SHILOH INTERNATIONAL MINISTRIES TANZANIA

Wednesday, August 13, 2014



SOMO: WATU AMBAO MBINGU ZIMEKAA KIMYA KWAAJILI YAO.
       Na:NABII FRANK JULIUS KILAWAH.

 Mbingu ni mlango au mfumo ambao Mungu anautumia kutunza na kukaa yeye mwenyewe kwaajili ya nchi. Pia tunaweza kusema Mbingu ni upeo wa Mungu katika mafundisho ya dini,ama upeo wa kiroho ambako nafsi za wafu hufikia baada ya kifo.

Mbinguni ni mahali ambapo mtakatifu Mungu wa Izrael anakaa


.
Katika kundi ambalo ninalizungumzia hapa la watu ambao mbingu zimekaa kinywa kwaajili yao.ni kundi ambalo hawatendi dhambi lakini wanahangaika kwenda kwa watumishi wa Mungu tofauti tofauti ilikupata nafasi ya kumaliza matatizo yao.jambo ambalo ni zuri lakini kwa upande mwingine sio zuri, ukienda kwa utaratibu huo utapotea lakini pia kukaa na mtumishi ambaye hamjui Mungu kwa muda mrefu itakudumaza akili yako.

Kwamaana hiyo unapo taka kukubalika ni lazima usimamie zamu yako,maana  kila mtumishi unaye muona chini ya jua amebeba maono ya Mungu kwa watu anaokubalika nao, na usipo jua wewe unataka nini na ndani mwako kumekosekana nini na niwapi utakipata, hivyo ni rahisi kusikiliza kilanayefundisha ukifikiri analo jibu la kwako.

Lakini ukijua wapi unapoelekea ili upate majibu ya matatizo yako, ukienda kwa aina hiyo utaelewa jinsi ya kuilinda roho yako lakini pia utafaniksha roho yako kukutana na unacho hitaji. 

UFUNUO 8:1.”Hata alipoifungua muhuri ya saba,kukawa kimya mbinguni kama muda wa nusu saa.Nami nikawaona wale malaika saba wasimamao mbele za Mungu,  nao wakapewa baragumu saba”.

Uwe tayari kuunganika na Mungu maana mbele yako kuna mtu ataachia nafasi kwaaji yako,maandiko yanasema muhuri wa saba ulipofunguliwa mbingu zote zikawa  kinywa, maana yake na ulimwengu wa roho ukawa kinywa kwasababu kiongozi wa ulimwengu wa roho ni mbingu na mbingu zimenyamaza kinywa kwamaana hiyo hata waombaji na wahubiri wote wapo kinywa.

Hivyo unatakiwa ujue nafasi yako ipo vipi, kwamaana huwezi kuachia vitu vingine vilivyokuwa ndani mwako ndio maana mbingu hazifunguki kwako na zimenyamaza kinywa. Pia kwaupande mwingine mbingu zinapo funga Mungu anaruhusu nafasi yaw ewe kushuka ili upate kubwa zaidi na malaika  ambao hawahitaji msaada wa mbingu wanahitaji wewe kuunganika nao ili unaposhindwa wawajibike kwako.

Unatakiwa kufaha mbinguni tunaenda kupumzika ili tuweze kwenda kwenye mbingu nyingine, hivyo mbingu inapo nyamaza nikupoteza muunganiko wa upande mmoja ilikuunganika upande mwingine,kwamaana hiyo upande wa pili ni kwaajili yako kuweza kuwajibika.

UFUNUO 9:1,2 “Malaika wa tano akapiga baragumu, nikaona nyota iliyotoka mbinguni, imeanguka juu ya nchi; naye akapewa ufunguo wa shimo la kuzimu. Akalifungua shimo la kuzimu;moshi ukapanda kutoka mle shimoni kama moshi wa tanuru kubwa;jua na anga vikatiwa giza kwasababu yaule moshi wa shimoni”.

