SHILOH INTERNATIONAL MINISTRIES TANZANIA

Monday, May 26, 2014

JINSI NGUVU YA MUNGU INANYOTENDA KAZI NDANI YA NGUO.



SOMO: BIASHARA YA NGUO

 Na:  NABII  FRANK   JULIUS  KILAWAH

Biashara ni kuhamisha fedha kwenye mikono ya mtu na kumpatia alicho kipenda kwenye biashara yako na kuridhika nacho.Unapofanya biashara ni lazima uongee na Mungu kwa sababu ndio chanzo cha biashara yako na yeye ndiye anayekupatia wateja, maana mnunuzi ndiye bosi wako, yeye ndiye anayekupatia asilimia nyingi na kuweza kufikia malengo yako na ikitokea wanunuzi wakaondoka  basi na biashara inakufa.

Kuna vitu vinavyoweza kukufanya wewe uweze kufanya biashara, kama fedha unayofanyia biashara uliomba kwa mtu na akakupatia kwa moyo mmoja basi hiyo biashara itakuwa na neema iliyo jaa roho mtakatifu na kama unafanya biashara kwa kutumia fedha za uchawi  basi hiyo biashara ndani yake itakuwa imejaa roho chafu ambazo zitakazokwamisha biashara yako.

UFUNUO 18:11-13 “Nao wafanya biashara wa nchi walia na kuombolezea, kwa sababu hapana mtu anunuaye bidhaa yao tena; bidhaa ya dhahabu, na fedha, na kitu chenye thamani, na lulu, na kitani nzuri na nguo ya rangi ya zambarau, na Hariri na nguo nyekundu; na kila mti wa uudi na kila chombo cha pembe, na kila chombo cha mti wa thamani nyingi na cha shaba, na cha chuma, na cha marimari”.

Nguo na tafsiri ya kuivaa, tafsiri yake ni kwa ajili ya dhambi, kwa maana hata nguo ya kwanza ya Adamu, yalikuwa matawi ya mti, baada ya vazi hilo ndio Mungu akampatia vazi la ng’ozi ambalo ndiyo nguo ya pili ya Adamu. Na ilipokuja sheria ya kuvaa nguo , Mungu aliweka sheria yake,na kila mtu akampatia sharti na aina ya nguo anayo stahiri kuvaa .

MWANZO 3:7 “Wakafumbuliwa macho wote wawili wakajijua kuwa wapo uchi, wakashona majani ya mti, wakajifanyia nguo, kisha wakasikia sauti ya BWANA Mungu akitembea bustanini wakati wa jua kupunga; Adamu na mkewe wakajifika  kati ya miti ya bustani, Bwana Mungu asiwaone”.

Maandiko yanasema Adamu  na mkewe waliweza kuvaa mavazi ya matawi ya mti,kwa andiko hilo tunaona jinsi vazi lilivyo na heshima mbele za macho ya Mungu,na chochote unachokiva lazima uomaombe na kukiingiza kwenye ulimwengu wa roho, ili hiyo nguo iweze kukubariki na na kukuletea mafanikio katika kazi zako unazozifanya na pia kukukinga katika magonjwa mbalimbali.
Nguo ni jambo la kiroho na ndani yake kuna kitu, kitendo cha Mungu kutengeneza nguo basi hata shetani anatengeneza nguo, kwamaana hiyo, yapo mavazi yenye  shepu shetani, na katika ulimwengu tulionao vijana wengi wanaishi kwa mitindo ya mavazi ya kuiga ndio maana  wanapotea katika njia iliyo sahihi.

MATHAYO 9:20   Akatokea mwanamke mmoja ambaye alikuwa amesumbuliwa na tatizo la kutokwa damu kwa muda wa miaka kumi na miwili, akaja nyuma ya Yesu akagusa upindo wa nguo yake, 21 kwa maana alisema moyoni mwake, “Nikigusa tu nguo yake, nitaponywa.” 22 Yesu akageuka, na alipomwona akamwambia, “Binti, jipe moyo, imani yako imekuponya.” Na wakati huo huo yule mwanamke akapona”

Nguvu ya Mungu ipo ndani ya nguo hivyo basi sivema kuvaa upendavyo , kwa maana mavazi yaliweza kumponya mwanamke aliye kuwa akivuja damu kwa muda wa miaka kumi na miwili baada tu ya kushika pindo la vazi la Yesu na damu ikakata papo hapo,tunaona jinsi nguo ilivyo kuwa na roho ya uponyaji pale tu ukiwa na imani.

No comments: