SHILOH INTERNATIONAL MINISTRIES TANZANIA

Friday, October 24, 2014

MAFUNDISHO YA SEMINA YA NENO LA MUNGU YENYE KICHWA KINACHOSEMA

JINSI YA KUONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU.

Na. NABII FRANK JULIUS KILAWAH.  

                          Neno Roho si jina geni masikio mwa watu  na wala si jina baya . Tunaelewa kabisa kuwa Roho ni kitu ambacho hakina umbo ila Roho yenyewe inao uwezo wa kuongoza kitu chochote chenye umbo  ili kuweza kutimiza kusudi lake. Ninapozungumzia kuongozwa na Roho Mtakatifu ninamaanisha kuwa Roho Mtakatifu ndio kiongozi wako wa  kila kitu katika maisha yako haijalishi unapenda au haupendi. Wapo watu wengi wamemdharau Roho Mtakatifu kwa kuweka madaraja  kuwa Roho Mtakatifu ni mdogo kisa imeanza Baba, mwana ,Roho Mtakatifu wakati hakuna kitu kama hicho imekaa kwa majina ila ni watenda kazi pamoja na ndio maana maandiko yanatuambia katia mwanzo 1: 26 “Mungu akasema na tufanye mtu kwa mfano wetu…..” lile neno TUFANYE inaonyesha ni mtu zaidi ya mmoja na ndio maana dhambi zote zinasamahewa isipokuwa dhambi ya kumkashfu Roho Mtakatifu.
Nabii Frank Kilawah akifundisha.

Nini maana ya Roho Mtakatifu?
 Roho Mtakatifu ni Roho ya Mungu aliyoiachilia duniani mara baada ya Yesu kuondoka au  ni Nafsi ya tatu ya Utatu Mtakatifu .Japo kuwa wengi wanafikiri Roho Mtakatifu alikuja mara baada ya Yesu kuondoka ila uwepo wa Roho wa Mungu unatajwa toka  uumbaji wa ulimwengu. 
Mwanzo 1:1-2 “…..Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.”
Roho Mtakatifu  ndiye anayetengeneza mazingira ya mtu kuishi, Mungu anatengeneza mazingira kwanza kabla hajamtenegeza mtu kuishi  na ndio maana Mungu alimtengeneza mazingira kwanza ndio akamleta mwanadamu baadaye.  

Ngoja tutazame baadhi ya kazi za Roho Mtakatifu katika maisha yetu ya kila siku.

                   A)  KUTEMBEA PAMOJA NAYE KAMA RAFIKI.

 Tunajua kabisa kuwa kila mtu anarafiki, na kazi ya rafiki ni kusaidiana katika shida na raha. Hakuna mtu atakayempenda rafiki ambaye anampenda wakati wa raha peke yake na kipindi cha shida atamuacha, ndivyo alivyo  pia Roho Mtakatifu anataka unapoamua kuwa pamoja naye unaenda naye hatua kwa hatua, unafanya kazi naye pamoja na si siku ukiwa na tatizo ndio unamuita hawezi kukusaidia kwasababu kipindi chote hicho wewe uliamua kwenda peke yako mpaka ulipopata tatizo ndio namkumbuka.Biblia inatuambia katika  Yohana 14:26 "Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia"  lile neno  "MSAIDIZI "  ni mtu anayefanana naye na lile neno "ATAWAFUNDISHA YOTE " maana yake kuna vitu ambavyo Yesu alifundisha yeye anakuja kuweka msisitizo ndani mwako na kitu kipya ambacho hakuna mtu alishawahi kukisema (mafunuo mapya).

           Mtu hawezi kuwa msaidizi wako ikiwa wewe hauoneshi ushirikiano naye, lazima ujifunze kutambua uwepo wa Roho Mtakatifu kama msaidizi au rafiki ili chochote na muda wowote unaotaka msaada anakuwepo pamoja nawe, na unaelewa kabisa msaidizi anafanya kazi kubwa kuliko mhusika ndivyo itakavyokuwa kwako hakuna jambo utakalolifanya pasipo Roho Mtakatifu kukuruhusu yeye  ulifanye.

         Jifunze kujenga ushirika na Roho Mtakatifu, kwasababu Yeye ni mtu roho, kama vile wewe ulivyo ila Yeye hafungwi na mwili. Unaweza kumwomba jambo lolote naye akakupa maarifa ya kufanya na hatokuacha peke yako bali mtakuwa pamoja.

Waumini wakifurahi mafundisho
B)  HUNYAMAZISHA TAMAA AMBAZO HAZITOKANI NA YEYE.

