SHILOH INTERNATIONAL MINISTRIES TANZANIA

Monday, July 14, 2014



14/07/2014
SOMO:  MACHO YA ROHONI
Na: NABII FRANK JULIUS KILAWAH.

Macho ya rohoni .Ni macho ambayo yanauwezo wa kuona vitu ambavyo kwa macho ya kawaida (nyama) hayawezi kuona  ila mpaka uwe na macho haya,ila inatengemaea unamtumikia Mungu gani, maana ukiwa unamtumikia Mungu utakuwa unaviona vya kwake na Shetani utakuwa unaona vya kwake,ingawa macho haya yote yana uwezo wa kuona vitu vyote vya gizani na  vya nuruni. lakini macho ya mungu yana nguvu ya kukuvusha zaidi kwa kila upande utakao onyeshwa.


Umuhimu wa kuwa na macho ya rohoni, utakuwa katika ulimwengu tofauti katika hali isiyokuwa ya kawaida kwako, kwasababu utaona vitu vilivyo pita vya sasa  na vinavyokuja mbele yako, itakuwa rahisi katika maisha yako na kutambua nini unatakiwa kufanya sasa, mfano wa kitu kilicho pita inawezekana kuna mahali ulikosea na baada ya kupata macho ya rohoni ukajua ulipokosea ni rahisi kuenda mbele za Mungu na kuomba msamaha,maana hata ulimi hauwezi kutamka kitu kama macho hayajaona , maandiko yanasema  jicho likiwa na giza mwili hauwezi kuona kwamana jicho ndio linaweza kumsaidia kuona.

MWANZO 6:14,17 “Kwahiyo akapeleka huko farasi na magari, na jeshi kubwa; wakafika usiku, wakauzingira mji ule pande zote.Hata asubuhi na mapema mtumishi wake yule mtu wa Mungu alipoondoka,na kwenda nje,kumbe! Panajeshi la watu, na farasi na magari,wameuzingira mji ule.mtumishi wake akamwambia,Ole wetu! Bwana wangu,tufanyeje?Akamjibu, usiogope;maana waliopamoja nasi ni wengi kuliko wale waliopamoja nao.Elisha akaomba akasema,Ee Bwana,nakusihi mfumbue macho yake,apate kuona.Bwana akamfumbua macho yule mtumishi; naye akaona; na tazama kile kilima kilikuwa kimejaa farasi na magari ya moto yaliyomzunguka Elisha pande zote”.





Mungu anamacho? Kweli Mungu ana macho, maana maandiko yanasema katika kitabu cha MWANZO 3,”Baada ya Adamu kumuacha mke wake na kuwa mbali naye, na huyu mwanamke hakumuaga Adamu lakini alikoelekea njia zote zina majina na Mungu alisha weka malaika katika zile njia iliasiweze kula tunda,lakina nyoka aliweza kuwadanganya,na baada ya kula wakafunguliwa macho, kwamaana ya kufunguliwa macho sikwamba hawakuwa na macho, bali walikuwa nayo lakini kuna kitu kilikuwa kikisubiriwa kwa hamu kikiingia ndani ya miili yao kitafungua macho waliyokuwa nayo na kama mungu aliwanyima kwa muda ule wasione kitu, lakini aliwapatia macho ya kuona kitu kingine wakati haya haja funguliwa”.
 
Baada ya kula tunda na kufunguliwa macho, adamu aliposikia sauti ya Mungu alikimbia,Maandiko ya nasema alipoulizwa na Mungu, Kwanini umejificha?akamjibu nipo uchi, Mungu akamwambia adamu umejuaje kama upo uchi wakati sikuzote ulikuwa uchi na hujajiona na mimi niliyafunika macho yako iliusijione upo uchi. kwamana  umejua upo uchi basi kutakuwa na mtu mwingine anaye fanana na mimi Mungu.

Adamu akamwambia Mungu  umenipatia mwanamke bila kukuomba kwa hiyo huyu mwanamke uliye nipati,amekwenda na amekutana na shetani  wakaongea wakanipatia tunda akaniletea ndilo ambalo lilinifungua macho nikaona nipo uchi. Maandiko yanasema Mungu alipo anza kugawa adhabu Adamu alikuwa wa mwisho kupokea adhabu, wa kwanza alikuwa mwanamke, wapili shetani adamu akawa wa tatu, maana alikuwa yupo  kwenye namba ya tatu akijua baada ya namba tatu ya Adamu kuna namba tatu ya Masia atakae kaa ndani yake.

