SOMO: BIASHARA YA NGUO
Na: NABII
FRANK JULIUS KILAWAH
Biashara ni kuhamisha fedha kwenye mikono ya mtu na kumpatia
alicho kipenda kwenye biashara yako na kuridhika nacho.Unapofanya biashara ni
lazima uongee na Mungu kwa sababu ndio chanzo cha biashara yako na yeye ndiye
anayekupatia wateja, maana mnunuzi ndiye bosi wako, yeye ndiye anayekupatia
asilimia nyingi na kuweza kufikia malengo yako na ikitokea wanunuzi
wakaondoka basi na biashara inakufa.
Kuna vitu vinavyoweza kukufanya wewe uweze kufanya biashara,
kama fedha unayofanyia biashara uliomba kwa mtu na akakupatia kwa moyo mmoja
basi hiyo biashara itakuwa na neema iliyo jaa roho mtakatifu na kama unafanya
biashara kwa kutumia fedha za uchawi
basi hiyo biashara ndani yake itakuwa imejaa roho chafu ambazo
zitakazokwamisha biashara yako.
UFUNUO 18:11-13 “Nao wafanya biashara wa nchi walia na kuombolezea,
kwa sababu hapana mtu anunuaye bidhaa yao tena; bidhaa ya dhahabu, na fedha, na
kitu chenye thamani, na lulu, na kitani nzuri na nguo ya rangi ya zambarau, na
Hariri na nguo nyekundu; na kila mti wa uudi na kila chombo cha pembe, na kila
chombo cha mti wa thamani nyingi na cha shaba, na cha chuma, na cha marimari”.
Nguo na tafsiri ya
kuivaa, tafsiri yake
ni kwa ajili ya dhambi, kwa maana hata nguo ya kwanza ya Adamu, yalikuwa matawi
ya mti, baada ya vazi hilo ndio Mungu akampatia vazi la ng’ozi ambalo ndiyo nguo
ya pili ya Adamu. Na ilipokuja sheria ya kuvaa nguo , Mungu aliweka sheria
yake,na kila mtu akampatia sharti na aina ya nguo anayo stahiri kuvaa .
MWANZO 3:7 “Wakafumbuliwa macho wote wawili wakajijua
kuwa wapo uchi, wakashona majani ya mti, wakajifanyia nguo, kisha wakasikia
sauti ya BWANA Mungu akitembea bustanini wakati wa jua kupunga; Adamu na mkewe
wakajifika kati ya miti ya bustani,
Bwana Mungu asiwaone”.
Maandiko yanasema Adamu
na mkewe waliweza kuvaa mavazi ya matawi ya mti,kwa andiko hilo tunaona
jinsi vazi lilivyo na heshima mbele za macho ya Mungu,na chochote unachokiva lazima
uomaombe na kukiingiza kwenye ulimwengu wa roho, ili hiyo nguo iweze kukubariki
na na kukuletea mafanikio katika kazi zako unazozifanya na pia kukukinga katika
magonjwa mbalimbali.
Nguo ni jambo la kiroho na ndani yake kuna kitu, kitendo cha Mungu
kutengeneza nguo basi hata shetani anatengeneza nguo, kwamaana hiyo, yapo mavazi
yenye shepu shetani, na katika ulimwengu
tulionao vijana wengi wanaishi kwa mitindo ya mavazi ya kuiga ndio maana wanapotea katika njia iliyo sahihi.MATHAYO 9:20 “Akatokea mwanamke mmoja ambaye alikuwa amesumbuliwa na tatizo la kutokwa damu kwa muda wa miaka kumi na miwili, akaja nyuma ya Yesu akagusa upindo wa nguo yake, 21 kwa maana alisema moyoni mwake, “Nikigusa tu nguo yake, nitaponywa.” 22 Yesu akageuka, na alipomwona akamwambia, “Binti, jipe moyo, imani yako imekuponya.” Na wakati huo huo yule mwanamke akapona”
Nguvu ya Mungu ipo ndani ya nguo hivyo basi sivema kuvaa upendavyo , kwa maana mavazi yaliweza kumponya mwanamke aliye kuwa akivuja damu kwa muda wa miaka kumi na miwili baada tu ya kushika pindo la vazi la Yesu na damu ikakata papo hapo,tunaona jinsi nguo ilivyo kuwa na roho ya uponyaji pale tu ukiwa na imani.