SHILOH INTERNATIONAL MINISTRIES TANZANIA

Monday, June 23, 2014

JINSI NAFSI ILIVYO HARIBIKA KWA VITU ..

SOMO:  NAFSI  ILIVYO  HARIBIKA  KWA VITU VIWILI.

      Na:  NABII  FRANK  JULIUS  KILAWAH.

Neno “nafsi “ linamaana ya mwili wa nje na ndani wa mwanadamu, mbali na mwanadamu  kuwa na roho pia ni nafsi  katika maana yake  ya kawaida , neno “nafsi” linamaanisha “ uhai” ingawa zaidi ya hii  maana kuu , Bibilia inazungumzia nafsi katka maana mbalimbali, na moja wapo ya hizi ni nia  ya mwanadamu kutenda  dhambi.na nafsi  zetu zime jeruhiwa na kuharibika kwaajili  hiyo.


Vitu viwili vilivyo haribu nafsi za watu, Moja nafsi inaharibika kwa kitu unacho kisikia na cha pili  ni kile kitu unacho kiona kwa macho ya kwako na hukupaswa kukiona  wala  kukisikia kwa mana kitaharibu nafsi yako, Kwa maana  hiyo hayupo mtu anaye weza kuibadilisha nafsi yako zaidi ya yeye aliye ifanya nafsi kuwepo, ni Mungu pekee.hata mwanadamu akibadilisha nafsi yako  ataharibu ya nje lakini ya ndani  itaumia tu.

Wapo watu wengi nafsi zao zimeharibika na wamebaki wakilalamika na kuwa na roho ya hasira, kupaniki, hawana stori nzuri za kuongea,wana mchukia mtu kwa ghafla  na hata histori ya maisha yao imeharibika.

ZABURI 35:1 “Ee BWANA, utete nao wanaoteta  nami, Upigane nao wanaopigana nami. Ushike ngao na kigao, usimame unisaidie.Uutoe na mkuki uwapinge wanaonifuatilia, Uiambie nafsi yangu, mimi ni wokovu wako”.

Maandiko yanaonyesha jinsii Daudi alivyo jigawanya kwenye makundi mawili, la kwanza ni pale anapo sema Bwana pigana nao wanao pigana nami, la pili amejiona kwamba anapigana na vita anavyo vipiga lakini nafsi yake imenyamaza  na haiwezi kumsidia vita vinavyoendelea.ndipo Daudi alipo mwambia Mungu sema na nafsi yangu na uiambie wewe ni wokovu wako. Ili mimi nipigane nje na  nafsi ipigane kama ninavyo pigana mimi.

Ukisoma vizuri na kuelewa maneno ya Paulo utagundua kuna watu wawili wa nje na ndani, wanje anachakaa na akichakaa anampatia  nafasi wa ndani afanye upya kipindi cha mabadiliko kinachofanyika kule ndani iliyule wa ndani awe mpya , nje ni lazima kusinyae ni kwasababu Yule yupo gereji anafanyiwa kazi upya iliatokea na vita ya kumsaidia  wa nje.

Kama tunavyo soma na kuona  wapo watu wawili wa ndani na nje, hivyo ni muhimu sana kusikiliza nafsi yako inasema nini , maana unavyo sikia na kujiona ni vitu viwili tofauti, na hakuna kitu kibaya katika maisha yako kama kutokuelewa nafsi yako ipoje,  hayupo mtu anaye weza kuibadilisha nafsi yako zaidi ya  yeye aliye itengeneza nafsi  na kufa msalabani  kwaajili  yako.

ZABURI 35:4 “Waaibishwe, wafedheheshwe, wanaoitafuta nafsi yangu. Warudishwe nyuma, wafadhaishwe, wanaonizuria mabaya. wawe kama makapi  mbele ya upepo , malaika wa Bwana  akiwafuatilia , maana bila sababu wamenifichia  wavu,, Bila sababu wameichimbia shimo nafsi yangu”.

