ALHAMISI 05/06/2014
SOMO: JINSI YA KULINDA
LANGO
Na: NABII FRANK JULIUS
KILAWAH
Lango ni mlango wa
kuingizia ama kupitishia vitu tofauti vizuri na vibaya,kiroho na kimwili,pia
kwa maana nyingine ni Yule mtu anaye simama kwa miaba ya mafanikio yako. kikubwa ni
kujua nani ni lango la kwako na unalilinda kwa kiasi gani,maana lango limebeba
mafanikio ya maisha ya kwako kifedha na kiuchumi, bila kulitambua lango lako na
kulilinda ni rahisi kupoteza kile kilichokuwa kinakuletea mafanikio katika
maisha ya kwako.
Sijajua kama unaelewa ndugu zako ambao maisha yao
yameharibika wakati wewe unamjua Mungu, uwe na uhakika Mungu atakudai maisha
yao mikononi kwako, sasa haimanishi
atadai zambi zao mikononi mwako,si hivyo bali Mungu atadai maisha yao mikononui
mwako.
Mungu alikuwa anaongea na Ibrahimu, na Ibrahimu alikuwa
anaongea na Mungu, lakini maongezi ya Ibrahimu yalikuwa ni kupunguza ghadhabu
ya Mungu aliyo ipanga kwaajili ya watu wa Sodoma na Gomola, Maana Mungu alikuwa
ashapanga kwenda kuichoma ile Sodoma na gomola, maandiko yanasema Mungu
alijadili mwenyewe na kusema tumfiche
Ibrahimu? Lakini baada ya hapo, akasema hapa siwezi kumficha kitu na akamua
kumweleza.
MWANZO 18:16 “Kisha watu hawa wakaondoka huko
wakaelekeza nyuso zao sodoma. Ibrahimu akaenda pamoja nao awasindikize.Bwana
akanena, je! nimfiche Ibrahimu jambo nilifanyalo,Ikiwa Ibrahimu atakuwa taifa kuu, hodari, na katika yeye
mataifa yote ya dunia watabarikiwa”.
Bwana akasema , nikiona katika sodoma wenye haki
hamsini mjini nitapaacha mahali pote kwa
ajili yao, Ibrahimu akaanza kusema wakiwepo wenye haki hamsini, Mungu akajibu
sitapiga, na wakiwepo Arobain na tano, Pia akajibu hivyo hivyo mpaka ilipo
fikia kwenye kumi, Mungu akamjibu sitopiga tena. Lakini Ibrahimu alipoishia
hapo kwenye kumi, ndipo alipojiingiza
kwenye agano la Mungu na kutomsikilizwa tena,ndipo Mungu alimwambia
Ibrahimu, sasa hivi nitasema mara hii moja tu wala sitaongeza kitu tena.
MWANZO 18:23 “Ibrahimu akakaribia,akasema je! Utaharibu mwenye haki pamoja na mwovu? Huenda
wakawapo wenye haki hamsini katika mji, utaharibu, wala hutaacha mji kwa ajili
ya hao hamsini wenye haki waliomo? La
hasha usifanye hivyo, ukamuuwa mwenye haki pamoja na muovu, Hasha;
Mhukumu ulimwengu wote msitende haki? ”.
Ibrahimu akauliza je! Ukikuta wenye haki kumi
utawapiga, Mungu akasema nikiwakuta wenye haki kumi sitapiga sodoma wala
gomola, Pengine Ibrahimu asingejiingiza kwenye lileagano
labda Mungu asinge weza kusema kuwa atasema mara hii
tu. Mungu angetumia sentensi nyingine kwamba pia ni kiwakuta watano sitapiga, kwa
kuwa Mungu alishashusha ghadhabu yake, basi angeweza kusema kama kuna watu wa tano sitapiga tena. Ibrahimu
alichokosea mbele ya macho ya Mungu aliishi watu kumi alishindwa kuhesabu ndugu
yake Lutu ana watu wangapi katika nyumba yake ili kwa hao Mungu asiipige nchi.
Katika Dunia tuliokuwa nayo si watu wengi wanaelewa
maandiko, bali watu wengi waliopo ni warahisi wa kukuza tatizo kuliko kujua
maandiko, na ndicho kinacho fanyika kwenye maisha ya watu, kwa hali hiyo mzani
wa maisha ya kwao ni kukuza tatizo sio kulikuza neono la Bwana na ndani mwao ni
rahisi kulishusha likawa dogo.
Maandiko yana tuambia Ibrahimu alipoishia kwenye watu
kumi angeweza kuendelea kulembele naamini Sodoma na gomola isinge chomwa moto, ndipo
malaika na Mungu wakaondoka kwenye uso wa Ibrahimu, maandiko yanasema
walipofika kwenye nchi ile ya sodoma wakaingia, lakini maombi ya Ibrahimu
hayakumuokoa lutu. ikiwa watu wengi wamejijengea imani kwamba maombi ya
Ibrahimu ndio yalimuokoa lutu kitu ambacho si kweli,maana hata katika nyumba ya
mzee Ibrahimu hapakua na mtu mmoja bali walikuwepo watu wanne akiwemo yeye na
mkewa na dada wawili.
Ghadhabu ya Mungu iliapa kama nikikuta watu kumi
sitahukumu na maadamu hakuna watu kumi na maombi yako yameishia hapo hapo
kwenye watu kumi, hukutaka kuendelea hivyo utakuwa umeungana na mimi Mungu
kuhukumu ninacho kwenda kukihukumu, kwa sababu
nilikupa nafasi ya kunihoji
kuhusu adhabu na hukumu ninayo kwenda kuiachi, na umeishia mahali fulani
na hukutaka kuendelea.
Kwa hiyo Ibrahimu alienda na kukaa na kufanya anayo ya
fahamu na kuomba kwake kote akaishia kwenye watu kumi, na kushindwa kuelewa
ndugu yake lutu anawatu wangapi nyumbani kwake na wote wanahitaji kuokolewa,
Maandiko yanasema kilichomsaidia lutu alikuwa amekaa kwenye lango la kuingilia mjini maana ndiye alikuwa anajua
nani wa mwisho kutoka na kuingia kwa sababu alikaa kwenye lango la mji.
Na unatakiwa kujua ni kwanini Ibrahimu alikataa kukaa
katikati ya mji na akaamua kwenda kukaa
kwenye lango la mji, na sijui kama watu wengi mnaelewa kwamba mtu aliyeokoka hawezi kukaa katikati ya mji, nilazima akae
kwView blogenye maingilio ya lango la mji maana ndio mlango wa kila kitu.
No comments:
Post a Comment