JUMA TANO 18/05/2014
SOMO: ROHO YA UOGA
Roho ya uoga inaleta
giza karibu yako na kukuweka mbali na uwepo wa Mungu, na kuwapatia nafasi adui zako waweze kufanya
kitu chochote unacho kifanya wewe na kupata nguvu pale tu unapokuwa na roho ya
uoga mbele zao,,na kukufanya uangalie wingi wa adui zako katika kila jambo unalo
fikilia kulifanya na kupelekea kushindwa kwasababu umebeba roho ya uoga.
Hutakiwi kuwa na roho ya uoga wala kusikiliza vitu vinavyo
ogopesha, maana hata maombi hutaweza kupokea na kumwamsha mtu yule ambaye hana
imani ndani yake,na kuto kuogopa kwako kutakufanya umalize wingi wa adui
zako, ushindi ndio unatakiwa kuzunguka
akili zako na kuupata kwa wakati ulioutaka sio kuwa na uoga.
YOSHUA 1:6,7 “Uwe hodari na moyo wa ushujaa, maana ni
wewe utakaye warithisha watu hawa nchi hii niliyo waapia baba zao ya kwamba nitawapa. Uwe hodari tu na
shujaa mwingi, uangalie na kutenda sawasawa na sheria yote aliyokuamuru Musa,
mtumishi wa Mungu;usiiache,kwenda mkono wa kulia wala kushoto,upate kufanikiwa
sana kila uendako”.
Tunaona katika bibilia jiinsi Mungu anavyotoa agizo, na agizo
hili halikutolewa kwa wayahudi wote bali lilitolewa kwa mtu aliyepewa
majukumu,hivyo wayahudi hawakuagizwa wawe na roho ya kishujaa lakini aliyetakiwa
kuwa na roho ya kishujaa ni kiongozi wao aliye pewa majukumu na ndiye atakae
ongoza watu kwenda kanani.
Kama Mungu aliweza kutoa agizo usiwe na roho ya uoga basi
mambo yanayo kuja mbele yako yatakuwa yanaogopesha, hata kwa nje yatakuwa
yanaogopesha kwa sababu hiyo utakuwa ukiangalia kushoto na kulia utakuwa huoni
uwepo wa Mungu, maandiko yana niambia Mungu alimwambia Yoshua usiogope nipo
pamoja nawe kwa hiyo kwa lugha nyingine kwenye hiyo safari kitakachokuwa
kinaonekana mara zote ni matatizo na
yatakuwa mengi tofauti na uwepo wa Mungu.
Uwepo wa Mungu utaonekana baada ya wewe kuingia katikati ya
vinavyo ogopesha kutokuviogopa,maana alitoa agizo kile kitendo cha kutokuogopa
vinavyo ogopesha sio cha kufanya maombi,wa kufanga, bali kitendo cha wewe
kutokuogopa kina leta uwepo wa Mungu aliyesema usiogope katikati ya vinavyo ogopesha,na utaibeba roho
yangu ya kuto kuogopa na nitakutetea na kukulinda katikati yako, maana hata
ukifanya maombi hawezi kutokea mana sijakuagiza ufanye hivyo.
YOSHUO1:9 “Je! Si mimi niliye kuamuru? Uwe hodari na
moyo wa ushujaa; usiogope wala usifadhaike; kwa kuwa Bwana, Mungu wako, yu
pamoja nawe kila uendako”.
Mwanangu nakuambia jua katika maisha yako kuna maeneo mengine
sio ya Yesu lazima yawe ya kwako, kwa maana yeye amesha maliza na kutoa kibali
cha wewe kutokuogopa,sasa funga roho ya uoga chukua roho ya ujasiri na uende
nayo, kitendo cha wewe kutokuogopa kinainua upendo wa Mungu katikati yako na
kuweza kufikia malengo yako katika eneo hilo.
Roho ya uoga inakufanya umuondoe Mungu katikati ya maisha
yako na kukuzuia usipanuke kiakili na mawazo maana kila unalotaka kulifanya
unaogopa na mahali popote unapo kuwa na uoga ndipo nguvu ya Mungu
inapatikana.hivyo ni vyema kuondoa roho yoyote ya uoga ili uweze kufikia
halifulani katika ulimwengu wa roho.
1 comment:
That's very true and the truth in it has power to deliver us all. I'm still going on reading your messages, and now, I come across another message, titled "fear".
God has never given us the spirit of fear, but of POWER, LOVE AND SOUND MIND-2 Timothy 1:7.
Prophet! I love your messages because they are simple, clear and impactive. Even a standard seven pupils can clearly understand and actualise it.
May the lord pour out more revelation and demonstrations of his Spirit upon you.
Apostle Kuhanda J.N
Post a Comment