Kuokoka ni sawa na kuondoa nafsi ya kabila la kwenu na utaichukuwa nafsi isiyo chakaa ya Yesu kristo, ndio itakaa huko ndani  kwako, lakini katika kipindi hicho watatokea watu wengi watasema wanachokisema lakini ndani  kwako jua yanafanyika mabadiliko makubwa. Nafsi  yako ina kazi  ya  kuzalisha  na inaweza ikakata mawasiliano na Mungu  wakati akili  zako bado zinawasiliana na Mungu, kwasababu usingeweza kutegemea kama Daudi aliweza kumwambia Mungu  azungumze na  nafsi yake.


ZABURI 35:9 “Na nafsi yangu itamfurahia BWANA, Na kuushangilia wokovu  wake”.

Friday, June 20, 2014

ROHO YA UOGA

JUMA TANO 18/05/2014

SOMO: ROHO YA UOGA

Na: NABII   FRANK JULIUS KILAWAH.

Roho ya uoga  inaleta giza karibu yako na kukuweka mbali na uwepo wa Mungu, na  kuwapatia nafasi adui zako waweze kufanya kitu chochote unacho kifanya wewe na kupata nguvu pale tu unapokuwa na roho ya uoga mbele zao,,na kukufanya uangalie wingi wa adui zako katika kila jambo unalo fikilia kulifanya na kupelekea kushindwa kwasababu umebeba roho ya uoga.



Hutakiwi kuwa na roho ya uoga wala kusikiliza vitu vinavyo ogopesha, maana hata maombi hutaweza kupokea na kumwamsha mtu yule ambaye hana imani ndani yake,na kuto kuogopa kwako kutakufanya umalize wingi wa adui zako,  ushindi ndio unatakiwa kuzunguka akili zako na kuupata kwa wakati ulioutaka sio kuwa na uoga.

YOSHUA 1:6,7 “Uwe hodari na moyo wa ushujaa, maana ni wewe utakaye warithisha watu hawa nchi hii niliyo waapia  baba zao ya kwamba nitawapa. Uwe hodari tu na shujaa mwingi, uangalie na kutenda sawasawa na sheria yote aliyokuamuru Musa, mtumishi wa Mungu;usiiache,kwenda mkono wa kulia wala kushoto,upate kufanikiwa sana kila uendako”.

Tunaona katika bibilia jiinsi Mungu anavyotoa agizo, na agizo hili halikutolewa kwa wayahudi wote bali lilitolewa kwa mtu aliyepewa majukumu,hivyo wayahudi hawakuagizwa wawe na roho ya kishujaa lakini aliyetakiwa kuwa na roho ya kishujaa ni kiongozi wao aliye pewa majukumu na ndiye atakae ongoza watu kwenda kanani.

Kama Mungu aliweza kutoa agizo usiwe na roho ya uoga basi mambo yanayo kuja mbele yako yatakuwa yanaogopesha, hata kwa nje yatakuwa yanaogopesha kwa sababu hiyo utakuwa ukiangalia kushoto na kulia utakuwa huoni uwepo wa Mungu, maandiko yana niambia Mungu alimwambia Yoshua usiogope nipo pamoja nawe kwa hiyo kwa lugha nyingine kwenye hiyo safari kitakachokuwa kinaonekana  mara zote ni matatizo na yatakuwa mengi tofauti na uwepo wa Mungu.

Uwepo wa Mungu utaonekana baada ya wewe kuingia katikati ya vinavyo ogopesha kutokuviogopa,maana alitoa agizo kile kitendo cha kutokuogopa vinavyo ogopesha sio cha kufanya maombi,wa kufanga, bali kitendo cha wewe kutokuogopa kina leta uwepo wa Mungu aliyesema usiogope  katikati ya vinavyo ogopesha,na utaibeba roho yangu ya kuto kuogopa na nitakutetea na kukulinda katikati yako, maana hata ukifanya maombi hawezi kutokea mana sijakuagiza ufanye hivyo.

YOSHUO1:9 “Je! Si mimi niliye kuamuru? Uwe hodari na moyo wa ushujaa; usiogope wala usifadhaike; kwa kuwa Bwana, Mungu wako, yu pamoja nawe kila uendako”.

Mwanangu nakuambia jua katika maisha yako kuna maeneo mengine sio ya Yesu lazima yawe ya kwako, kwa maana yeye amesha maliza na kutoa kibali cha wewe kutokuogopa,sasa funga roho ya uoga chukua roho ya ujasiri na uende nayo, kitendo cha wewe kutokuogopa kinainua upendo wa Mungu katikati yako na kuweza kufikia malengo yako katika eneo hilo.