Kwamaana hiyo mbingu haihitaji sapoti yoyote, mana mimi nimejenga ukuta mkubwa, mbingu haziwezi kufanya kitu chochote kwaajili nimesha jijengea ukuta na unanisaidia kujilinda na adui zangu.
Mwanangu kunawakati unaweza kuamka saa saba za usiku kuomba lakini mwili hautaki,usiogope,jua ni upande wa pili unakuja kwako na kupata kuunganika.elewa  mbingu zitakuwa zimenyamaza zinatafuta mafanikia ya upande wa pili kwako.

Saturday, August 9, 2014



SOMO: ULIMWENGU WA ROHO.
       Na: NABII FRANK JULIUS  KILAWAH.

 Ulimwengu wa roho, ni ulimwengu ambao hauonekani kwa macho ya kawaida bali mpaka uwe na macho ya rohoni au ulimwengu wa asili, mambo yanaanzia rohoni ndio yanaweza kudhihirika mwilini,ushindi wake unaanzia rohoni na baadae unaonekana katika ulimwengu wa mwili, na uhalisi wake ndani kuna watu wanaoishi huko.
Maana hata maombi tunayo omba kila siku ni namna ya mtu kwenda katika ulimwengu wa roho, kuwasiliana na Mungu wake na kuuathiri ulimwengu wa kipepo.ili kutimiza haja ya ombi lake mbele ya macho ya Mungu.

Kwa maana nyingine ulimwengu waroho ndio una fursa ya kuona mambo yanayoenda kutokea dunia, na kabla hayaja tokea ni kwenye ulimwemgu wa roho kwanza.
Maisha kabla hujazaliwa hayana hesabu na baada ya kufa pia hayana hesabu ila yenye hesabu ni haya baada ya kuzaliwa na kabla hujafa,na hesabu yake ni fupi sana maandiko ya sema ni miaka 80.lakini haya maisha yana hesabika katika kitabu cha Ayubu.

AYUBU 14:1,3. “Mwanadamu aliye zaliwa na mwanamke, siku zake za kuishi  si nyingi, naye hujaa tabu. Yeye huchanua kama vile ua kisha hukatwa; Hukimbia kama kivuli, wala hakai kamwe. Nawe, je! Wafumbua macho yako kumwangalia mtu kama yeye, na kunitia katika hukumu pamoja nawe?”.

Hili neno tabu kwa lugha nyingine, mtu aliyezaliwa siku zake zote zilizo baki ni za tabu, lakini mimi katika andiko hili nimeona kuna nafasi ya pili ambayo Ayubu hajaisema, kwamba siku za mwanadamu zimegawanyika katika sehemu mbili,ya kwanza ni raha pili ni shida.lakini inawezekana kwa upande wake alikuwa anajaribu kumwambia Mungu mimi sikustahili kunyanganywa mali zangu,kufiwa wala kuugua.
Mwanangu  nataka usimsome Ayubu kiroho bali umsome kimwili na kwa hisia za kibinadamu, na uondoe Roho mtakatifu na Mungu iliuweze kujua nini alikuwa anakimaanisha katika andiko.

Kwa maana Ayubu alitumia hekima ya wito, ambayo inapita kwenye moto na unajua mbele kuna msalaba ambao hauwezekani kwa akili za kibinadamu, lakini hekima ya wito unaweza ukamwambia kikombe hiki hakuna anayeweza kukinyweya ila ni mimi tu,hiyo ndio hekima ya wito lakini huku mwili wako haupo tayari.

Na kile kitendo cha Mungu kumsifia Ayubu mbele ya shetani ndipo shetani alipoanza kumpiga kwa majipu mwili mzima, na baada ya hapo Mungu alinyamaza na shetani alinyamaza na hakuweza kumuona hata mmoja.zaidi ya mkewe Ayubu na rafiki wake wa tatu.

