JINSI YA KUONGOZWA
NA ROHO MTAKATIFU.
Na. NABII FRANK JULIUS KILAWAH.
Neno
Roho si jina geni masikio mwa watu na
wala si jina baya . Tunaelewa kabisa kuwa Roho ni kitu ambacho hakina umbo ila Roho
yenyewe inao uwezo wa kuongoza kitu chochote chenye umbo ili kuweza kutimiza kusudi lake. Ninapozungumzia
kuongozwa na Roho Mtakatifu ninamaanisha kuwa Roho Mtakatifu ndio kiongozi wako
wa kila kitu katika maisha yako
haijalishi unapenda au haupendi. Wapo watu wengi wamemdharau Roho Mtakatifu kwa
kuweka madaraja kuwa Roho Mtakatifu ni mdogo
kisa imeanza Baba, mwana ,Roho Mtakatifu wakati hakuna kitu kama hicho imekaa
kwa majina ila ni watenda kazi pamoja na ndio maana maandiko yanatuambia katia
mwanzo 1: 26 “Mungu akasema na tufanye mtu kwa mfano wetu…..” lile
neno TUFANYE
inaonyesha ni mtu zaidi ya mmoja na ndio maana dhambi zote zinasamahewa
isipokuwa dhambi ya kumkashfu Roho Mtakatifu.
Nabii Frank Kilawah akifundisha. |
Nini
maana ya Roho Mtakatifu?
Roho
Mtakatifu ni Roho ya Mungu aliyoiachilia duniani mara baada ya Yesu kuondoka
au ni Nafsi ya tatu ya Utatu Mtakatifu .Japo
kuwa wengi wanafikiri Roho Mtakatifu alikuja mara baada ya Yesu kuondoka ila uwepo
wa Roho wa Mungu unatajwa toka uumbaji
wa ulimwengu.
Mwanzo 1:1-2 “…..Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.”
Roho
Mtakatifu ndiye anayetengeneza mazingira
ya mtu kuishi, Mungu anatengeneza mazingira kwanza kabla hajamtenegeza mtu
kuishi na ndio maana Mungu alimtengeneza
mazingira kwanza ndio akamleta mwanadamu baadaye.
Ngoja
tutazame baadhi ya kazi za Roho Mtakatifu katika maisha yetu ya kila siku.
A) KUTEMBEA PAMOJA NAYE KAMA RAFIKI.
Tunajua kabisa kuwa kila mtu
anarafiki, na kazi ya rafiki ni kusaidiana katika shida na raha. Hakuna mtu
atakayempenda rafiki ambaye anampenda wakati wa raha peke yake na kipindi cha
shida atamuacha, ndivyo alivyo pia Roho
Mtakatifu anataka unapoamua kuwa pamoja naye unaenda naye hatua kwa hatua,
unafanya kazi naye pamoja na si siku ukiwa na tatizo ndio unamuita hawezi
kukusaidia kwasababu kipindi chote hicho wewe uliamua kwenda peke yako mpaka
ulipopata tatizo ndio namkumbuka.Biblia inatuambia katika Yohana 14:26 "Lakini huyo Msaidizi, huyo
Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na
kuwakumbusha yote niliyowaambia"
lile neno "MSAIDIZI " ni mtu
anayefanana naye na lile neno "ATAWAFUNDISHA
YOTE " maana yake kuna vitu ambavyo Yesu alifundisha yeye anakuja
kuweka msisitizo ndani mwako na kitu kipya ambacho hakuna mtu alishawahi
kukisema (mafunuo mapya).
Mtu hawezi kuwa msaidizi wako ikiwa
wewe hauoneshi ushirikiano naye, lazima ujifunze kutambua uwepo wa Roho
Mtakatifu kama msaidizi au rafiki ili chochote na muda wowote unaotaka msaada
anakuwepo pamoja nawe, na unaelewa kabisa msaidizi anafanya kazi kubwa kuliko
mhusika ndivyo itakavyokuwa kwako hakuna jambo utakalolifanya pasipo Roho Mtakatifu
kukuruhusu yeye ulifanye.
Jifunze kujenga ushirika na Roho
Mtakatifu, kwasababu Yeye ni mtu roho, kama vile wewe ulivyo ila Yeye hafungwi
na mwili. Unaweza kumwomba jambo lolote naye akakupa maarifa ya kufanya na
hatokuacha peke yako bali mtakuwa pamoja.
Waumini wakifurahi mafundisho |
Kazi
ya Roho Mtakatifu ni kuhakikisha mwili wako hautamani chochote mfano gari nk kwasababu mwili unatamani vitu
vinavyoonekana kwenye mwilini ambavyo
havina faida ya sasa na pengine ya baadaye pia. Lakini Roho haitamani vya mwili
inahakikisha inabeba vitu mahali ambapo Mungu anakaa na kuvichua vya Mungu na kuvipeleka katika mwili. kwahiyo basi mtu
anayeenda kwa mwili vitu vyake anavyovifanya ni tofauti na mtu anayeenda kwa Roho.
wagalatia
5:16 “ Basi enendeni kwa Roho wala
hamtazitamani kamwe tamaa za mwili” Na ndio maana watu wengine wanaoenda katika ulimwengu
wa roho huwa wanatafuta msaada kwa miungu
mingine eidha kwa kutoa kafara au chochote kile ambacho wataagizwa wafanye
ili kuweza kuivuta hiyo roho iweze kuwaingia na kuleta mafanikio ya rohoni
yaweze kutokea kwenye mwili. Watu wanaotoa kafara hawatoi kafara ili wajenge
nyumba ila wanatoa kafara ili waipate roho, ili ile roho iwawezeshe kufanya mambo
mbalimbali wanayoyataka hapa duniani.
C) KUACHILIA NGUVU JUU YA MTU.
matendo 1:7 “Lakini
mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu……” Roho Mtakatifu anapokushuka juu
yako huwa anaachilia nguvu na kipawa kipya ndani ya mtu..
matendo 2:1-3 “ …..
Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho
alivyowajalia kutamka…..”
Roho Mtakatifu kuna maeneo huwa
anakaa na huwa kuna namna anavyotengeneza ndani yako namna ya kufanya kazi
pamoja naye.
1) Juu yako – Utumishi Matendo 2:2
2)Ndani yako – kwa ajili ya utoto wa Mungu rumi 8:20
3) Pamoja na wewe – kukuongoza Mdo 13:2 na Mdo 16:6-10
Yohana 14:16-17 “ ANAKAA KWENU NAYE ATAKUWA NDANI YENU” maana yake mazingira yote yeye atakuwepo lazima ufike mahali utambue uwepo wa Roho Mtakatifu katika nyumba yako, katika kazi zako na katika kila jambo lolote unalolifanya kwenye maisha yako. Anaposema Ulimwengu hauwezi kumpokea kwakuwa haumwoni wala haumtambui kwa lugha nyingine tunaweza kusema Roho Mtakatifu anaonekana kwa mtu anayetambua uwepo wake na nafasi yake katika maisha ya mtu, hawezi kuachilia nguvu kwa mtu ambaye na hayuko tayari kumpokea wala hajua nafasi yake au umuhimu wake.
LITAENDELEA………
No comments:
Post a Comment