Kazi ya Roho Mtakatifu ni kuhakikisha mwili wako hautamani chochote  mfano gari nk kwasababu mwili unatamani vitu vinavyoonekana kwenye  mwilini ambavyo havina faida ya sasa na pengine ya baadaye pia. Lakini Roho haitamani vya mwili inahakikisha inabeba vitu mahali ambapo Mungu anakaa na kuvichua vya Mungu  na kuvipeleka katika mwili. kwahiyo basi mtu anayeenda kwa mwili vitu vyake anavyovifanya ni tofauti na mtu anayeenda kwa Roho. wagalatia 5:16  “ Basi enendeni kwa Roho wala hamtazitamani kamwe tamaa za mwili” Na ndio maana watu wengine wanaoenda katika ulimwengu wa roho  huwa wanatafuta msaada kwa miungu mingine eidha kwa kutoa kafara au chochote kile ambacho wataagizwa wafanye ili  kuweza kuivuta hiyo roho  iweze kuwaingia na kuleta mafanikio ya rohoni yaweze kutokea kwenye mwili. Watu wanaotoa kafara hawatoi kafara ili wajenge nyumba ila wanatoa kafara ili waipate  roho, ili ile roho iwawezeshe kufanya mambo mbalimbali wanayoyataka hapa duniani.

 
          
             C)  KUACHILIA NGUVU JUU YA MTU.

matendo 1:7  “Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu……” Roho Mtakatifu anapokushuka juu yako huwa anaachilia nguvu na kipawa kipya ndani ya mtu..

matendo 2:1-3 “ ….. Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka…..” 

Roho Mtakatifu kuna maeneo huwa anakaa na huwa kuna namna anavyotengeneza ndani yako namna ya kufanya kazi pamoja naye.
 
     1)  Juu yako – Utumishi Matendo 2:2 

     2)Ndani yako – kwa ajili ya utoto wa Mungu   rumi 8:20

 
3) Pamoja na wewe – kukuongoza  Mdo 13:2 na Mdo 16:6-10


Yohana 14:16-17  “ ANAKAA KWENU NAYE ATAKUWA NDANI YENU” maana yake mazingira yote yeye atakuwepo  lazima ufike mahali utambue uwepo wa Roho Mtakatifu  katika nyumba yako, katika kazi zako na katika kila jambo lolote unalolifanya kwenye maisha yako. Anaposema Ulimwengu hauwezi kumpokea kwakuwa haumwoni wala haumtambui  kwa lugha nyingine tunaweza kusema Roho Mtakatifu  anaonekana kwa mtu anayetambua uwepo wake na nafasi yake katika maisha ya mtu, hawezi kuachilia nguvu kwa mtu ambaye na hayuko tayari kumpokea wala hajua nafasi yake au umuhimu wake.


 
LITAENDELEA……





Saturday, October 11, 2014

NAMNA YA KUTUMIA UVUMBA KUWEZA KUMILIKI ULIMWENGU WA ROHO


 Nabii. Frank J. Kilawah

Somo: Namna ya kutumia uvumba na kuweza kumiliki ulimwengu wa roho.

Uvumba ni nini?
              Ni aina ya manukato ambayo yanachomwa na kutoa moshi na ule moshi huwa na harufu nzuri ambayo inamleta Mungu wa kwako karibu yaani kama unamuabudu Mungu aliye hai anashuka mahali hapo na kama unaabudu miungu mingine anashuka mahali hapo. Uvumba hutokana na utomvu wa mti unaoitwa mbani  au manemane. Utomvu huo ukinganda hukusanya na kuhifadhiwa  kisha huchanganywa na vitu kama viungo, maua ili kutengeneza aina mbalimbali za manukato.

Ulimwengu wa Roho ni nini? 
              Ulimwengu wa roho ni  ulimwengu usioonekana ila ni ulimwengu ambao ni wa asili na upo. Na ndani ya ulimwengu wa roho kuna mji, nafasi ya mtu kubarikiwa ,waefeso 1:3  nk. Kila vinavyooneka vimetokana na vile visivyoonekana , mafanikio ya mwili yanatokana na mafanikio yaliyoanzia kwenye ulimwengu usioonekana yaan ulimwengu wa roho. Ndio sababu vile visivyoonekena ni vya kudumu milele na vinavyoonekana ni vya muda.
Nabii Frank Julius Kilawah
Watu wengi wamefundishwa au wamesikia kuwa kutumia uvumba ni dhambi au unawaita majini au wanaotumia uvumba ni waganga,wachawi na watu ambao wanaabudu miungu mingine. Kitu ambacho si kweli maana maandiko yanatuambia katika kutoka 30:8 “ Na haruni atakapoziwasha zile taa wakati wa jioni, ataufukiza, uwe uvumba wa DAIMA mbele za Bwana katika VIZAZI VYENU VYOTE”  lile neno DAIMA  maana yake yake ni milele haijalishi kuwa YESU alikuja au laa ila Mungu ameshaagiza kuwa lifanyike daima kwahiyo Mungu aliweka agano na wayahudi kwa namna ambavyo kuhani atakuwa akienda mbele zake kwa namna ya kufukiza uvumba. Mungu asingeweza kumwagiza Haruni kama hakuna kitu ambacho Mungu alikuwa anakitafuta katika vizazi vya kwako wakati wa maombi  kupitia ule  uvumba.