AYUBU 2:7 “Basi shetani akatoka mbele za uso wa Bwana,akampiga Ayubu na majipu tangu wayo wa mguu hata utosi wa kichwa”.

Mwanangu ukiona unaakili nyepesi jua utakuwa na maisha marahisi, na ukiwa na akili nzito jua hata maisha yako yatakuwa magumu sasa ni wewe kuchagua wapi unaelekee simamia nafasi yako ili uweze kushinda majaribu ya shetani.

Thursday, August 7, 2014

MAFUTA YA UPAKO YATENDA MIUJIZA KWENYE NG'OMBE.


MAFUTA YA UPAKO YATENDA MIUJIZA KWENYE MIFUGO YA MR.STEVEN MBUJI.

Siku ya tarehe  05/08/2014 Mr. Steven Mbuji alipokea unabii kuhusu ng’ombe zake zilizokula majani maeneo ya makaburini ambapo uchawi ulifanyika kipindi cha nyuma, na ng’ombe aliyekuwa amekula majani hayo ni  ng’ombe dume.
Kutokana na ng’ombe dume huyo kula hayo majani roho ya kipepo ilimwingia na alipokuwa akiwapanda ng’ombe wengine alikuwa anapandikiza roho hiyo ndani mwao na  kupelekea ng’ombe hao jike kutokushika mimba japokuwa alikuwa anawapandisha na walikuwa wanaingia kwenye joto kama kawaida na walikuwa hawaonyeshi dalili zozote za kuwa na mimba kitu ambacho kilikuwa kinamshangaza Mr. Steven Mbuji.

 
              siku ya kwanza Mr. Steven Mbuji alopokuwa anapokea unabii wake.


Mr Steven Mbuji aliendelea kupokea unabii kutoka kwa Mtumishi wa Mungu Nabii Frank Julius Kilawah   kuwa kati ya  ng’ombe wako kuna mmoja mwenye jicho bovu, ambapo alikiri kuwa ni kweli anang’ombe mmoja  ambaye jicho lake ni bovu, kilichompelekea Mr Steven kupokea unabii kwa imani yote, baada ya hapo aliombewa na kupewa mafuta ya upako ambayo aliambiwa akawapake ng'ombe wake na baada ya hapo watatoa uchafu kisha watakuwa wamefunguliwa kabisa.

 
                 Mr. Steven akionyesha mafuta ya upako aliyowapaka ng'ombe zake.

Mnamo majira ya saa 10 jioni Mr Steven Mbuji alipiga simu kwenye ofisi ya Shiloh  Media na kuelezea kuwa baada ya kutumia mafuta ya upako aliyopewa na Nabii Frank Kilawah na kufanya kama alivyoelekezwa hatimaye ng’ombe  wake mmoja leo tarehe 07/08/2014 ameweza kuzaa ndama ambaye hajakamilika mwenye miezi saba ambapo siku 18 zilizopita alikuwa amempandisha. Kitu ambacho kilikuwa cha ajabu  na kilimshangaza sana, kitaalum ni kitu ambacho hakiwezekani lakini kupitia mafuta ya upako nguvu ya Mungu iliweza kujidhihirisha juu ya ng’ombe huyo.


 

 huyu ndiye ng'ombe aliyepakwa mafuta na baada ya kupakwa mafuta ndio akazaa ndama huyu.

 
                   huyu ndiye ndama aliyezaliwa baada ya kupakwa mafuta ya upako.

Sanjari ya hayo waandishi wa habari kutoka ofisi ya Shiloh media baada ya kupokea habari hiyo waliweza kufika eneo la tukio,  na  kuthibitisha unabii huo kuwa ni kweli ng’ombe huyo amezaa ndama dume na amefariki.
Tunaamini kuwa ni mwanzo wa kufunguliwa kwa mifugo yake yote kwasababu  mimba ile ilikuwa haionekani lakini baada tu ya kutumia mafuta ya upako aliweza kuzaa mimba ya muujiza.

Tunamshukuru Mungu kwa muujiza huu mkubwa kwa Mr Steven Mbuji kupitia mtumishi wa Mungu  Nabii Frank Julius Kilawah.
Hakika hakuna jambo gumu la kumshinda Bwana anayetenda miuijiza kwa wanadamu na hata wanyama .


 KWA IMANI YOTE YANAWEZEKANA.

MTUMISHI WA MUNGU NABII FRANK JULIUS KILAWAH



Tuesday, August 5, 2014

JIFUNZE KUHESHIMU NAFASI AMBAYO MUNGU AMEKUPATIA





JIFUNZE KUHESHIMU NAFASI AMBAYO MUNGU AMEKUPATIA.
Watu wengi wamekuwa wakidharau nafasi zao katika mahali ambapo Mungu amewaweka, na wakati mwingine inafika mtu kuacha kazi tu kwasababu nafasi ambayo aliyokuwa nayo yeye hakuitaka au kutoridhika au kutopandishwa cheo kwa muda ambao yeye aliona anastahili kupandishwa cheo. Na unashindwa kuelewa kuwa Mungu amekuweka mahali hapo kwa kusudi gani? Kama Mkristo lazima ujifunze kuishi kwa mtindo wa kumuuliza Mungu maswali  katika eneo  ulipo? Je huko mahali hapo kwa mpango na kusudi la Mungu? Na kama ndio  je? Ni kusudi gani  Mungu kukuweka mahali hapo na si mahali pengine na kama hapana je?  ni mahali gani ambapo yeye amekuandalia na kukusudia wewe uwepo?. ukienda kwa mtindo huu hauwezi kuacha kazi , biashara au jambo lolote la kwako unalolifanya kwasababu utaelewa kabisa umewekwa mahali pale kwa kusudi maalum la Mungu.

Neno la Mungu linasema katika  isaya  43:26 “ unikumbushe na tuhojiane ; eleza mambo yako, upate kupewa haki yako. Kama Mungu mwenyewe amesema njoo tuhojiane maana yake kuna vitu anataka kusikia kutoa kwako , na anaposema UPATE KUPEWA HAKI YAKO maana yake kuna haki nyingine haipatikani hivi hivi pasipo wewe kumwambia Mungu mfano umeonewa kazini  wenzako kila siku wanapadishwa cheo na msharaha halafu wewe uko katika kiwango kile kile cha mshahara na cheo,  ni wajibu wako uende mbele za Mungu na kumwambia haki yako unakosa mahali pale ili yeye awezekukutetea na ukapata haki yako.

Pia utakuta wapo watu wengine wanashindwa kuanzisha biashara au kuendeleza biashara zao kwanini kwasababu yupo mtu ambaye biashara yake ina jina kubwa au huyo mfanyabiashara jina lake ni kubwa na utakuta biashara yake haina ubora ila kinachomfanya biashara yake itoke ni jina lake ,  basi utakuta mtu anakata tamaa au anashindwa kuendelea kufanya biashra katika eneo hilo na kuenda kutafuta eneo lingine, swali la kujiuliza ni hili je?  utahama maeneo mangapi kwa kuogopa mtu biashara  yake inavyotoka.

Hupaswi kuogopa , lazima uelewe wakati unaanza biashara yako ni Roho Mtakatifu ndiye alisema na wewe kwahiyo hautofanya kwa akili zako bali utafanya kwa akili za Roho Mtakatifu na uwepo wake, kumbuka hakuna mtu Mungu anayemuwazia mabaya katika yeremia 29:11 inasema “ Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana ni mawazo ya amani wala si ya mabaya kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.” Kama Mungu amesema mwenyewe  hakuna mtu anayemuwazia mabaya maana yake hakuna mtu ambaye amepangiwa kufeli katika jambo lolote lile ambalo Mungu amemuagiza kufanya na akafanya sawasawa na  jinsi alivyomuagiza. Haleluyah..

            Ngoja tuangalie mfano mmoja wa mtu aliyeweza kuheshimu nafasi na mahali ambapo Mungu alimuweka.
1sam 16:1 “ BWANA akamwambia Samweli, hata lini utamlilia Sauli, ikiwa mimi nimemkataa asiwamiliki Israel? Ijaze pembe yako mafuta uende, nami  nitakupeleka kwa Yese, Mbethlehemi; maana nimejipatia mfalme katika wanawe.
Mungu anajaribu kumwambia Samweli asiendelee kumlilia mtu ambaye yeye tayari ameshamkataa na Roho yake haipo pamoja naye   na anajaribu kumuelekeza mahali pengine ambapo amejipatia mfamle huko, kuna kitu nataka uone Sauli ndiye alikuwa ni mfame katika nchi ya Israel na alikuwa hodari sana na maarufu kwasababu ya uwezo wake wa kupigana vita na kumcha Bwana, siku alipomkosea Bwana ndipo Mungu alipoamua kumuinua Mfalme mwingine japokuwa Sauli bado alikuwa mfalme ila uwepo wa Bwana haukuwa pamoja naye kwanini kwasababu tayari Mungu amemwambia Samweli nimejipatia mfalme mwingine.Kama Mungu alivyoweza kumchagua  Daudi  ikiwa Sauli bado alikuwa  ni mfalme  basi haina sababu ya wewe kuendelea kuogopa  kufanya biashara yako kwasababu huwezi kujua Mungu ameacha kuwabariki watu wangapi na amekuchagua wewe , huwezi kujua pia ameinua wateja wangapi kuja kwako. Daudi hakujua ni nini kinaendelea ila Mungu alijua ni kwanini alimuweka mahali pale kuchunga kondoo za kwako kwasababu Mungu alimpitisha katika shule ya kumuuwa dubu na simba kwa mikono yake ila yamkini Daudi hakujua ni kwanini yuko mahali pale ila baada ya kukutana na goliati ndipo Daudi aliweza kugundua kwanini Mungu alimuweka mahali pale kwanza na sehemu nyingine. Tatizo watu wengi kinachowafanya wakate tamaa ni kutokana na namna wanavyoangali nje  tofauti na jinsi Mungu anavyoaangalia ,

 Wakati mwingine mtu ameweka imani yake katika jambo flani na lile jambo linapokuja tofauti na yeye alivyodhani utakuta anakata tamaa na anashindwa kujua ni kitu gani afanye? Kumbuka wanafunzi wa Yesu walipoona Yesu ametuliza upepo Yesu aliwauliza Iko wapi Imani yenu? Wao walichojibu walimwambia Bwana tuongezee Imani, hawakusema nimekataa tamaa kwanini kwasababu kuna 
jambo/mambo mengine ambayo yanakuja juu ya kiwango chako cha Imani, sasa wewe huwapaswi kukata tamaa wala kulia unachotakiwa ni kumwambia Yesu niongezee Imani katika hilo jambo na wala si dhambi kuomba kuongezewa Imani. Nafasi au mahali ambapo Mungu amekuweka usiidharau kwasababu katika nafasi hiyihiyo ndogo ndipo Mungu anapoenda kukuinua, kumbuka hakuna vitu vikubwa vilivyoanza vikubwa vitu vyote vikubwa vimetokana na vidogo hivyo paheshimu heshimu mahali hapo huku ukiwa na bidii katika kazi yako na kumuomba Mungu kusudi lake likasimame mahali hapo.
                             
                   
       UBARIKIWE


 JOSHUA  1:5 HAPATAKUWA NA MTU YEYOTE ATAKAYEWEZA KUSIMAMA MBELE YAKO SIKU ZOTE ZA MAISHA YAKO”