 
Maandiko yanasema baaada ya Adamu kujijua yupo uchi akajisikia aibu na yale macho yaliyo mwonyesha kuwa yupo uchi, yalikuja  kwa aina yake kule ndani na kuanza  kumuonyesha  vitu vingine tofauti, ambapo Mungu alikasirika na kuiziba njia ya kwenda kwenye mti wa uzima, alipo ifunika hiyo njia, zile njia nyingine zote ambazo yale macho yaliyo funguliwa yakawa yapo wazi kwa hiyo kila alichokuwa akikiona ndicho kilichokuwa kikimwingia.

Ukitaka kuwa na macho ya rohoni, kwanza unatakiwa kuwa na hekima ndani yako na msiri wa kila utakacho kiona ama kutokea mbele yako,pia unatakiwa kujua aina ya vyakula unavyo kula kwa maana  sikila chakula na kila nyama unatakiwa kula,  

KUTOKA 12:5 “Mwana kondoo wenu atakuwa hana ila,mume wa mwaka mmoja; mtamtwaa katika kondoo au  katika mbuzi. Nanyi mtamweka hata siku ya kumi na nne ya mwezi ule ule; na kusanyiko lote la Israel watamchinja jioni. Nao watatwaa baadhi ya damu yake na kuitia miimo miwili na katika kizingiti cha juu katika zile nyumba watakazo mla.Watakula nyama yake usiku ule ule,imeokwa motoni, pamoja na mkate usiotiwa chachu;tena pamoja na mboga zenye uchungu; msiile mbichi, wala ya kutokoswa majini,bali imeokwa moto;kichwa chake pamoja na miguu yake, na nyama zake za ndani”.

MWANZO 2.1” Mungu alipo umba kila kitu akawaleta wanyama mbele ya Adamu iliaone atawaitaje, na alipo tokea nyati na Adamu akasema ataitwa nyati na ika hivyo,Mungu hakupinga  Kwasababu macho aliyokuwa akiyatumia Adamu kipindi hicho atakacho kiona ndicho kitakacho tokea kwasababu yalikuwa ni macho ya Mungu ndiyo yapo ndani yake. Macho aliyofunguliwa macho ya aibu kwahiyo macho hayakuishia kuona uchi wa Adamu na Mke wa Adamu.na ndipo akaanza kuona zaidi akaona uchi akakimbia akahitaji nguo akavaa lakini kwa adamu hazikuwa na umuhimu.

Roho ikiwa kwenye mwili inaweza kumudu lakini mwili ukifa nafsi yako ikiwa inatoka kwenye mwili ikienda kwenye ulimwengu wa roho na kukaa na kujadilia kuhusu kesho utaona au kukuonyesho mambo gani yanatokea kesho, lakini utakuja kufahamu kwamba roho inataka lakini nafsi haiwezi kuvuka kwa sababu imezuia kwaajili nafsi ndiye mtu wa ndani na roho ya mtu inafanya kazi kupitia nafsi na mwili.

Ili roho iweze kusema ni rahisi roho yako kuamini umepona na roho yako ikaiambia nafsi mweleze mwili umepona na mwili atamwambia nafsi kamwambia roho anaamini kwake amepona lakini mimi huku kwangu inje bado mwili unauma, roho anamwambia nafsi kamwambie mwili imani bila matendo inakufa na asimame  sasa, kama mwili umeunganika na nafsi uponyaji wa roho hauwezi kuja kwenye mwili mpaka nafsi iunganike na roho ndipo mwili uwe sawa.kwamaana hazina ya mtu iliko ndio roho ilipo.

Mwanangu mimi Baba yako nataka ufike mahali huna kitu kinakusumbu kwenye ulimwengu wa mwili kwa sababu nina kutengeneza na kukuweka katika sehemu ambayo Mungu atajibu kwa upesi na kuwa na macho ya rohoni ambayo yanaweza kuona kila kitu bila kuambiwa na mtu,maana ulimi hauwezi kutamka kitu kama  macho hayaja ona.





1 comment:

Unknown said...

Thank you prophet!

I have learned a great lesson tonight. "Spiritua eyes" as topic, has touched me so much.

You quoted 2 kings 6:14,17, where we find the story of Elisha, the prophet of God and how he prayed to God for the eyes of Gehazi to be opened!

It means that sometimes God's children always fear because they do not SEE what has for them.

It's rare to hear these teachings and inspirational lessons in the church.

Most believers believe that the pastor is the only person that must have these spiritual eyes, and others do not bother to ask God to open their eyes so that they can see what God has in mind for them.

May the good lord grant you more revelations by which you can build up the body of christ.

Hallelujah.

Apostle Kuhanda J.N