SOMO: ULIMWENGU WA ROHO.
Na: NABII FRANK JULIUS KILAWAH.
Ulimwengu wa roho, ni ulimwengu ambao
hauonekani kwa macho ya kawaida bali mpaka uwe na macho ya rohoni au ulimwengu
wa asili, mambo yanaanzia rohoni ndio yanaweza kudhihirika mwilini,ushindi wake
unaanzia rohoni na baadae unaonekana katika ulimwengu wa mwili, na uhalisi wake
ndani kuna watu wanaoishi huko.
Maana hata maombi tunayo omba kila siku ni namna ya mtu
kwenda katika ulimwengu wa roho, kuwasiliana na Mungu wake na kuuathiri
ulimwengu wa kipepo.ili kutimiza haja ya ombi lake mbele ya macho ya Mungu.
Kwa maana nyingine ulimwengu waroho ndio una fursa ya kuona
mambo yanayoenda kutokea dunia, na kabla hayaja tokea ni kwenye ulimwemgu wa roho
kwanza.
Maisha kabla hujazaliwa hayana hesabu na baada ya kufa pia
hayana hesabu ila yenye hesabu ni haya baada ya kuzaliwa na kabla hujafa,na
hesabu yake ni fupi sana maandiko ya sema ni miaka 80.lakini haya maisha yana hesabika
katika kitabu cha Ayubu.
AYUBU 14:1,3. “Mwanadamu aliye zaliwa na mwanamke, siku
zake za kuishi si nyingi, naye hujaa
tabu. Yeye huchanua kama vile ua kisha hukatwa; Hukimbia kama kivuli, wala
hakai kamwe. Nawe, je! Wafumbua macho yako kumwangalia mtu kama yeye, na
kunitia katika hukumu pamoja nawe?”.
Hili neno tabu kwa lugha nyingine, mtu aliyezaliwa
siku zake zote zilizo baki ni za tabu, lakini mimi katika andiko hili nimeona
kuna nafasi ya pili ambayo Ayubu hajaisema, kwamba siku za mwanadamu
zimegawanyika katika sehemu mbili,ya kwanza ni raha pili ni shida.lakini inawezekana
kwa upande wake alikuwa anajaribu kumwambia Mungu mimi sikustahili kunyanganywa
mali zangu,kufiwa wala kuugua.
Mwanangu nataka
usimsome Ayubu kiroho bali umsome kimwili na kwa hisia za kibinadamu, na uondoe Roho mtakatifu na Mungu iliuweze kujua nini alikuwa anakimaanisha katika
andiko.
Kwa maana Ayubu alitumia hekima ya wito, ambayo
inapita kwenye moto na unajua mbele kuna msalaba ambao hauwezekani kwa akili za
kibinadamu, lakini hekima ya wito unaweza ukamwambia kikombe hiki hakuna
anayeweza kukinyweya ila ni mimi tu,hiyo ndio hekima ya wito lakini huku mwili
wako haupo tayari.
Na kile kitendo cha Mungu kumsifia Ayubu mbele ya
shetani ndipo shetani alipoanza kumpiga kwa majipu mwili mzima, na baada ya hapo
Mungu alinyamaza na shetani alinyamaza na hakuweza kumuona hata mmoja.zaidi ya
mkewe Ayubu na rafiki wake wa tatu.
AYUBU 2:7 “Basi shetani akatoka mbele za uso wa
Bwana,akampiga Ayubu na majipu tangu wayo wa mguu hata utosi wa kichwa”.
Mwanangu ukiona unaakili nyepesi jua utakuwa na maisha
marahisi, na ukiwa na akili nzito jua hata maisha yako yatakuwa magumu sasa ni
wewe kuchagua wapi unaelekee simamia nafasi yako ili uweze kushinda majaribu ya
shetani.
1 comment:
"Spirit world" is another topic I enjoy. In fact I can't thank you enough what I have gained from God through you.
Be anointed and protected!!
Post a Comment