SHILOH INTERNATIONAL MINISTRIES TANZANIA

Saturday, October 11, 2014

NAMNA YA KUTUMIA UVUMBA KUWEZA KUMILIKI ULIMWENGU WA ROHO


 Nabii. Frank J. Kilawah

Somo: Namna ya kutumia uvumba na kuweza kumiliki ulimwengu wa roho.

Uvumba ni nini?
              Ni aina ya manukato ambayo yanachomwa na kutoa moshi na ule moshi huwa na harufu nzuri ambayo inamleta Mungu wa kwako karibu yaani kama unamuabudu Mungu aliye hai anashuka mahali hapo na kama unaabudu miungu mingine anashuka mahali hapo. Uvumba hutokana na utomvu wa mti unaoitwa mbani  au manemane. Utomvu huo ukinganda hukusanya na kuhifadhiwa  kisha huchanganywa na vitu kama viungo, maua ili kutengeneza aina mbalimbali za manukato.

Ulimwengu wa Roho ni nini? 
              Ulimwengu wa roho ni  ulimwengu usioonekana ila ni ulimwengu ambao ni wa asili na upo. Na ndani ya ulimwengu wa roho kuna mji, nafasi ya mtu kubarikiwa ,waefeso 1:3  nk. Kila vinavyooneka vimetokana na vile visivyoonekana , mafanikio ya mwili yanatokana na mafanikio yaliyoanzia kwenye ulimwengu usioonekana yaan ulimwengu wa roho. Ndio sababu vile visivyoonekena ni vya kudumu milele na vinavyoonekana ni vya muda.
Nabii Frank Julius Kilawah
Watu wengi wamefundishwa au wamesikia kuwa kutumia uvumba ni dhambi au unawaita majini au wanaotumia uvumba ni waganga,wachawi na watu ambao wanaabudu miungu mingine. Kitu ambacho si kweli maana maandiko yanatuambia katika kutoka 30:8 “ Na haruni atakapoziwasha zile taa wakati wa jioni, ataufukiza, uwe uvumba wa DAIMA mbele za Bwana katika VIZAZI VYENU VYOTE”  lile neno DAIMA  maana yake yake ni milele haijalishi kuwa YESU alikuja au laa ila Mungu ameshaagiza kuwa lifanyike daima kwahiyo Mungu aliweka agano na wayahudi kwa namna ambavyo kuhani atakuwa akienda mbele zake kwa namna ya kufukiza uvumba. Mungu asingeweza kumwagiza Haruni kama hakuna kitu ambacho Mungu alikuwa anakitafuta katika vizazi vya kwako wakati wa maombi  kupitia ule  uvumba.

Kama ingekuwa kuvukiza uvumba ni dhambi basi Mungu asingemwambia Musa ijengwe madhabahu ya kufukiza uvumba, na kama Mungu alimuagiza Musa ijengwe madhabahu ya kuvukizia uvumba maana yake yapo maombi mengine hayawezi kujibiwa au kupokeleawa mbele za Mungu bila kuvukiza uvumba au tunaweza kusema  yapo maombi mengine lazima yaunganike na uvumba ili yaweze kupata kibali mbele za Mungu. Na  kazi ya uvumba ni kukamata uwepo wa hiyo Roho au unakusaidia kufanya Roho uliyopewa iwe inaishi mahali hapo na  sikuzote anayefukiza uvumba huwa ni kuhani na si mchungaji, nabii au mwalimu. Endapo mtu atakuwa anaomba  peke yake lazima aombe maombi ya kikuhani na mavazi anayopaswa kuvaa ni ya kikuhani kama ilivyokuwa kipindi cha kina Haruni na wanawe.

Lazima kama mkristo uwe na maarifa mengi ya  kumshusha Mungu katika maombi yako. Kuna mahali pengine hupaswi kuomba kama mtu wa kawaida unapaswa kuomba kama kuhani . na kazi ya kuhani ni kubeba maombi ya kwake na ya wengine yamkini wewe katika familia au ukoo wenu mambo hayaendi vizuri unachopaswa kufanya ni kuomba maombi ya kikuhani beba katika maombi  familia yako na kupitia wewe Mungu ataonekana kwenu. Katika  ufunuo 8:2-3  inasema “ nami nikaona wale malaika saba wasimamao mbele za Mungu, nao wakapewa baraganu saba 3. Na malaika mwingine akaja akasimama mbele ya madhabahu , mwenye chetezo cha dhahabu akapewa uvumba mwingi ili autie pamoja na maombi ya watakatifu wote juu ya madhabahu ya dhahabu iliyo mbele ya kiti cha enzi.”  Malaika wanaosimama mbele ya kiti cha enzi cha Mungu kazi yao ni kuchanganya maombi ya watakatifu na uvumba ili Mungu aweze kujibu sawasawa na jinsi walivyoomba watakatifu wake  na sio kwamba maombi ambayo haya uvumba hayajibiwi laa ila yapo maombi ambayo ukiomba lazima yaende na uvumba. Wakati Yesu anazaliwa mamajusi walipoona nyota kuwa ni ya tofauti ndipo walipochukua hatua na kwenda kumtazama Yesu huku wakibeba  zawadi ambazo ni manemane,uvumba na dhahabu.
Na sisi kama ukoo wa Yesu inatupasa kuwa na uvumba katika nyumba zetu na tujizoeshe kufanya maombi ya namna hiyo.
 
Ezekieli 1:5 anasema wazi nikaona viumbe hai vinne , na ufunuo 5:8 inasema kuwa kuna viumbe vinavyosimama mbele ya kiti cha enzi na wao pia kazi yao ni kubeba manukato ambayo ni maombi ya watakatifu kwa lugha nyingine tunaweza kusema tunapofanya maombi ya kikuhani mbele ya Mungu yanakuwa ni manukato.  Unapotumia uvumba  katika maombi unaipa nguvu nafsi yako  kuweza kumiliki lango la ulimwengu wa Roho. Ninaposema neno LANGO inamaana zipo mahali ambapo ROHO huwa zinatoka na kuingia. Kwa mfano mtu utakuta anafanya biashara na hiyo biashara haendi vizuri anachofanya anaenda kutafuta msaada katika ulimwengu wa giza(mganga) ili apewe ROHO itakayoweza kusaidia mwili katika sehemu aliyokwamwa katika biashara yake au kitu ili aweke katika hiyo biashara yake na iende vizuri.

Kwa mfano katika kitabu cha Mwanzo 1:26-27 kinasema Mungu alituumba kwa mfano wake  na biblia inatuambia kuwa Mungu ni Roho kwahiyo mfano wa sisi kufanana na Mungu ni  Roho na si mwili. Kwasababu hiyo basi ndani ya Roho ya mwanadamu kuna picha ya Mungu na kama umeokoka unapopata tatizo unakimbia kwa mtumishi wa Mungu na kama hujaokoka utaenda kwa mganga kutokana na ile Roho inayokaa ndani yako au kwa lugha nyingine tunaweza kusema ile Roho uliyofanana nayo au inayotawala ndani yako ndio itakusukuma wapi uende kupata msaada.
 
Wakati mwingine watu wanalalamika hawapati fedha  na wanashindwa kuelewa kuwa fedha ni roho , Mathayo 6:21 " Hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako” neno hazina ni maana yake ni fedha. Na watu wengi wanatembea  na maagano mfano Mungu alimwambia Musa afanye  uvumba na avae pete  jaribu kufikiri umekutana na watu wangapi wamevaa pete na umebadilishana nao fedha au unafanya biashara nao na wakati unafanya naye biashara yeye anaingia agano na fedha yako, na matokeo yake unakuja kugundua kuwa kiwango cha ufanyaji wako kazi ni tofauti na kipato unachokiingiza katika biashara zako.
Lazima ukienda kufanya kazi au biashara sehemu flani jifunze kuchunguza agano la mahali hapo kwasababu zipo ofisni nyingine zimewekwa maagano ya watu kutoendelea zaidi ya bosi, na matokeo yake unakuwa  mtumwa wa mahali hapo .
Utakuta kipo kitu ndani yako kinachompa faida bosi wako na wewe kinakumaliza ndani, yaani nafsi yako inanyonywa inazalisha upande wa pili na  inafifisha kwako jaribu kuangali mshahara unaopewa na maisha yako utakuta ni vitu viwili tofauti.

                
    Je! unajua kuwa kuna mahali ukifika katika kiwango cha kumtumikia Mungu, unaweza ukawa unasema na malaika? "nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika..." 1kor 13:1 maana yake tunao uwezo wa kuzungumza, kukaa na kuwatuma malaika sehemu yoyote nao wakafanya.
Maandiko yanatuambia wakati zekaria anaenda hekalu kuvukiza uvumba Malaika alimtokea na kusema naye juu ya mtoto atakayezaliwa? na jinsi atakavyokutokea Roho Mtakatifu atakupa uhakika ndani ya moyo wako ya kuwa ni Malaika wa Bwana na si pepo aliyejifanya ni malaika wa nuru.            Unapoingia katika maombi ya kikuhani, lazima pia uwe na neno la Mungu la kutosha ndani yako. wengi wamejikuta wanatoka na mafunuo baada ya kuomba, ambayo wameshindwa kuyatofautisha ikiwa hayo mafunuo ni ya Mungu au la.
        Ukiwa na neno la Mungu litakusaidia kujua ni Mungu au shetani ndio anayesema. Katika ulimwengu wa Roho Mungu anakaa na shetani pia anakaa, Zekaria wakati malaika anampa ujumbe na aliposhindwa kuamani waliweka agano la malaika kwamba hatasema (bubu) mpaka  pale Mungu alichokisema kupitia malaika kitapotokea, jaribu kufikiri ni shetani ndio anasema na wewe halafu ukashindwa kutofautisha na ukafanya kama alivyokuagiza.

Kumbuka katika uwepo wa Mungu na shetani pia yupo. Roho Mtakatifu akusaidie kuweza kupambanua sauti kati ya Mungu na shetani wakati unapokuwa katika maombi yako.


Mungu awabariki.

6 comments:

Unknown said...

Amen, Mungu azidi kuinua huduma ya Shiloh International Ministries Tanzania na mtumishi wake baba yetu Prophet Julias Kilawah hakika Mungu unaemtumikia ni Mungu aliye hai Milele na Enzi zote. Asante sana kwa kunifumbua macho ya kiroho na Mungu anisaidie Nizishike sheria zake na kumtumikia kwa ukamilfu wangu wote

Unknown said...

Amen uwepo wako ndani ya ulimwengu huu umekua mwl bora na kiongozi hasa kwa yule anaye kufatria nakuyashika mafundisho yako lazima atafunguliwa kwa namna yoyote ile.Mungu azidi kukuinuwa katika viwango vikubwa zaid na Huduma yako ndani ya Shiloh International Ministries ikawe kubwa Zaidi ya sasa Roho wa Mungu azidi kuimarisha jina lako ee Baba yetu Nabii Frank Julius Kilawah nasi nami najiungamanisha nawe

Anonymous said...

Hili fundisho???

Anonymous said...

Uvumba tena ndani ya Agano jipya? Tatizo hapa ni namna ya kuitafsiri biblia ki u sahihi,.

Anonymous said...

Yesu alikabidhiwa uvumba alipozaliwa. Hiyo ni agano jipya.

Anonymous said...

Amen