Roho ya uoga inakufanya umuondoe Mungu katikati ya maisha yako na kukuzuia usipanuke kiakili na mawazo maana kila unalotaka kulifanya unaogopa na mahali popote unapo kuwa na uoga ndipo nguvu ya Mungu inapatikana.hivyo ni vyema kuondoa roho yoyote ya uoga ili uweze kufikia halifulani katika ulimwengu wa roho.

Wednesday, June 18, 2014



JUMANNE 17/05/2014
SOMO: NGUVU ZA GIZA

Na:  NABII FRANK   JULIUS KILAWAH.

Maana ya nguvu za giza.Ni akili za watu ambazo zimefunikwa  na haziwezi kitu fulani ndani yake,na hukaa na kufanya kazi ndani ya mtu muongo,na roho ya uongo inaleta karibu nguvu za giza,na kudili  nazo inahitaji ujasili maana uoga unasababisha adui zako kukipata kile unachokitafuta na chochote unachokiogopa ndicho kitakacho kutokea, ni lazima unachokifanya kitetemeshe watu.

Giza ni kitu kinacho funika kitu kisionekane, ndivyo ambavyo maandiko yanatuambia, maana giza ndani yake linalo uwezo wa kubadilisha kitu hatakama kipo wazi,na tunapo zungumzia habari za giza sio tunazungumzia usiku peke yake, bali akili fulani iliyofunikwa ndani ya akili za watu ambayo haiwezi kujua nini kifanyike na kiweze kutokea.pia  nguvu ni kitu kinacho lazimisha kitu kingine kiweze kutokea.

MWANZO 1:1,3. “Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. Nayo nchi ilikuwa ukiwa,tena utupu,na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru. Mungu akaiona nuru,yakuwa ni njema;Mungu akatengeneza nuru na giza”.

Kutanda kwa giza maana yake giza halikuumbwa, bali lilikuwepo lakini nuru ilikuwepo na iliubwa, maandiko hayatuambii giza lilitoka wapi lakini yanatuelezea nuru ilitoka wapi, kwamaana wa kwanza kutengeneza nuru ni Mungu, na Mungu akasema kuwe nuru na ikawa nuru lakini haikuweza kumaliza giza lote.

Tunapo zungumzia habari za nguvu za giza kwa maana nyingine tunazungumzia habari za wachawi, maana  wachawi wanakaa kwenye nguvu za giza,kila unacho taka kukifanya na wachawi wanataka kufanya pia kama wewe, na sio kwako wewe tu, bali hata mimi Baba yako Nabii Frank Julius Kilawah ninapo hubiri na kutoa unabii basi wachawi nao huwa nyanyua wa chawi wengine wahubiri injili kinyume na mimi, kwa maana hiyo hata nikitoa unabii wa mtu kupata mimba na mganga wa kienyeji naye atatafuta dawa na kumpatia mtu apate mimba.yote ilikumeza miujiza ya Mungu ninaye mtumikia.

Mwanangu ninayo fimbo ya kumeza anayetabiri kwa jina la shetani, hivyo ndivyo maandiko yananyo niambia, maana hata wewe ukipanga mipango ya kwako kazi yake ni kumeza mipango mingine ya Falao, lakini siku ya leo fimbo ya Musa itameza fimbo ya falao.nataka nikubadilishe kuanzia leo uwe ni mtu wakuchukuwa neno  na kulituma.

Maana maandiko yanasema nimelituma neno likaokoe mataifa ,hivyo kudili na nguvu za giza unahitaji kuwa na ujasili, kwaamana chochote unacho kiogopa ndicho kitakacho kuharibia malengo yako na kukuuwa kabisa,hutakiwi kuogopa nguvu yoyote ile ya giza maana sisi ni nuru ya ulimwengu kwa maana nuru haingii katikati ya nuru bali inangaa katikati ya giza.

WAKOLOSAI 1:9 “Kwasababu hiyo sisi nasi,tangu siku ile tulipo sikia hatuachi kufanya maombi na dua kwaajili yenu, ilimjazwe maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote na ufahamu waroho”.

Neno yote katika andiko hili,nikufanikiwa katika ulimwengu waroho uwekamili, na kushindwa au kuto kufanikiwa sio kwa sababu hatuna Mungu, tatizo kubwa ni kukosa maarifa,maana maarifa ni matendo  yanayo kiumba kitu ilikiweze kutokea kwenye macho ya kawaida.







Monday, June 9, 2014




SOMO: UPANDE  B WA MUNGU USIO  UJUA.
Na: NABII FRANK  JULIUS  KILAWAH
Upande B huwa haufi wala haushindwi kama upande A, kama kuna mapito unayo pitia katika maisha yako tambua ya kuwa huo ni upande A, lakini mbele yako kuna upande B ambao Mungu ameuandaa kwa ajili yako ambao ni ushindi kwako, na hapo utakuwa wewe umezaliwa na mbegu isiyo haribika wala kufa.na kuzaliwa kwako ni kwa mara ya pili. Mana hata katika maandiko Mungu akamwambia Yoshua awapatie wayahudi upande B iliwaweze kujilinda na Israel kwamaana watakuwa upande B wenye nguvu.
YOSHUA 6:1,2 “Basi Yeriko ulikuwa umefungwa kabisa kwa sababu ya wana wa Israel; hapana mtu aliye toka wala hapana mtu aliyeingia , Bwana akamwambia Yoshua, Tazama, nimeutia Yeriko katika mkono wako, na mfalme wake, na mashujaa wake”.
Kwanini Yeriko ilifungwa, ni kwasababu ya mtu mmoja jina lake Izrael na haikufungwa kwaajili ya watu wote bali ni kwaajili ya huyo mtu mmjoja tu,na watu wa mji huo walikuwa hawawezi kutoka wala kuingia, na ukiuliza ni kwanini mlango umefungwa na wakajibu ni kwasababu ya mtu mmoja hatumtaki huyo Izrael, na milango hatuta fungu mpaka aondoke ndipo watu wataingia na kutoka.
Maandiko yanasema hapata kuwa na mtu wa kuingia wala kutoka, hapo lazima uelewe kwamba ni lazima mji uwe na mabadilishano ya fedha zinazo toka na kuingia na kama kuna upako itakua vivyo hivyo kama fedha,maana maandiko yanasema ni bora kutoa kuliko kupokea, kwa hiyo kuna milango ya kuingiza na  yakutoa, Lakini kibibilia milango ya kutoa ni muhimu sana kuliko ya kuingiza, hivyo kama utaenda kwa mtindo huo unaweza ukaelewa vizuri ni kwanini yeriko imefungwa kwaajili ya wana wa Izrael, na ukienda kwa mwendo huu pengine kwenye maisha ya kwako ya kawaida unaweza ukaelewa kabisa kunabaadhi ya vitu haviendi vizuri kwenye maisha yako si kwaajili ya watu bali na wewe mwenyewe hauwezi kutoka wala kuingia.
Hata hivyo hao wate waliokuwepo watasababisha vita na Yule mtu aliye sababisha milango kufungwa, kwa maana waliokuwepo ndani walikosa mahitaji kwaajili ya Izrael, hivyo nilazima kutakuwa na vita kubwa  kwaajili ya milango  kufungwa, na milango hiyo wayahudi wanataka kupita, na nguvu za mfalme wa Eriko kazielekeaza kwenye malango yake na kusema haruhusiwi mtu kupita wala kutoka. Mfalme wa eriko akasema peleka wanajeshi na fungeni hiyo milango mtu asiweze kutoka.
Lakini Mungu akamwamba Yushua waambie wayahudi wasibomoe milango na waiache kama ilivyo, bali wao wanachotakiwa kufanya maana upande A ndio wanaoujua hebu wapatie upande B wasio ujua, najua watachanganyikiwa, kwa maana maombi yao wanayofanya kwaajili ya kujilinda na waizrael wamepewa mpango na mbinu za upande A hawana mbinu za upande B na kwasababu hawana mbinu za upande B uwenauhakika hawajajipanga na kujikinga na upande B na itakapo anza kazi na kwasababu hawana upande wa B na hawapo makini na kitakacho tokea upande B bali wapo makini na kitakacho tokea kwenye mlango.

Hivyo basi Mungu akawambia hamhitaji  tena kupambana na milango ya eriko, Maandiko yanasema Mungu alimwambia Yoshua chukuwa makuhani, maana yake chukuwa  waombaji, ndani  yao wabebe sanduku la agano, maana maombi haya  hauwezi  ukaomba kama ndani yake hamna agano,  kama wataka nikusikilize ni kweli lazima uwe na makuhani lakini siwezi kukusikiliza mpaka mikononi  mwao  wawe na maagano,  ili mimi Mungu nitumie maombi yao ni changanye na agano ni weze kuwavusha wanapotakiwa kupita. “Mungu anasema mimi ni Mungu wa maangano na siwezi kuipiga eriko kwa sababu umeomba bali cha kufanya lazima uchukuwe agano ambalo nimewekeana na waizilaeli ndio naweza kuomba” .
YUSHUA 6:12 “Yoshua akaondoka asubuhi na mapema, nao makuhani wakalichuka sanduku la Bwana, Na wale makuhania  saba wakazichukuwa tarumbeta saba za pembe za kondoo waume mbele ya sanduku la Bwana. Wakaendelea wakazipiga tarumbeta; nao watu wenye silaha wakawatanguli na hao waliokuwapo nyuma wakalifuata sanduku la Bwana; makuhani wakazipiga tarumbeta walipokuwa wakienda”.
Mungu akamwambia Yushua kama unataka ufanikiwa upande B nenda na uchukuwe agano la Baba yako Ibrahimu weka ndani ya sanduku halafu nenda alfajili nitakuelekeza hilo agano linasema kitu gani na nitakapo kuelekeza utafanya sawasawa na hilo agano na ndipo nitakapo ifuta nchi yote ya Izrael.
Kama Mungu aliweza kuwazuia wasipite kwenye mlango wa eriko na miji mingine kwa sababu hao wameshapita kwenye mlango wa kwao na umesha wafungua kwasababu wao wametoka utumwani na walitoka kwa damu iliyo pakwa kwenye ile milango, na milango yote ilifungwa bali mmoja wa nyumba ya Falao ulikombolewa kwa damu ya wazaliwa wa kwanza ya wanyama na binadamu,na hata hiyo iliyofungwa wanajua imefunguliwa. Lakini maadamu  Yesu tunae mtumikia alikufa na hakutoka kwenye mlango bali alitoka ukutani, na hawa jaama wanasema tulipita kwenye mlango mara moja sasa tunapita kwenye ukuta.


Friday, June 6, 2014

JINSI YA KULINDA LANGO



ALHAMISI 05/06/2014

SOMO: JINSI YA KULINDA LANGO

Na: NABII FRANK JULIUS KILAWAH

Lango ni mlango wa kuingizia ama kupitishia vitu tofauti vizuri na vibaya,kiroho na kimwili,pia kwa maana nyingine ni Yule mtu anaye simama kwa miaba ya mafanikio yako. kikubwa ni kujua nani ni lango la kwako na unalilinda kwa kiasi gani,maana lango limebeba mafanikio ya maisha ya kwako kifedha na kiuchumi, bila kulitambua lango lako na kulilinda ni rahisi kupoteza kile kilichokuwa kinakuletea mafanikio katika maisha ya kwako.

Sijajua kama unaelewa ndugu zako ambao maisha yao yameharibika wakati wewe unamjua Mungu, uwe na uhakika Mungu atakudai maisha yao  mikononi kwako, sasa haimanishi atadai zambi zao mikononi mwako,si hivyo bali Mungu atadai maisha yao mikononui mwako.

Mungu alikuwa anaongea na Ibrahimu, na Ibrahimu alikuwa anaongea na Mungu, lakini maongezi ya Ibrahimu yalikuwa ni kupunguza ghadhabu ya Mungu aliyo ipanga kwaajili ya watu wa Sodoma na Gomola, Maana Mungu alikuwa ashapanga kwenda kuichoma ile Sodoma na gomola, maandiko yanasema Mungu alijadili mwenyewe  na kusema tumfiche Ibrahimu? Lakini baada ya hapo, akasema hapa siwezi kumficha kitu na akamua kumweleza.

MWANZO 18:16 “Kisha watu hawa wakaondoka huko wakaelekeza nyuso zao sodoma. Ibrahimu akaenda pamoja nao awasindikize.Bwana akanena, je! nimfiche Ibrahimu jambo nilifanyalo,Ikiwa Ibrahimu  atakuwa taifa kuu, hodari, na katika yeye mataifa yote ya dunia watabarikiwa”.

Bwana akasema , nikiona katika sodoma wenye haki hamsini mjini nitapaacha  mahali pote kwa ajili yao, Ibrahimu akaanza kusema wakiwepo wenye haki hamsini, Mungu akajibu sitapiga, na wakiwepo Arobain na tano, Pia akajibu hivyo hivyo mpaka ilipo fikia kwenye kumi, Mungu akamjibu sitopiga tena. Lakini Ibrahimu alipoishia hapo kwenye kumi, ndipo alipojiingiza  kwenye agano la Mungu  na  kutomsikilizwa tena,ndipo Mungu alimwambia Ibrahimu, sasa hivi nitasema mara hii moja tu wala sitaongeza kitu tena.

MWANZO 18:23 “Ibrahimu akakaribia,akasema je!  Utaharibu mwenye haki pamoja na mwovu? Huenda wakawapo wenye haki hamsini katika mji, utaharibu, wala hutaacha mji kwa ajili ya hao hamsini wenye haki waliomo? La  hasha usifanye hivyo, ukamuuwa mwenye haki pamoja na muovu, Hasha; Mhukumu ulimwengu wote msitende haki? ”.

Ibrahimu akauliza je! Ukikuta wenye haki kumi utawapiga, Mungu akasema nikiwakuta wenye haki kumi sitapiga sodoma wala gomola, Pengine Ibrahimu asingejiingiza kwenye lileagano
labda Mungu asinge weza kusema kuwa atasema mara hii tu. Mungu angetumia sentensi nyingine kwamba pia ni kiwakuta watano sitapiga, kwa kuwa Mungu alishashusha ghadhabu yake, basi angeweza  kusema kama kuna watu wa tano sitapiga tena. Ibrahimu alichokosea mbele ya macho ya Mungu aliishi watu kumi alishindwa kuhesabu ndugu yake Lutu ana watu wangapi katika nyumba yake ili kwa hao Mungu asiipige nchi.

Katika Dunia tuliokuwa nayo si watu wengi wanaelewa maandiko, bali watu wengi waliopo ni warahisi wa kukuza tatizo kuliko kujua maandiko, na ndicho kinacho fanyika kwenye maisha ya watu, kwa hali hiyo mzani wa maisha ya kwao ni kukuza tatizo sio kulikuza neono la Bwana na ndani mwao ni rahisi kulishusha likawa dogo.

Maandiko yana tuambia Ibrahimu alipoishia kwenye watu kumi angeweza kuendelea kulembele naamini Sodoma na gomola isinge chomwa moto, ndipo malaika na Mungu wakaondoka kwenye uso wa Ibrahimu, maandiko yanasema walipofika kwenye nchi ile ya sodoma wakaingia, lakini maombi ya Ibrahimu hayakumuokoa lutu. ikiwa watu wengi wamejijengea imani kwamba maombi ya Ibrahimu ndio yalimuokoa lutu kitu ambacho si kweli,maana hata katika nyumba ya mzee Ibrahimu hapakua na mtu mmoja bali walikuwepo watu wanne akiwemo yeye na mkewa na dada wawili.

Ghadhabu ya Mungu iliapa kama nikikuta watu kumi sitahukumu na maadamu hakuna watu kumi na maombi yako yameishia hapo hapo kwenye watu kumi, hukutaka kuendelea hivyo utakuwa umeungana na mimi Mungu kuhukumu ninacho kwenda kukihukumu, kwa sababu  nilikupa nafasi ya kunihoji  kuhusu adhabu na hukumu ninayo kwenda kuiachi, na umeishia mahali fulani na hukutaka kuendelea.

Kwa hiyo Ibrahimu alienda na kukaa na kufanya anayo ya fahamu na kuomba kwake kote akaishia kwenye watu kumi, na kushindwa kuelewa ndugu yake lutu anawatu wangapi nyumbani kwake na wote wanahitaji kuokolewa, Maandiko yanasema kilichomsaidia lutu alikuwa amekaa kwenye lango  la kuingilia mjini maana ndiye alikuwa anajua nani wa mwisho kutoka na kuingia kwa sababu alikaa kwenye lango la mji.

