SHILOH INTERNATIONAL MINISTRIES TANZANIA

Friday, April 4, 2014

MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU KUTOKA KWA PAPAA WISDOM NYIRENDA



JUMANNE
03.APRIL2014.
SOMO:
ROHO SABA ZA MUNGU ZILIZOMPONYA NAAMANI.
Na. Wisdom Nyirenda.Malawi
( Son of Mojor Shepherd Bushiri)alipohubiri katika Kanisa la Shiloh International Ministry,Tanga,Tanzania.

Roho wa Mungu ni dawa kwa kila mwanadamu,Neno hili linajidhihirisha unapoangalia habari ya Naamani
ambaye alitakaswa Ugonjwa wa Ukoma alioishi nao kwa muda wa miaka mingi,mara baada ya Roho wa Mungu kuingia ndani yake.

 2WAFALME 5:14 “Ndipo akashuka ,akajichovya mara saba katika Yordani,sawasawana neno lake yule mtu wa Mungu;nayo nyama ya mwili wake ikarudi ikawa kama nyama ya mwili wa mtoto mchanga,akawa safi”.

Ukisoma katika kitabu cha ISAYA: 11,utaelewa kwa nini tunasema Roho saba za Mungu,kitabu hiki kimezitaja Roho za Mungu ambapo ndizo zilizomponya na kumbadilisha Namaan ambaye alikuwa  anaabudu Miungu waliyoitengeneza wenyewe na kutokuamini kuhusiana na habari ya Mungu aliye hai YEHOVA YIRE.

ISAYA 11:2 “Na roho ya BWANA,atakaa juu yake,roho ya hekima na ufahamu,roho ya ushauri na uweza,roho ya maarifa na ya kumcha Bwana”.

Leo ninakwenda kuzielezea hizi Roho saba na namna ambavyo kila moja ilivyoleta uponyaji na mabadiliko katika maisha ya Naamani,jemedari wa jeshi la mfalme  wa Shamu.

Ukiangalia katika 2WAFALME 10,tunaona Nabii Elisha alivyokuwa akitoa maelekezo kwa mjumbe ambaye alipeleka ujumbe kwa Naaman aliyekuwa amesimama mlangoni pa nyumba ya Elisha kuwa, aende akaoge katika mto Yordani mara saba,na nyama ya mwili wake itarudi ,naye atakuwa safi.

Mabadiliko katika mwili wa Naamanai na katika imani yake  yalianza punde tu alipojichovya katika maji kwa mara ya kwanza,Maandiko yanasema alipojivyovya kwa mara ya Kwanza Roho ya Mungu ilikuja juu yake ikampa AMANI kisha aakanza kuona mabadiliko katika mwili wake.

Kwa sababu hiyo Hasira iliondoka katika moyo wa Naamani na kuendelea kujichofya kwa mara ya Pili,na alipojichovya kwa mara ya pili Roho ya HEKIMA ikashuka juu yake, akaanza kuona sehemu zilizo katika-katika mwilini mwake zinaanza kuungana .

Kawaida ya roho ya HEKIMA uwa inawapa watu maarifa,Naamani akaanza kujiangalia akafikiri jinsi alivyokuwa hapo awali na jinsi alivyokuwa mara baada ya kujichovya kwa maea ya pili,akagundua kuna kitu kimebadilika katika mwili wake na ndani yake,hapa Roho ya hekima ilisema nae.

Alipoendelea kujichovya kwa mara ya Tatu,Roho ya Ufahamu ikaja juu yake,akaanza kutafakari namna alivyokuwa akioga katika mito ya nyumbani kwao kwa mda mrefu bila mabadiliko na namna alivyobadilika alipokuwa anaendelea kujichovya katika mto Yordan.

Biblia inatuambia kuwa alipojichovya kwa mara ya Nne,Roho ya ushauri ilishuka juu yake,ndipo Naamani alipojigundua kuwa hahitaji mtu yeyote  wa kumfundisha,ndipo Roho wa Mungu aliyeingia ndani yake akaanza kumfundisha ,kisha akaanza kujishauri yeye mwenyewe na kuona kuwa alikuwa anafanya mambo yasiyo sahihi.

Ilipofika Mara ya Tano, Roho ya Uweza na nguvu ikaja juu yake,tukizungumzia Neno Nguvu,linamaana ni  kitu ambacho kinasababisha mabadiliko,kwa mfano, nikimkamata mtu nikamsukuma nitakuwa nimesababisha mabadiliko,hivyo wakati Roho ya Nguvu  ilipokuja juu yake,maumivu yake yote yaliyotokana na vidonda yalitoweka.

Naamani alipojichovya kwa mara ya sita,Roho ya Maarifa ikaja juu yake,ilipokuwa juu yake ilisababisha kukiri kuwa hakuna Mungu mwingine zaidi ya Mungu wa Israel,Nami nawahakikishia kuwa yeyote ambaye haamini kuhusu Mungu wa Shiloh unayemtumikia, akikanyaga mahali hapa atakiri kuwa hakuna Mungu mwingine zaidi ya Mungu wa Shiloh,Mungu aliye hai (ELISHADAI).

Katika maandiko matakatifu tunaona kuwa ,Mara baada ya kujichovya kwa mara ya saba,ambayo ilikuwa ni mara ya mwisho kulingana na maagizo ya Nabii Elisha,Roho ya kumcha Bwana ikaja juu yake,akapata uponyaji kamili  na ngozi ya mwili wake ikawa laini kama ya mtoto mchanga.

Ndani ya somo hili tunajifunza kuhusu kulitii neno la Nabii,awali tunaona Naamani  alivyokaidi agizo la Nabii Elisha,2WAFALME 11, “Lakini Naamani akakasirika,akaondoka,akasema,Tazama ,nalidhani a,Bila shaka atatoka kwangu,na kusimama,na kuomba kwa jina la BWANA,Mungu wake ,na kupitisha mkono wake mahali penye ugonjwa,na kuniponya mimi mwenye ukoma”.

Lakini mara baada ya kutenda  kulingana na maagizo ya Nabii,Naamini alipokea uponyaji wake na maisha yake yalibadilika,agizo la Nabii Elisha kwa Naamani lilikuwa la kinabii  na ikumbukwe kwamba mto  Yordan ni mto wa Uhai.





1 comment:

Unknown said...
This comment has been removed by the author.