Kama ingekuwa kuvukiza uvumba ni dhambi basi Mungu asingemwambia Musa ijengwe madhabahu ya kufukiza uvumba, na kama Mungu alimuagiza Musa ijengwe madhabahu ya kuvukizia uvumba maana yake yapo maombi mengine hayawezi kujibiwa au kupokeleawa mbele za Mungu bila kuvukiza uvumba au tunaweza kusema  yapo maombi mengine lazima yaunganike na uvumba ili yaweze kupata kibali mbele za Mungu. Na  kazi ya uvumba ni kukamata uwepo wa hiyo Roho au unakusaidia kufanya Roho uliyopewa iwe inaishi mahali hapo na  sikuzote anayefukiza uvumba huwa ni kuhani na si mchungaji, nabii au mwalimu. Endapo mtu atakuwa anaomba  peke yake lazima aombe maombi ya kikuhani na mavazi anayopaswa kuvaa ni ya kikuhani kama ilivyokuwa kipindi cha kina Haruni na wanawe.

Lazima kama mkristo uwe na maarifa mengi ya  kumshusha Mungu katika maombi yako. Kuna mahali pengine hupaswi kuomba kama mtu wa kawaida unapaswa kuomba kama kuhani . na kazi ya kuhani ni kubeba maombi ya kwake na ya wengine yamkini wewe katika familia au ukoo wenu mambo hayaendi vizuri unachopaswa kufanya ni kuomba maombi ya kikuhani beba katika maombi  familia yako na kupitia wewe Mungu ataonekana kwenu. Katika  ufunuo 8:2-3  inasema “ nami nikaona wale malaika saba wasimamao mbele za Mungu, nao wakapewa baraganu saba 3. Na malaika mwingine akaja akasimama mbele ya madhabahu , mwenye chetezo cha dhahabu akapewa uvumba mwingi ili autie pamoja na maombi ya watakatifu wote juu ya madhabahu ya dhahabu iliyo mbele ya kiti cha enzi.”  Malaika wanaosimama mbele ya kiti cha enzi cha Mungu kazi yao ni kuchanganya maombi ya watakatifu na uvumba ili Mungu aweze kujibu sawasawa na jinsi walivyoomba watakatifu wake  na sio kwamba maombi ambayo haya uvumba hayajibiwi laa ila yapo maombi ambayo ukiomba lazima yaende na uvumba. Wakati Yesu anazaliwa mamajusi walipoona nyota kuwa ni ya tofauti ndipo walipochukua hatua na kwenda kumtazama Yesu huku wakibeba  zawadi ambazo ni manemane,uvumba na dhahabu.
Na sisi kama ukoo wa Yesu inatupasa kuwa na uvumba katika nyumba zetu na tujizoeshe kufanya maombi ya namna hiyo.
 
Ezekieli 1:5 anasema wazi nikaona viumbe hai vinne , na ufunuo 5:8 inasema kuwa kuna viumbe vinavyosimama mbele ya kiti cha enzi na wao pia kazi yao ni kubeba manukato ambayo ni maombi ya watakatifu kwa lugha nyingine tunaweza kusema tunapofanya maombi ya kikuhani mbele ya Mungu yanakuwa ni manukato.  Unapotumia uvumba  katika maombi unaipa nguvu nafsi yako  kuweza kumiliki lango la ulimwengu wa Roho. Ninaposema neno LANGO inamaana zipo mahali ambapo ROHO huwa zinatoka na kuingia. Kwa mfano mtu utakuta anafanya biashara na hiyo biashara haendi vizuri anachofanya anaenda kutafuta msaada katika ulimwengu wa giza(mganga) ili apewe ROHO itakayoweza kusaidia mwili katika sehemu aliyokwamwa katika biashara yake au kitu ili aweke katika hiyo biashara yake na iende vizuri.

Kwa mfano katika kitabu cha Mwanzo 1:26-27 kinasema Mungu alituumba kwa mfano wake  na biblia inatuambia kuwa Mungu ni Roho kwahiyo mfano wa sisi kufanana na Mungu ni  Roho na si mwili. Kwasababu hiyo basi ndani ya Roho ya mwanadamu kuna picha ya Mungu na kama umeokoka unapopata tatizo unakimbia kwa mtumishi wa Mungu na kama hujaokoka utaenda kwa mganga kutokana na ile Roho inayokaa ndani yako au kwa lugha nyingine tunaweza kusema ile Roho uliyofanana nayo au inayotawala ndani yako ndio itakusukuma wapi uende kupata msaada.
 
