na jina la ukoo,na kuziondoa chembe chembe zote za laana ya ukoo wako,unaweza kujiuliza LAANA hii inabaki vipi katika maisha yako, wakati unaenda mbele za mungu mara kwa mara kwa ajili ya TOBA.
Neno TOBA maana yake ni ubadilike unavyofikiri,na ni kweli Toba inaweza kujibu,lakini ni baada ya kwenda kwanza kwenye ASILI yako na kuiondoa LAANA ya ukoo wako.
Ezekiel 16:1 -3 Neno la Bwana likanijia tena, kusema,Mwanadamu,uujulishe Yerusalemu machukizo yake,useme,Bwana MUNGU auambia Yerusalemu hivi;Asili yako na kuzaliwa kwako kwatoka katika nchi ya Mkanaani;Mwamori alikuwa Baba yako,na Mama yako alikuwa Mhiti.
Andiko hili linatuonyesha, kumbe kuna ASILI ya mtu,na katika maisha ya kawaida, ukizungumzia Asili yako ina maamisha chimbuko la ukoo wako lilipoanzia,sasa kuna laana ambazo zimeanzia katika chimbuko la ukoo wako,ili uweze kupiga hatua kwenda mbele ni lazima ujitenge kwanza na laana hizo za ukoo wako.
Tunaona ni namna gani ASILI yako inavyoweza kumzuia Mungu kuingilia kati matatizo uliyonayo,ili Mungu aingilie kati,mruhusu kwanza aingie katika Asili ya Ukoo wenu.
YEREMIA 1:4-5 Neno la Bwana lilinijia,kusema,kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua,na kabla hujatoka tumboni ,nalikutakasa;nimekuweka kuwa Nabii wa kimataifa.
Andiko hili linamaanisha kwamba kabla Mungu hajakupitishia Kitovu kutoka katika kitovu unachokijua alikujua,akakutakasa maana hakutaka ASILI yenu iambatane na wewe,na aliposema nimekuweka kuwa Nabii wa kimataifa inamaana hakuna siri itakayojificha kwako,unakuwa na taarifa ya kinachotokea kabla hakijatokea
Hujawahi kujiuliza kwa nini baadhi ya koo mtoto anapozaliwa wanadai Kitovu,nywele za kwanza,na wengine hudai hadi kondo la nyuma la mama anayejifungua, katika hali ya kawaida vitu hivyo ni uchafu,na baadhi ya familia mwanamke anapotaka kujifungua ni lazima aende akajifungulie kwao,umeshawahi kujiuliza ni kwa nini, ni kwa sababu wanatumia KITOVU chako kukuunganisha na Asili ya ukoo wako,unapounganishwa,unaunganika pamoja na LAANA za ukoo wako.
Kwa sababu hiyo ASILI yako inamzuia Mungu kuingilia kati matatizo uliyonayo mpaka utakapojitenga nayo kwa kumruhusu Mungu aingie kwanza katika ASILI ya ukoo wenu na kuiondoa Laana.
Kuna mifumo mitatu ya Laana, ambayo ni laana ya afya,uhai na mafanikio, Hivyo ukitaka kutafuta chanzo cha kukwama kwako,rudi na uchunguze kati ya ASILI hizi mbili ya Baba yako na Mama yako na Mungu atasema nawe juu ya hilo kama ambavyo amesema nao katika kitabu cha Ezekieli ndivyo atakavyosema na wewe .
Ukielewa ASILI yenu utajua nini cha kufanya ,Mamajusi walielewa asili ya aliyezaliwa (Yesu Kristo) ndio maana hawakwenda mikono mitupu pia Nguvu ya Yesu kujifufua mwenyewe asili ya kitovu chake ni mbinguni,lakini ili mauti yamfike asili ya kitovu chake ni mwanadamu ambaye ndiye alimsulubisha Yesu na kumuua.
Asili uliyonayo haiwezi kukupatia kwanza unachokitaka,itakupatia usichokitaka mpaka pale utakapojitoa kwenye asili hiyo,kama ambavyo Mungu alipomwita Ibrahimu na kumwambia nataka nikuanzishie asili nyingine.
Ni watu wachache kabisa katika kundi la watu waliookoka walioacha asili za kwao,wengi bado wanashiriki katika mambo ya asili za kwao kama matambiko,ujenzi wa makaburi na mengineyo hivyo kujiwekea kitanzi na kushindwa kujitoa katika Asili zao.
Ili uweze kusonga mbele kiafya,katika Uhai na kimaendeleo ni lazima kwanza ujitenge na laana za ukoo wenu,Jitenge kwanza na asili za ukoo wenu uletao laana uweze kufunguliwa na kupokea muujiza wako.
1 comment:
Mungu awainue zaidi kazi yenu ni njema!!!
Post a Comment