Na unatakiwa kujua ni kwanini Ibrahimu alikataa kukaa katikati  ya mji na akaamua kwenda kukaa kwenye lango la mji, na sijui kama watu wengi mnaelewa kwamba mtu aliyeokoka  hawezi kukaa katikati ya mji, nilazima akae kwView blogenye maingilio ya lango la mji maana ndio mlango wa kila kitu.

Thursday, June 5, 2014

NDOA NA MAHUSIANO



SOMO: NDOA NA MAHUSIANO
Na: NABII FRANK JULIUS KILAWAH

Ndoa, ni muungano kati ya mwanamume na mwanamke kuishi pamoja kama mume na mke muda wote wa maisha yao,na mpango na utaratibu wa Mungu umewekwa wazi katika kitabu cha MWANZO 2:18. “Bwana Mungu akasema,sivema huyo mtu awe peke yake nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye’’
.
Mungu hakuumba watu bali aliumba mtu, kwa maana hiyo Mungu aliumba mwanamume peke yake inamana alikuwa hana mpango wa kumuumba mwanamke, ni vizuri ukaelewa na kuwa na ufahamu juu ya uumbaji wa Mungu, iliuweza kujua mambo mengi, ndani ya Mwanamume ndio alikuwepo mwanamke, maandiko yanasema Mungu alipomaliza kuumba aliangalia kazi yake akaona ipo sawa na sahii mbele ya macho yake akaamua kupumzika.

Katika kitabu cha Mwanzo sura ile ya kwanza Mungu aliumba mtu kwa mfano wake, maana yake mwanamume na mwanamke washatokea.

MWANZO 1:26,27 ''Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi, Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimuumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba".

Tukisoma maandiko katika kitabu cha Mwanzo ile sura ya pili, inatuelezea hatua ya umbaji wa mwanadamu, maandiko ya nasema, mwanadamu ametoka katika udongo, lakini sura ya kwanza haijatuelezea ametoka wapi bali inasema tumfanye mtu kutoka katika sura ya kwetu na mfano wa kwetu, kwa hiyo sura ya kwanza unayoiona ni image ambayo Mungu alimtengenezea mtu kutoka kwenye sura, rangi na mfano wa kwake
.
MWANZO 2:7 “Bwana Mungu alimfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai. Bwana Mungu akampanda bustanii upande wa mashariki wa Edeni, akamweka ndani yake huyo mtu aliemfanya”.

Katika sura ya pili inamtengeneza mtu wa pili ambaye hatokani na sura ya Mungu wala rangi image na mfano wa Mungu, bali alimtengeneza kwa mfano wa nchi,maandiko yanatuambia Mungu alimuumba mwanamke na mwanaume kwa mfano wake,pia tumfanye hilo neno maana yake picha ya kwanza ya mwanadamu iliyopo kwenye sura ya kwanza mfano wake duniani haupo, bali unafanana na hao waliokuwa wamesema tumfanye mtu kwa mfano wetu na sura yetu hiyo ndiyo image.

Na ukisoma maandiko vizuri na kuyaelewa unaweza kujua kuwa aliye pulizia pumzi ya uhai kwenye udongo hakuwa Mungu, bali aliye pulizia pumzi ya uhai kwenye udongo, kwenye ile sura ya pili alikuwa ni huyu aliyeumbwa kwa mfano na sura ya nchi, kwa sababu katika sura ya kwanza inatuelezea amepewa mamlaka ya kuzaa na kuongezeka kwa hiyo alipokuja kwenye hii sura ya pili ya nchi umbaji wa Mungu haupo.

MWANZO 1:28 “Mungu akawabariki, Mungu akawaambia, zaeni,mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi”.

Sambamba na hayo umbaji wa sura ya pili, ni yule alieumbwa kwenye sura ya kwanza, ametokea kwenye sura ya pili sasa anataka kuzaa na kuongezeka na akajitoa na kujitengeneza mwili wa kwake, akaufanya na kuupulizia pumzi ya kwake na akajiita mwenyewe na akisimama akisema jina langu ni Adamu.