Wakati mwingine watu wanalalamika hawapati fedha  na wanashindwa kuelewa kuwa fedha ni roho , Mathayo 6:21 " Hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako” neno hazina ni maana yake ni fedha. Na watu wengi wanatembea  na maagano mfano Mungu alimwambia Musa afanye  uvumba na avae pete  jaribu kufikiri umekutana na watu wangapi wamevaa pete na umebadilishana nao fedha au unafanya biashara nao na wakati unafanya naye biashara yeye anaingia agano na fedha yako, na matokeo yake unakuja kugundua kuwa kiwango cha ufanyaji wako kazi ni tofauti na kipato unachokiingiza katika biashara zako.
Lazima ukienda kufanya kazi au biashara sehemu flani jifunze kuchunguza agano la mahali hapo kwasababu zipo ofisni nyingine zimewekwa maagano ya watu kutoendelea zaidi ya bosi, na matokeo yake unakuwa  mtumwa wa mahali hapo .
Utakuta kipo kitu ndani yako kinachompa faida bosi wako na wewe kinakumaliza ndani, yaani nafsi yako inanyonywa inazalisha upande wa pili na  inafifisha kwako jaribu kuangali mshahara unaopewa na maisha yako utakuta ni vitu viwili tofauti.

                
    Je! unajua kuwa kuna mahali ukifika katika kiwango cha kumtumikia Mungu, unaweza ukawa unasema na malaika? "nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika..." 1kor 13:1 maana yake tunao uwezo wa kuzungumza, kukaa na kuwatuma malaika sehemu yoyote nao wakafanya.
Maandiko yanatuambia wakati zekaria anaenda hekalu kuvukiza uvumba Malaika alimtokea na kusema naye juu ya mtoto atakayezaliwa? na jinsi atakavyokutokea Roho Mtakatifu atakupa uhakika ndani ya moyo wako ya kuwa ni Malaika wa Bwana na si pepo aliyejifanya ni malaika wa nuru.            Unapoingia katika maombi ya kikuhani, lazima pia uwe na neno la Mungu la kutosha ndani yako. wengi wamejikuta wanatoka na mafunuo baada ya kuomba, ambayo wameshindwa kuyatofautisha ikiwa hayo mafunuo ni ya Mungu au la.
        Ukiwa na neno la Mungu litakusaidia kujua ni Mungu au shetani ndio anayesema. Katika ulimwengu wa Roho Mungu anakaa na shetani pia anakaa, Zekaria wakati malaika anampa ujumbe na aliposhindwa kuamani waliweka agano la malaika kwamba hatasema (bubu) mpaka  pale Mungu alichokisema kupitia malaika kitapotokea, jaribu kufikiri ni shetani ndio anasema na wewe halafu ukashindwa kutofautisha na ukafanya kama alivyokuagiza.

Kumbuka katika uwepo wa Mungu na shetani pia yupo. Roho Mtakatifu akusaidie kuweza kupambanua sauti kati ya Mungu na shetani wakati unapokuwa katika maombi yako.


Mungu awabariki.

Thursday, October 2, 2014

MAPOKEZI YA NABII FRANK JULIUS KILAWA MKOANI KIGOMA

 
Nabii Frank Julius Kilawa akishuka kwenye ndege na kukanyaga kwa mara ya kwanza ardhi ya Kigoma.
          Nabii Frank Julius Kilawah akisalimiana na watu wa itifaki waliokuja kumpokea.


 

Muandishi wa habari kutoka Shiloh Media akiwahoji watu kuhusu ujio wa Mtumishi wa Mungu

         Wakazi wa Kigoma wakiwa uwanja wa ndege wa Kigoma kwa ajili ya mapokezi ya Nabii  Frank Julius Kilawah.


Mtumishi wa Mungu Nabii Frank Julius Kilawa akiutaza mkuki aliokabidhiwa na vijana wa Kigoma.

Nabii Frank Julius Kilawah akiwapungia kwa furaha wakazi wa Kigoma waliojitokeza kumlaki katika uwanja wa ndege.



 Msafara wa wakazi wa Kigoma waliojitokeza kumzindikiza Mtumishi wa Mungu Nabii Frank Julius Kilawah.
                                                   Karibu Mtumishi wa Mungu Kigoma.

                     Waandishi wa habari wakimuhoji Nabii Frank Julius Kilawah.
Wakazi wa Kigoma wakicheza nyimbo maalum ya kumkaribisha Nabii Frank Julius Kilawah
Furaha na Nderemo karibu mtumishi wa Mungu.
Nabii Frank Julius Kilawah akielekea kwenda kuwazungumza na  wakazi wa Kigoma.


     Nabii Frank Julius Kilawah akitoa neno la shukurani kwa wakazi wa Kigoma kwa upendo waliouonyesha kwake.