SOMO: NDOA NA MAHUSIANO
Na: NABII FRANK JULIUS
KILAWAH
Ndoa, ni muungano kati ya mwanamume na mwanamke kuishi pamoja kama mume na
mke muda wote wa maisha yao,na mpango na utaratibu wa Mungu umewekwa wazi
katika kitabu cha MWANZO 2:18. “Bwana
Mungu akasema,sivema huyo mtu awe peke yake nitamfanyia msaidizi wa kufanana
naye’’
.
Mungu hakuumba watu bali aliumba mtu, kwa maana hiyo Mungu aliumba
mwanamume peke yake inamana alikuwa hana mpango wa kumuumba mwanamke, ni vizuri
ukaelewa na kuwa na ufahamu juu ya uumbaji wa Mungu, iliuweza kujua mambo mengi,
ndani ya Mwanamume ndio alikuwepo mwanamke, maandiko yanasema Mungu alipomaliza
kuumba aliangalia kazi yake akaona ipo sawa na sahii mbele ya macho yake
akaamua kupumzika.
Katika kitabu cha Mwanzo sura ile ya kwanza Mungu aliumba mtu kwa mfano
wake, maana yake mwanamume na mwanamke washatokea.
MWANZO 1:26,27 ''Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura
yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi
yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi, Mungu akaumba mtu
kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimuumba, mwanamume na mwanamke
aliwaumba".
Tukisoma maandiko katika kitabu cha Mwanzo ile sura ya pili, inatuelezea
hatua ya umbaji wa mwanadamu, maandiko ya nasema, mwanadamu ametoka katika
udongo, lakini sura ya kwanza haijatuelezea ametoka wapi bali inasema tumfanye
mtu kutoka katika sura ya kwetu na mfano wa kwetu, kwa hiyo sura ya kwanza
unayoiona ni image ambayo Mungu alimtengenezea mtu kutoka kwenye sura, rangi na
mfano wa kwake
.
MWANZO 2:7 “Bwana Mungu alimfanya mtu kwa mavumbi ya
ardhi, akampulizia pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai. Bwana Mungu akampanda
bustanii upande wa mashariki wa Edeni, akamweka ndani yake huyo mtu
aliemfanya”.
Katika sura ya pili inamtengeneza mtu wa pili ambaye hatokani na sura ya
Mungu wala rangi image na mfano wa Mungu, bali alimtengeneza kwa mfano wa nchi,maandiko
yanatuambia Mungu alimuumba mwanamke na mwanaume kwa mfano wake,pia tumfanye
hilo neno maana yake picha ya kwanza ya mwanadamu iliyopo kwenye sura ya kwanza
mfano wake duniani haupo, bali unafanana na hao waliokuwa wamesema tumfanye mtu
kwa mfano wetu na sura yetu hiyo ndiyo image.
Na ukisoma maandiko vizuri na kuyaelewa unaweza
kujua kuwa aliye pulizia pumzi ya uhai kwenye udongo hakuwa Mungu, bali aliye
pulizia pumzi ya uhai kwenye udongo, kwenye ile sura ya pili alikuwa ni huyu
aliyeumbwa kwa mfano na sura ya nchi, kwa sababu katika sura ya kwanza
inatuelezea amepewa mamlaka ya kuzaa na kuongezeka kwa hiyo alipokuja kwenye
hii sura ya pili ya nchi umbaji wa Mungu haupo.
MWANZO 1:28 “Mungu akawabariki, Mungu akawaambia,
zaeni,mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitisha; mkatawale samaki wa baharini, na
ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi”.
Sambamba na hayo umbaji wa sura ya pili, ni yule alieumbwa kwenye sura ya
kwanza, ametokea kwenye sura ya pili sasa anataka kuzaa na kuongezeka na
akajitoa na kujitengeneza mwili wa kwake, akaufanya na kuupulizia pumzi ya
kwake na akajiita mwenyewe na akisimama akisema jina langu ni Adamu.
No comments:
Post a Comment